Mkuu SteveD,hawa watu ndiko wanakotupeleka.Kilichobakia ndani ya nchi yetu hii ni MOB JUSTICE. Utawala wa sheria kama unavyoelezeka kwenye vitabu na majukwaa ya siasa unahusiana na walalahoi pekee.
Kuna watu watachukizwa, watanuna na wataona nahimiza uvunjaji sheria. Lakini kilichobakia na kinachoonekana kila tunapoamka na kusoma matukio na yanayosemekana kupangwa ndiyo hayo.
Hata hivyo kuna pahala kadhaa hiyo habari juu haijitoshelezi. Kwamba,
Kitu kama hiki sidhani kinaweza kusukwa bila wao kufahamu. Kuna ulakini hapa.
Je, tumelogwa?
Wewe ni miongoni mwa Watanzania waliolala fofofo huku nchi ikiangamia. La sivyo ni mmoja wa watu wanaonufaika na ufisadi wa hawa watu. Kwa taarifa yako hawa mafisadi wamejipanga vizuri sana kwa kutumia udhaifu na ufinyu wa akili za watanzania walio wengi (utapima kama na wewe ni mmojawapo) kujaribu kujinasua na tuhuma nyingi zinazowakabili. Issue ni kwamba bado wana nia ya kutaka kuendeleza ufisadi, na hawawezi kufanya hivyo wasipokuwa kwenye power.
Mara baada ya kikao cha Bunge walikutana Mbozi, shambani kwa kigogo wa zamani wa Usalama wa Taifa, ambaye ni mtu wao. Walipanga kumng'oa Sitta na kumpachika mtu wao ili kazi kubwa ya Kwanza iwe kuwasafisha na tuhuma zote zinazowakabili na baadaye kuweka mikakati ya kutwaa urais.
Hili watu wa Usalama wa Taifa wanalijua, kama wanavyojua jinsi pesa zilivyotembea kwa wajumbe wa NEC kuanzia Z'bar, Dar es Salaam na baadaye Dodoma. Lakini kwa kuwa hakuna kinachofanyika, inabidi sisi wana wa nchi tujadili hatua za kuchukua... Au mnasemaje? Kama wote tutakuwa na mawazo kama ya huyu MTM na vibaraka wengine wa mafisadi nchi hii itaangamia. Amini amini nawaambia watu hawa hawana nia njema na nchi hii hata kidogo. Vizazi vijavyo vitatushangaa kwa utaahira wa kuiacha nchi ikiwa maskini licha ya kuzungukwa na resources ambazo zingetufanya tuwe miongoni mwa nchi tajiri katika bara hili la Afrika. Amkeni jamani...
Nimeona hiyo mapema tu mkuu, ndiyo maana nika comment hapo juu kuhusiana na jinsi ilivyo andikwa.
Lakini ninachoona mimi kinaifanya hii habari iwe na percentage kubwa ya ukweli ni mapokezi ya Mh. Sitta Urambo. What a parallel coincidence!!
mze punch, sijawahi unga mkono ufisadi, soma post zangu humu zaidi ya 1000; tatizo wewe umedandia treni kwa mbele kwa sababu ulitaka niandike utakavyo... Soma majibu yangu kwa steved na another fella huko page 2 ya hii thread... My worry is on strategies and not infomration... Too many fronts zinaleta dilution ya mikakati. Napenda this day na nasoma sana ripoti za humu jamvini!!! Na najifunza mengi, sikatai walikutana mbeya, na sikatai walikuwa na birthday party na sikatai wamepiga vita dhidi ya usawa na hekima na sikatai kwamba walimpinga sitta [thread ya fmes iko very clear] na pia sikatai ya ripoti ya meremeta
ninachokataa ni kwamba tusipoangalia, tutadilute efforts na kufanya ufisadi uwe kama ada, jaribu kuelewa between the lines, otherwise take it as you want
wanasema kabla hujamuelewa mtu, uliza kwanza
once again, i am clear in my stance and i would neva support fisadization because i am also a victim, wanaonijua watasema
It seems these guys (ThisDay) have got a very reliable source.
------------------------------------------------------------------
nimekupata mkuu, kumbe tupo pamoja. Unajua haya mambo yanaudhi kupita kiasi ndio maana wakati mwingine tunakuwa na jazba. Sorry, tuendeleze mapambano...
Kinachoshangaza ni courage ya watu kuhalalisha ubaya biya haya wala soni..
Mtu anakuibia na anajua kwamba unajua amekuibia lakini bado anakushawishi uamini kwamba hajakufanyia ubaya! Simply kwa sababu ameweza kuepuka mfumo wetu wa sheria.
Daa kweli nchi hii haina mwenyewe wale wote mafisadi wanathubutu kutaka tena uongozii kama ule wa speaker haahha yaani hata jumuia za kimataifa zinatushangaa sana kama Zimbabwe vile hatuna hata aibu....hivi hawa wajumbe wamekuwa na tamaaa na wamesahau hata wajibu wao kikatiba???yaani inaniuma sana hawa mafisadi....ila dawa yao inakuja
Uzuri wa haya yote, Mungu amekuwa upande wa wale wanaoitakia mema nchi hii. Ametuonyesha mapema kasoro za uongozo tulionao sasa angalau mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu ili tuweze kupima ni upi mchele kati ya pumba nyingi. Fikiria watu wapeane kiasi cha kati ya Tshs 4 - 5mill, ili kumwondoa mtu mmoja na bado wakashindwa, wataweza vipi kuwaaondoa walio wengi kwenye mapambano ya ufisadi hapo mwakani ikiwa wao wenyewe wako katika vita ya kujinusuru kutoswa kwenye sanduku la kura? Hakika CCM imeshindwa kusoma alama za wakati!
- Badala ya kuwepo Segerea where they belong, wapo bungeni na wanajaribu hata kuchukua u-Spika wa Jamhuri, only in Tanzania inawezekana haya mambo.
- Hii cancer ya Lowassa sijui tutaondokana nayo vipi na lini, maana inaonekana it is here to stay mpaka arudi kwenye power by any means necessary! Naona uamuzi ni wetu wananchi kumruhusu au kutomruhusu!
Mungu Aibarikie Tanzania!
Respect.
Field Marshall Es.
Jamani, naona sasa kama tunaanza kupoteza mwelekeo... tumekuwa too much "gossip mongers", kama ni kweli basi mtu kabla hajashare news awe tayari kutoa ushahidi!!
Mimi naona sasa tumekuwa tunatumika tu na waandishi wa habari wanaogeuza hata siasa na utawala wa nchi yetu kama novel na riwaya fupifupi ili wauze magazeti ambayo kwa sasa hayana tofauti kubwa na vitabu vya "someni kwa furaha" n.k.
Vita dhidi ya ufisadi itashindwa kama watanzania watakuwa na "too many fronts"!!!
Lets be focused on a few fronts [with evidence kama ripoti zilizofanyiwa uchunguzi] na kupambana kwenda mbele
KILA KITU KINAWEZEKANA CHINI YA JUA --- HATA MAENDELEO YA KWELI YA NCHI YETU
Wewe ni miongoni mwa Watanzania waliolala fofofo huku nchi ikiangamia. La sivyo ni mmoja wa watu wanaonufaika na ufisadi wa hawa watu. Kwa taarifa yako hawa mafisadi wamejipanga vizuri sana kwa kutumia udhaifu na ufinyu wa akili za watanzania walio wengi (utapima kama na wewe ni mmojawapo) kujaribu kujinasua na tuhuma nyingi zinazowakabili.
Mara baada ya kikao cha Bunge walikutana Mbozi, shambani kwa kigogo wa zamani wa Usalama wa Taifa, ambaye ni mtu wao. Walipanga kumng'oa Sitta na kumpachika mtu wao ili kazi kubwa ya Kwanza iwe kuwasafisha na tuhuma zote zinazowakabili na baadaye kuweka mikakati ya kutwaa urais. Hili watu wa Usalama wa Taifa wanalijua, kama wanavyojua jinsi pesa zilivyotembea kwa wajumbe wa NEC kuanzia Z'bar, Dar es Salaam na baadaye Dodoma. Lakini kwa kuwa hakuna kinachofanyika, inabidi sisi wana wa nchi tujadili hatua za kuchukua... Au mnasemaje? Kama wote tutakuwa na mawazo kama ya huyu MTM na vibaraka wengine wa mafisadi nchi hii itaangamia. Amini amini nawaambia watu hawa hawana nia njema na nchi hii hata kidogo. Vizazi vijavyo vitatushangaa kwa utaahira wa kuiacha nchi ikiwa maskini licha ya kuzungukwa na resources ambazo zingetufanya tuwe miongoni mwa nchi tajiri katika bara hili la Afrika. Amkeni jamani...
It seems these guys (ThisDay) have got a very reliable source.
UZURI ULIOPO SASA NI KWAMBA ndani ya ccm yenyewe hakuna siri tena, kila move wanayoianzisha gizani basi kwa kudura za mwenyezi MUNGU yanakuwa adharani,