Elections 2015 Lowassa: Je, alikosea wapi? Akiamua kuendelea, arekebishe wapi?

Elections 2015 Lowassa: Je, alikosea wapi? Akiamua kuendelea, arekebishe wapi?

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2007
Posts
4,850
Reaction score
9,434
Mchakato wa kutafuta mgombea urais kwa tiketi ya CCM umeshakamilika, na mgombea aliyepatikana ni John Pombe Magufuli. Pamoja na hayo, ukweli unabakia kwamba katika mchakato wa kutafuta wadhamini, ni Edward Lowassa ndiye aliyeungwa mkono na wanachama na makada wengi wa CCM kuliko mgombea mwingine yoyote.

Edward Lowassa aliungwa mkono na wanachama karibia milioni moja wa Chama Cha Mapinduzi. Pamoja na jina la Edward Lowassa kutorudishwa na vikao vya ngazi za juu ya CCM, kuelekea uchaguzi mkuu, suala la Lowassa kupata wadhamini karibia milioni moja ni suala ambalo halitakiwi kuchukuliwa kimasihara au kubezwa, kote - ndani na nje ya CCM. Kwanini tunasema hivyo:

1. Wadhamini hawa karibia milioni moja ni mchanganyiko wa wanachama na viongozi wa ngazi mbali mbali wa CCM. Wanatoka katika kona mbalimbali za Tanzania. Ni hawa ambao kwa kawaida, ndio wanaochukuaga jukumu la kumbeba na kumnadi mgombea urais (CCM) baada ya jina la mgombea kupatikana.

2. Kwa kuzingatia historia inavyotueleza, upinzani umeweza kunyakua makada wengi wa CCM baada ya makada hao kuenguliwa majina yao na vikao vya juu vya chama, licha ya makada husika kukubalika na kuwa chaguo la wanachama na makada wengi wa ngazi za chini. Kilichofuatia ni kwamba, CCM ilikuja kupoteza majimbo kadhaa kwa upinzani.

Kama ilivyotokea huko nyuma kwa makada kadhaa kuenguliwa katika vinyang’anyiro cha ubunge hivyo safari yao ya matumaini kuzimishwa na vikao vya juu vya CCM licha ya kukubalika na makada wengi wa ngazi za chini za CCM, hali hii imejitokeza kwa mara ya kwanza katika kinyang’anyiro cha kutafuta mgombea urais (CCM) ambapo, Safari ya matumaini ya Edward Lowassa kubeba bendera ya CCM (urais) 2015, Safari hiyo imezimwa rasmi na vikao vya juu vya chama cha mapinduzi. Je:

· Edward Lowassa alikosea wapi katika safari yake ya matumaini ndani ya CCM?

Na iwapo itatokea akashawishika kuendelea na safari yake ya matumaini kupitia chama kingine cha siasa kama ilivyotokea kwa makada wengine walioenguliwa kwenye vinyang’anyiro vya ubunge (CCM), ili kutimiza safari yake ya matumaini nje ya CCM, je:

· Edward Lowassa arekebishe wapi ili kufika safari yake ya matumaini nje ya CCM?
 
Uchu wa kupitiliza wa Madaraka + Namna mbaya ya kukabiliana na Changamoto + Fikra Potofu ya Pesa ni kila kitu + Kiburi kwa Viongozi Serikalini na Chamani + Wafuasi waliolewa mapesa na matumaini ya madaraka = Kuanguka Kwake.

Na kama akiyaendeleza hayo anaenda kuanguka zaidi ya hapa.
 
Kwa sasa Tanzania tunaweza bila CCM /Lowassa,tunahitaji chama mbadala na CCM ibaki ijikosoe pale ilipokosea.Ikilazimisha CCM itakufa bila hata kubaki mifupa ya kuwaonyesha watoto na wajukuu
 
  • Inashangaza kumuona Lowassa na mbinu zoote zile hakukumbuka kuwa kuna mbinu moja rahisi saaana na ya uhakika na ilikuwa ndani ya mikono yake ya kumuwezesha kuwa Rais hapo October lakini kwa miaka 10 hakuwahi kuifikiria wala kuiwaza wala kujua ana uwezo nalo hilo na kulifanyia kazi haraka.

    Sio tu Lowassa, mtu mwingine aliekuwa na nafasi tena mara mbili ya kuweka mazingira ya yeye kuja kuwa Rais hapo October na akachezea hizo 'golden chances' twice ni Samuel Sitta.

    October mtu pekee ambae ana mamlaka ya kutangaza Rais ni mwenyekiti wa tume ya uchaguzi....na mwenyekiti wa tume hii bahati mbaya hayuko huru kutoka nje ya CCM kutotangazwa.... laiti kama hii tume ingekuwa huru hilo lisingekuwa jambo gumu sana.

    Sasa why hii tume sio huru? kwa nini katiba haikubadilishwa na kuifanya hii tume iwe huru kabisa? Je Samuel Sitta hakuwa na madaraka ya kufanya hili? ya kusimamia mabadiliko tuupate tume huru? ambayo ingemuwezesha yeye Sitta kugombea Urais popote pale bila wasiwasi? iwe CCJ au CCM au CCK?

    Je Lowassa kwa nguvu aliyokuwa nayo hadi kuleta 'mtiti' ndani ya CCM angtumia nguvu yake yoote kuhakikisha tunapata tume huru kabisa ya uchaguzi angeshindwa?

    Akiwa Waziri mkuu?akiwa rafiki mkubwa wa Chenge alie draft katiba mpya? akiwa mtu mwenye support ya wabunge wengi wa CCM na upinzani? Why hakuliona hili? Sitta nae si ndo alikuwa mwenyekiti wa Bunge la katiba?na Spika wa Bunge la muungano? hawakuona hili kabisa?

    Hivi Lowassa akienda chama kingine halafu agombee na ashinde lakini tume imtangaze mtu mwingine
    atakuwa na haki ya kumlaumu mtu? hakuona kabisa hili?

    nuruyamnyonge likes this.

    There are things in life that are very difficult to explain....

    Edit Post Reply Reply With Quote Send PM
  • user-offline.png
    Ritz

    Today 09:39
    #216
    JF Tanzanite Member
    tanzanite.png
    Array

    Join Date : 1st January 2011
    Location : Republic of Nauru
    Posts : 36,194
    Rep Power : 95729989
    Likes Received17503
    Likes Given2175

    icon1.png

    quote_icon.png
    By Kigogo
    huyu mzee ahame CCM tu ndio kilichobaki

    Ahamie wapi UKAWA?​

EL kawaloga watumish had wamemsahau mwenyez mungu,na kutukanana wenyewe,makada nao wanachezeana rafu,bodaboda wamejaziwa wese.hata katilion ka1 hakajaisha,namuomba akapunzike sasa aliyeyafanya yanatosha.i
 
Atulie kama ni histolia ameiandika,asitoke ssm kwa heshima yake,anaweza akatunga vitabu kadhaaa akaeleza ukweli wa kila kitu ktk maisha yake.
 
1. Kashfa ya Richmond ndo imemponza Lowassa - regardless of namna alivyohusika. Na lawama anastahili yeye mwenyewe kwa hili. Richmond ulikuwa ni mchezo wa hatari kwake hata kama na wenzake waliwahi kucheza michezo kama hiyo na wakasitiriwa. He has only himself to blame on this one.

2. Ametoswa na serikali nzima ya sasa na iliyostaafu. Bado ana marafiki wengi lakini hawakuwa na "power" ya kumwezesha kutimiza career aspirations zake. Sasa ajifunze tu hata kwa umri huu alionao sasa kwamba binadamu hawaaminiki; hata marafiki zake ambao hakukutana nao "barabarani" wamethibitisha hilo kwa matendo yao. Alipaswa tu kuwa makini yeye mwenyewe badala ya kuwekeza kwa marafiki.

By the way, yaliyomtokea Lowassa liwe somo lenye manufaa kwa wengine.
 
Arudishe vile vyote ambavyo hakuvipata kwa njia halali ikiwamo ardhi ya kanisa kule Mbezi na nyingine tumeambiwa alipora huko Ngerengere
 
Kupendwa hakununuliwi. Kujenga taswira ya kupendwa kwa kutumia hela -hongo ya moja kwa moja kwa watu na kununua vyombo vya habari Inawezekana lakini mwishowe ukweli hutamalaki!
Kutokubali kwamba uwezekano wa kushindwa upo, kulimpofua.
Katika siasa,pesa husaidia lakini sio kila kitu.
Hata wanaopewa pesa hufika mahali wakaona aibu.
The best way forward kwa Laigwanani ni kustaafu siasa.
 
Ila watu tunajisahau kishenzi coz mwaka 2008 tu tulikua tunamuona Lowasa hafai kabisa ni fisadi wa kutupwa sasa leo hii msafi hv lini kasafika kwani yaan hata hatujiulizi hela anazomwaga ametoa wapi? Ni kweli zinatoka kwenye mshahara wa kazi yake ya ubunge?? CCM wamefanya maamuzi mazuri na mema kwa ajili ya mama Tanzania.
 
Siasa na Wanasiasa wa Tanzania hazina utamaduni wa kufanya post moterm evaluation ya kilichotokea, kwa nini ngwe Fulani mtu alishinwa au kuchukua mud kujisuka na kujpanga vizuri ili kuwa tayari kuyakabili magumu na misukosuko ya kujaribu kugombea. Hili si la wagombea Urais pekee, Lowassa, Malecela au Sitta. Ni hata wagombea ubunge. Ni kna kamba jina na nafasi pekee ni guarantee na self evaluation haifanyiki kurekebisha kasoro za awali.
 
Kama ni shika basi Lowasa alishika makali akaacha mpini. Alitakiwa kuwashika wazee washauri badala ya wajumbe wa kamati mbalimbali. Nafikiri naye anajua hawa hawaongeki na badala yakw ka deal na wajumbe wa vikao ambao ni rahisi kuwahonga na wengine kuwapa ahadi za madaraka. Hii inaonyesha Lowasa alitegemea misingi miwili katika mafanikio yake: pesa na mchakato mzima kufuata utaratibu wa kawaida. Alisahau alichofanyiwa siyo mara ya kwanza kama ilivyokuwa 1995 na alichofanyiwa Malecela mwaka 1995 ma 2005. Mi lwa maoni yangu hawa wazee washauri nguvu yao ni kubwa na wana uwezo wa kuitumia kirahisi tofauti na Lowasa alivyofikiri.
 
Mchambuzi

Alikosea pale tu alipoombewa na Gwajima mtu mwenye matusi anayejiita mchungaji,tayari alikuwa amewekewa mkosi wa kishetani kutoka kwenye mdomo mchafu usio na baraka za MUNGU.
kimsingi amepotea iliyobaki ni kuachana na
SIASA.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu

Wanamkakati wa Lowassa ima ni wachanga katika fani au hawajui nini cha kufanya. Hilo ndilo limemuengua edo mapema

1 Alinza kampeni za chini chini kwa mtindo wa mtandao wa 2005 akidhani mbinu hiyo haijulikani.

2. Akaendesha kampeni kabla ya muda, na kutoa muda wa wabaya wake kutafuta mahali pa kumshika

3. Akaamini nguvu ya senti zaidi ya nguvu ya hoja. Kaacha kiporo cha Richmond bila kujua kitakuwa ni tatizo

4. Aliamini anaijua system ya CCM, akapanga CC, NEC akijua mkutano mkuu ni kumalizia. Hakujua kamati za maadili na ile ya wazee wa chama zina nguvu kiasi gani. Aliamini shinikizo kupitia NEC linatosha kumvusha. Kosa

5. Mpango wa wadhamini uliendeshwa kitoto. Team iliamini watu wengi wangezuia kukatwa jina.
Hawakujua kuwa wanachama waliotakiwa ni 450.

Mbinu ya watu wengi ilikusudia kufunika matatizo ya Richmond kwa kuonyesha anakubalika licha ya matatizo aliyo nayo.
Kosa lilomgharimu

Kwa ufupi team nzima iliongozwa na mkakati usiokuwa na uhalisia. EL alitakiwa kwanza ahakiishe anamaliza Richmond.

Yaani akabiliane nayo kiasi watu wampe benefit of doubt. Alichokifanya kiliongeza wasi wasi hata kwa aliyekuwa upande wake.

Akaajiri watu wasiojua kazi katika media na blog, badala ya kumpaisha watu hao wakwa chanzo cha kukumbusha vidonda
Tumesoma mitandaoni na JF vijana wakija na hoja tu bila kujua wanatetea nini. Hawa vijana walimuumiza sana.

Team EL ilidhani kuwa na watu kila chombo na kila blog ingesaidia sana. Hawakujua kuwa ni lazima watu hao wawe effective, hata kama ni watu 3 wawe na uwezo wa kujenga hoja na kuzitetea.

Tumeshuhudia vijana wake waliburuzwa na hilo lilikuwa doa kwa mzee. Watu walipata habari zaidi ya walizojua kupitia '' anafaa, amejenga shule, ni mfuatailiaji etc'' huku akibomelewa vibaya na wenye weledi

Angalia, Membe alikuja kupangua Libya dakika za mwisho. Alikabiliana na ukweli na ilimsaidia kimkakati

Richmond, mipango mibovu, kutotumia watu wa mkakati ndivyo vimemuangusha.

Pesa inafanya kazi ikiwa na mkono mwingine, haifanyi kazi ikigawanywa kama njugu

Pigo alilokutana nalo ni kama lile la Sitta. Wote sasa ni majeruhi wa CCM na ndio mwisho wa safari ya kisiasa.
 
Mkuu Nguruvi3,

Umechambua Vyema Sana. Naomba nikuulize maswali matatu:

1. Akiamua kuhama ccm na kwenda upinzani, Nini itakuwa athari kwake kisiasa?

2. Akiamua kuhama ccm na kwenda upinzani, Nini itakuwa athari kwa chama atakachohamia?

3. Akiamua kuhama ccm na kwenda upinzani, Nini itakuwa athari kwa chama chama cha mapinduzi?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom