Maswali mazuri sana haya Mchambuzi.
- Nafikiri CCM hawamwoni EL kama "individual" bali wanamwona EL kama "organization" mpya ndani ya chama chao.
- Hivyo naona CCM strategist wana-contain EL waves kama wanavyocontain waves zingine zinazotishia usalama wa taifa.
Tofauti na fikra za wengi kuwa EL ni tishio kwa CCM wao CCM wanamwona EL kuwa ni tishio LA usalama wa taifa.
Kama kweli Lowassa ni tishio la Usalama wa Taifa kama walivyokuwa Makaburu, Nduli, Walanguzi na vitu vingine, Lowassa angekuwa Segerea au Ukonga siku nyingi sana, tangu 1995.
Kwanini kama Lowassa alikuwa ni mhuni na mwivi, pale Nyerere alipomtukana 1995 kuwa ananuka harufu ya rushwa, hakuchukuliwa hatua bali Mkapa alimpa uwaziri na mbaya zaidi alipitishwa na chama kuwalikisha jimbo la Monduli?
Kwa nini kama tuhuma za Richmond (ukiondoa matumizi mabaya ya madaraka) zinalenga rushwa na ufisadi, kwa nini CCM na Serikali yake ziliachia akachaguliwa 2010 Monduli na Rais Kikwete alikwenda mpigia kampeni?
Kwa nini Lowassa kama aliendelea na uhuni akakiuka kanuni za chama, alifutiwa kifungo cha kuanza kampeni mapema na kuruhusiwa kuchukua fomu?
Je huko mikoani Lowassa alipokusanya kura karibu 20% ya wanachama wa CCM, iweje tuendelee kuamini ana uwezo wa kuhonga watu milioni moja, na tuna vyombo vya usalama wa taifa na sheria (TISS, PCCB, Polisi, DPP) ambao wangeweza kuleta ushahidi na mashitaka ya ukiukwaji wa kanuni na rushwa dhidi yake?
CCM na uongozi wake inataka kutuaminisha kuwa sasa wameinamisha mtungi na wamekamata panya au wamechinja kope kwa utaratibu, hilo ni changa la macho, tena ni dhihaka kubwa sana kwa Watanzania.
CCM ndi ililelea na kumruhusu LOwassa akawa jinamizi, mzoga, shombo, zimwi na walimfurahia na walinogewa na yote aliyofanya, kwa maana yeye ni kama wao. Tofauti kubwa ni kuwa Lowassa yeye tumbo lake lilikuwa kubwa zaidi na njaa yake na kupenda nguvu zaidi haikuwapendeza wao.
Hapo nitakubali yeye kama mfumo ni hatari kwa usalama wa Taifa kwa mtaji a hatari ndani ya CCM na kuepusha machafuko ndani ya CCM na CCM kupoteza madaraka, hivyo basi ni kuhatarisha usalama wa Taifa.
Kama CCM inataka haki, imfukuze uanachama, Serikali ya CCM imfungullie mashitaka ya tuhuma walzozipata kwenye kikao cha maadili kilichimchuja jina lake, ili ukweli ujidhihiri, mfumo na organization unayoisema kuwa ni hatari kwa usalama wa Taifa ukamatwe na ufutwe kabisa bila kuruhusu chembe moja wa upuuzi huu kujirudia au kujitutumua na kugangamala kama Lowassa alivyofanya.
Kuna viji-Lowassa vingi sana ndani ya CCM, walichofanya ni kumpa sumu nyangumi, Papa, Kasa, Taa, kambale, na dagaa bado wako wengi sana kutokana na mfumo ambao unakumbatiwa na kupewa baraka na uongozi wa juu wa CCm.