Elections 2015 Lowassa kuzungumza na wanahabari baada ya kumaliza kikao kizito na familia pamoja na marafiki zake

Elections 2015 Lowassa kuzungumza na wanahabari baada ya kumaliza kikao kizito na familia pamoja na marafiki zake

Kabwena

Senior Member
Joined
Jun 17, 2013
Posts
103
Reaction score
55
Mwanasiasa Edward Ngoyai Lowassa ambaye yupo katika sintofamamu na chama chake CCM atazungumza na waandishi wa habari leo au kesho nyumbani kwake Masaki jijini Dar es salaam iwapo atawahi kumaliza kikao na familia yake.

Taarifa kutoka kwa marafiki wa karibu wa mtoto wa Lowassa Fredy Lowassa ambaye alikuwa kiungo muhimu katika kampeni zake za kuelekea Urais kwa tiketi ya CCM zinaarifu kuwa Lowassa alianza kwa kufanya mazungumzo ya kina na familia yake huku katika kikao hicho Watoto wake wote wakihudhuria lakini pia wakwe zake akiwemo Sioi Sumari na kukubaliana baadhi ya mambo.

Mambo yanayodaiwa kukubaliwa na wanafamilia hao ni kwamba wawe tayari kumfuata katika chama chochote atakachoamua kuelekea, huku akishindwa kubainisha ni wapi atakapoelekea kwani alisisitiza kuwa hawezi kuhama au kutangaza uamuzi wowote pasipo kushauriana na marafiki zake wa karibu.

Hivi sasa waandishi wa habari wamefika nyumbani kwake Masaki hata hivyo wameombwa kuondoka na kuwa na subira kwani Lowassa bado anafanya mazungumzo na marafiki zake muhimu. mashuhuda kutoka eneo la tukio wanadai moja kati ya magari ya watu waliopo Nyumbani kwa Lowassa yameonekana kuwa ni yavmwenyekiti wa ccm wanawake taifa Sophia Simba, Lawrance Kago Masha, Adam Kimbisa, Emmqnuel Nchimbi, Mwenyekiti wa vijana taifa ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Donge zanzibar Sadifa Khamis, Hussein Bashe, Absolomon Kibanda, Khamis Mgeja(mwenyekiti ccm Shinyanga) Msukuma(mwenyekiti ccm Geita), Na Mgana Msindai(mwenyekiti CCM Singida).

===================

UPDATE: 12:40hours

Lowassa kaahirisha kuongea hadi taarifa zaidi itakapotolewa
.
 
Mzee Lowassa

Natumaini unaendelea kujikongoja baada ya a bitter defeat. Lakini nikukumbushe - haya pia yatapita. Mwisho wa siku yote yatapita.

Kumbuka -Jambo la muhimu kuliko yote kwa mtu yoyote ni familia. Bado unayo familia yako iliyo kuwepo na itakayokuwepo.

Kumbuka - Bwana ndio mchungaji wako hutapungukiwa na chochote

Madhumuni ya barua hii ni kukumbusha kile kitabu maarufu cha THE ART OF WAR BY SUN TZU.

Katika kitabu kile Tzu anaandika kuwa, you must know how to choose your battles and you must choose your battles carefully. Sio kila vita lazima upigani. Zingine ziache zipite.

Katika issue hii ya urais, you have won some battles and you have lost battles. But overall you are loosing the WAR.

Nakushauri uache sasa. Usiendelee kupigana. You are loosing the WAR!

Iache vita hii ipite Mzee.
 
Akimaliza hayo mazungumzo mtujulishe.
 
Hana tena nguvu ni sasa sawa na joka la kibisa halina tena sumu.
 
Aende act akagombee uraisi chochote kinawezekana akatimize ndoto zake,ikiwa ndoto yake ni kugombea uraisi.
 
Ngoma inogile!
Mimi nasema Lowasa aende chama chochote isipokuwa vinavyounda UKAWA, hasa CHADEMA asijaribu. Na kweli akienda huko UKAWA utakuwa umemaliza kazi. Vita vitakuwa kati ya CCM Magufuli na (ACT, nk., yaani CCM Lowasa).
Namwombea afya njema, walau afike mwisho wa kampeni, na ashuhudie akipigwa chini kwa aibu hapo Oktoba.
Kwa maoni yangu, Lowasa ni past-tense. Magufuli na CCM yake wanaandaa kukusanya virago vyao ili waiache Ikulu salama. UKAWA ndiyo habari kwa sasa.
 
Dah, nakuhakikishia mtu akitengeneza muv ya hii mambo mpaka Rais atakapopatikana october itauza mbaya.

Tunaamini mzeee wetu ana maamuzi magumu tunayasubiria. Ila ajue akienda ACT hawezi chomoka atakuwa amejimaliza kisiasa kabisa, maana hao bado sana. Na CCM watapita kirahisi sana.

Kama anampango wa kuiangusha CCM ajiunge tu na UKAWA, maana wana nguvu kubwa bado wakipata nguvu nyingine kidogo CCM chali,,
 
Namuunga mkono 100% ... JK amemfanyia Uhuni .... Mtaji anao wakutosha, Sababu anazo, nia anayo .... Hakika CCM itapasuliwa tu ...
Mwanasiasa Edward Ngoyai Lowassa ambaye yupo katika sintofamamu na chama chake CCM atazungumza na waandishi wa habari leo au kesho nyumbani kwake Masaki jijini Dar es salaam iwapo atawahi kumaliza kikao na familia yake.

Taarifa kutoka kwa marafiki wa karibu wa mtoto wa Lowassa Fredy Lowassa ambaye alikuwa kiungo muhimu katika kampeni zake za kuelekea Urais kwa tiketi ya CCM zinaarifu kuwa Lowassa alianza kwa kufanya mazungumzo ya kina na familia yake huku katika kikao hicho Watoto wake wote wakihudhuria lakini pia wakwe zake akiwemo Sioi Sumari na kukubaliana baadhi ya mambo.

mambo yanayodaiwa kukubaliwa na wanafamilia hao ni kwamba wawe tayari kumfuata katika chama chochote atakachoamua kuelekea, huku akishindwa kubainisha ni wapi atakapoelekea kwani alisisitiza kuwa hawezi kuhama au kutangaza uamuzi wowote pasipo kushauriana na marafiki zake wa karibu.

hivi sasa waandishi wa habari wamefika nyumbani kwake Masaki hata hivyo wameombwa kuondoka na kuwa na subira kwani Lowassa bado anafanya mazungumzo na marafiki zake muhimu. mashuhuda kutoka eneo la tukio wanadai moja kati ya magari ya watu waliopo Nyumbani kwa Lowassa yameonekana kuwa ni yavmwenyekiti wa ccm wanawake taifa Sophia Simba, Lawrance Kago Masha, Adam Kimbisa, Emmqnuel Nchimbi, Mwenyekiti wa vijana taifa ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Donge zanzibar Sadifa Khamis, Hussein Bashe, Absolomon Kibanda, Khamis Mgeja(mwenyekiti ccm Shinyanga) Msukuma(mwenyekiti ccm Geita), Na Mgana Msindai(mwenyekiti CCM Singida).
 
Huyo sasa kwishney! Akithubutu kuhama chama ndio atakuwa amejimaliza zaidi. Wenzake wanamsubiri kwa hamu ili waanike uozo wake waliokuwa wanamfichia.
 
Ramadhan Madabida yupo kwenye hiko kikao? ''Lowasa ni kama Mtume Mohamad''
 
Lowassa ni mtu wa watu,kama anataka kuhama basi aje UKAWA ila akienda kwingine atapotea kabisaaaaaaaaaa!
 
Mzee Lowassa

Natumaini unaendelea kujikongoja baada ya a bitter defeat. Lakini nikukumbushe - haya pia yatapita. Mwisho wa siku yote yatapita.

Kumbuka -Jambo la muhimu kuliko yote kwa mtu yoyote ni familia. Bado unayo familia yako iliyo kuwepo na itakayokuwepo.

Kumbuka - Bwana ndio mchungaji wako hutapungukiwa na chochote

Madhumuni ya barua hii ni kukumbusha kile kitabu maarufu cha THE ART OF WAR BY SUN TZU.

Katika kitabu kile Tzu anaandika kuwa, you must know how to choose your battles and you must choose your battles carefully. Sio kila vita lazima upigani. Zingine ziache zipite.

Katika issue hii ya urais, you have won some battles and you have lost battles. But overall you are loosing the WAR.

Nakushauri uache sasa. Usiendelee kupigana. You are loosing the WAR!

Iache vita hii ipite Mzee.

Nadhani si sahihi kutoa ushauri wenye koamrisha
 
Back
Top Bottom