Lowassa Kuanzisha ABC Television Arusha

Lowassa Kuanzisha ABC Television Arusha

nyinyi watanzania mna laana, na hamuendi popote, Lowassa hajawahi kuiba hata Pipi, alikuwa kiongozi pekee mkali kwelikweli na hana huruma wa uoga kwa vitambi au vigogo, bila kiongozi kama huyu hamna maendeleo africa hasa Tanzania, viongozi wetu asubuhi badala ya kuwa na tumbojoto ya majukumu yetu, wana tumbojoto baada ya kuvimbiwa chai heavy, na mda si mrefu lunch babkubwa na ....
Lowassa asiwekeze kwenye Media? awekeze mkenya au mhindi ndio mtafurahi? au mnapenda kuangalia CNN ya bwana R. Madorck? au mnapenda tuendelee kubembelezewa ujinga na mambo kidini yaliyopitwa na wakati na hako ka TBC ambocho kinasababisha watanzania wengi kupenda kuangalia channel za kigeni? haya tv hamtaki, akilima? akijenga? akiendelea na siasa na hatimae kuwa rais na mnajua atashinda tu akiamua? au auwawe ili asisahaulike kama kaka yake na jirani yake aliyemwachia kiti cha ubunge Monduli? angekuwa si msafi jimboni kwake yangetokea haya maajabu ya Loliondo? poleni watanzania, kama vipi wapeni wazenji nafasi japo wajaribu bila umbea wenu, wao walimpenda sana Lowassa, na alikuwa akiwatembelea kila miezi kadhaa, naona Pinda hatii mguu Zenji? sijui anaogopa popobawa?

Kweli akutukanae hachagui tusi.
 
...Booty-Licker!
 
Source:

Daily News, Friday, 24th October 2008, Page 22.

Public Notice

Application for Content Services Licences (Broadcasting Licences) to TCRA.

Name of Station:
ABC Television
P.O. Box 11843
Arusha

Shareholders:
Robert Francis Lowassa (Tanzanian) - 60%
Elias Stephen Kordun Lukumay - 40%

Who is Robert Francis Lowassa and Elias Lukumay?

Source: www.parliament.go.tz/Polis/PAMS/Docs/HS-4-44-2006.pdf

BUNGE LA TANZANIA
________
MAJADILIANO YA BUNGE
________
MKUTANO WA NNE
Kikao cha Arobaini na Nne – Tarehe 16 Agosti, 2006
(Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi)
. . . . . .
SPIKA: Sina shaka mtakubaliana nami Waheshimiwa Wabunge kwamba, hiyo ni hoja kabambe ya kuahirisha Bunge. Kabla sijawahoji, kuna matangazo mafupi yafuatayo:-

Napenda tutambue kuwepo kwa familia ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mama Regina Lowassa, Bwana Fred Lowassa, Bwana Robert Lowassa na Master, kwa hiyo, huyu ndiyo mdogo mdogo tu Richard Lowassa. Wale ambao mmeshiriki vizuri kwenye Bunge na mnahudhuria mara kwa mara, mtakumbuka kwamba, Richard si mgeni sana, hapa kwa sababu mara kwa mara tunaonana naye pale nje, sielewi Mwenyezi Mungu, mambo haya sijui yanakuwaje? Hatujui hatma ya Richard, lakini Mungu aendelee kumsaidia inaelekea anapenda sana Bunge. Pia marafiki zao Bwana John Bakilana na Bwana Elias Lukumai. Karibuni sana na ahsante kwa ushiriki wenu.

. . . . . .[/B][/COLOR][/SIZE][/FONT]

Lisemwalo lipo "RICHARD wa MONDULI= RICHMOND".
Watanunua vyombo vyote vya habari lakini hawata weza kununua ufahamu wa watu wote!
 
Big up Lowassa,wakati mwigine i see the good side of you,creativity na ujasiri,if kwa nia njema nakutakia kila la kheri katika uwekezaji wako.
 
Now kwenye hoja:

Kama mtu ameamua kuanzisha biashara yake nihaki yake kwa kadiri ya kwamba biashara hiyo imeanzishwa kihalali na fedha zilizotumika ni za halali. Hadi hivi sasa sijaona madai kuwa hawa jamaa wametumia kwa namna yoyote fedha za serikali au nafasi ya kisiasa ya Lowassa kujipatia leseni hiyo au mtaji wa biashara yao.

Lakini vile vile, hatuwahukumu watoto moja kwa moja kwa makosa ya wazazi wao isipokuwa kama watoto hao wanatumika na wazazi wao kuficha madhambi yao. So, kwenye hili mimi sijui hawa jamaa wanabiashara gani nyingine ya kuweza kuwapatia kipato cha kuweza kuanzisha televisheni. Kama uwezo huo wanao kibiashara basi ni haki yao kama mtanzania yeyote mwenye uwezo, kipaji na nia ya kutumia uwezo huo kujipatia mlo wa kila siku.

Vinginevyo, endapo kuna tetesi zenye kuashiria kuwa fedha hazikupatikana kihalali, utaratibu wa leseni haukufuatwa au sheria zimepindwa au kuvunjwa katika mchakato mzima basi vidokezwe. Vinginevyo, ABC kama zilivyo shughuli nyingine itapimwa kwa matunda yake, na tutaipima kwa kadiri inavyotumika aidha katika kupinga ufisadi, kutetea utawala bora na utawala wa sheria au kama itatumika kinyume na hayo. Hapo ndipo hukumu ya wananchi inapaswa kutolewa.

Kwa sasa nawapa asilimia 100!
Pesa za kuanzisha TV amechangiwa na RAFIKI zake.
Pili, Zile anazopeleka makanisani na misikitini nadhani mwenyezi mungu anazibariki zinazidi kuzaa.

Tatu, wanasema hivi mwizi si yule aliyekula nyama ni yule aliyekamatwa na ngozi. Lowassa alifanikiwa kutupa ngozi ndiyo maana hakuwa na gamba la kumvua.

Sijui tunaelekea wapi maana nduguye Lowassa ameshatoa ultimatum wachaga waondoke Arusha.
Nadhani TV itasadia sana katika kuhamasisha uondoaji wa Wachaga mjini Arusha. Hivi Wapare nao walitajwa au?

Superman, i like the way you have connected the story.
 
nisehemu ya maendeleo pia, mimi sina lakini sichukii wengine wakiwa nacho, sio mbaya nako Arusha kukawa na tv, baada ya star tv kule mwanza, dar , dtv , zije na nyingine nyingi tu, nchi huru hii
 
Mimi namuunga mkono sana mheshimiwa wanaosema yeye mwizi,mbona sijaona kesi hata moja mahakamani,kama wana ushahidi wa2 wapige kazi acheni majungu m2 akiwa na fedha mchawi,ni masonic,ni mwizi wengine hawawekezi hapa nchini acheni ushabiki na ulevi wa fikra mwenye contact zake naombeni nataka kuwasiliana na mzee.Big up white hair 4 investing in u'r homeland.
 
Bora mwizi ambaye mwisho wa cku anafungua vitega uchumi nchini kwake na hivyo kutoa àjira sambamba na kulipa kodi. CCM wengi wameiba, wamefanya nini cha kukumbukwa? Mkapa àlienda kujenga kwa mandela, chenge alienda kuficha Jersey, balali kaenda kujitangazia kifo marekani. Si bora Lowasaànawekeza nchini?
 
Hiyo Tv inaanza lini kufanya kazi....? Au ilikuwa danganya toto...Wanaojua mchakato wake tafazali tufahamisheni...
 
Wakuu...
Hii TiiVii mbado tu?! Tafadhali anayejua update atufahamishe.
 
Inawezekana walimbania leseni. Ila hawakufanya poa kubania kama kweli coz hii tiivii ingeleta ajira kwa watz wengi. Pia kwa jiji kama la Arusha na hadhi yake linahitaji tv station kwa kweli. TCRA wafikirie upya kuwapa leseni hawa jamaa.
 
Arusha kwa sasa inahitaji TV stations mji umetanuka, habari ni nyingi sana
 
Mi nalia na ajira tu. Watu wana roho za kwanini hata kwa raia wema wenye shida ya ajira.
 
Back
Top Bottom