Kisheria wabunge hawapaswi kupigiwa saluti. Na kama hiyo inafanyika ni makosa au mazoea ambayo yamefanywa kuwa ni kawaida. Isipokuwa, kuna exceptional cases ambapo mbuge ni afisa mstaafu wa jeshi. Kawaida maafisa wastaafu hubaki na vyeo vyao. Wanachopumzika ni utumishi katika jeshi, na ndo maana wanakuwa kwenye "reserve army", akiitwa kama kuna dharura ya vita anarudi kutumika akiwa na cheo kile alichokuwa nacho wakati anastaafu kwa hiyo akikutana na afisa ambaye bado yuko in-service, kwa kuzingatia seniority, atapigiwa saruti. Viongozi wa serikali wanaopigiwa saruti na wanajeshi ni hawa wafuatao
1. Rais na amiri jeshi mkuu
2. Makamu wa Rais
3. Waziri Mkuu
4. Mawaziri wote wa serikali
5. Wakuu wa mikoa
6. Wakuu wa wilaya
7. IGP (Hapa ni kutegemeana na seniority ya vyeo katika jeshi, NCOs wanampigia saluti IPP na Commissioned Officers to the rank of Junior Officers (Luteni-Usu hadi Major (sina uhakika sana).
8. Mawaziri wakuu wastaafu (?), Rais Mstaafu, Makamo wa rais mstaafu.
9. Retired CDF na Maafisa wote wastaafu kwa seniority ya vyeo vyao walivyokuwa navyo.
10. Maiti (Maiti au Marehemu hupigiwa saluti na askari wote bila kujali cheo alichokuwa nacho), hii kwa taratibu za kijeshi.
11. Chief Justice (Hapa sina hakika kama naye anapigiwa saluti), ila polisi humpigia.
12. Mahakamani na Bungeni askari hupiga saruti kwa sababu ya "coat of arms" ya serikali inayokuwemo ndani ya Bunge na Mahakamani.
Kwa hiyo wabunge si miongoni mwa wanaopigiwa saluti, isipokuwa tu pale huyo mbunge ni afisa mstaafu wa jeshi.
Nadhani wengine pia wenye kukumbuka haya mambo tuelimishane. Naamini wale tuliopita JKT bado tunayo kumbukumbu. Niko tayari kusahihishwa kama kuna mahali kuna makosa.
Mkuu ngereja hapa umetoa jibu sahihi sana. Wabunge hawamo katika wanaopigiwa saluti, na hata walipoleta mjadala kama huo bungeni, haukufikia muafaka (hawakuleta kama hoja, bali ilikuwa mjadala katika hoja nyingine).
Kwenye list ya junior commissioned officers, unaishia kwa Captain. Saluti pia hupigwa kwa alama za Taifa ambazo ni bendera, ngao ya taifa na wimbo wa taifa unapoimbwa. Kwa hiyo ukiona askari anapiga saluti mahakamani, bungeni etc hampigii hakimu wala wabunge, anapiga kwa heshima ya alama zile zinazowekwa mle. Na si kwamba saluti zinapigwa tu popote zinapoonekana alama hizo (mfano ngao ya taifa kwenye barua, au ukikutana na mashabiki wa michezo wanaonyesha uzalendo kwa kukimbia na bendera, wengine hata wanaivaa), kuna utaratibu wake ambao umewekwa wazi katika majeshi na miongoni mwa wanajeshi.