Elections 2015 Lowassa kuzungumza na wanahabari baada ya kumaliza kikao kizito na familia pamoja na marafiki zake

Elections 2015 Lowassa kuzungumza na wanahabari baada ya kumaliza kikao kizito na familia pamoja na marafiki zake

Mwanasiasa Edward Ngoyai Lowassa ambaye yupo katika sintofamamu na chama chake CCM atazungumza na waandishi wa habari leo au kesho nyumbani kwake Masaki jijini Dar es salaam iwapo atawahi kumaliza kikao na familia yake.

Taarifa kutoka kwa marafiki wa karibu wa mtoto wa Lowassa Fredy Lowassa ambaye alikuwa kiungo muhimu katika kampeni zake za kuelekea Urais kwa tiketi ya CCM zinaarifu kuwa Lowassa alianza kwa kufanya mazungumzo ya kina na familia yake huku katika kikao hicho Watoto wake wote wakihudhuria lakini pia wakwe zake akiwemo Sioi Sumari na kukubaliana baadhi ya mambo.

mambo yanayodaiwa kukubaliwa na wanafamilia hao ni kwamba wawe tayari kumfuata katika chama chochote atakachoamua kuelekea, huku akishindwa kubainisha ni wapi atakapoelekea kwani alisisitiza kuwa hawezi kuhama au kutangaza uamuzi wowote pasipo kushauriana na marafiki zake wa karibu.

hivi sasa waandishi wa habari wamefika nyumbani kwake Masaki hata hivyo wameombwa kuondoka na kuwa na subira kwani Lowassa bado anafanya mazungumzo na marafiki zake muhimu. mashuhuda kutoka eneo la tukio wanadai moja kati ya magari ya watu waliopo Nyumbani kwa Lowassa yameonekana kuwa ni yavmwenyekiti wa ccm wanawake taifa Sophia Simba, Lawrance Kago Masha, Adam Kimbisa, Emmqnuel Nchimbi, Mwenyekiti wa vijana taifa ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Donge zanzibar Sadifa Khamis, Hussein Bashe, Absolomon Kibanda, Khamis Mgeja(mwenyekiti ccm Shinyanga) Msukuma(mwenyekiti ccm Geita), Na Mgana Msindai(mwenyekiti CCM Singida).

Huu ni ujumbe wangu kwa wale wote wanao dhani wanahaki sana na taifa hili kwa kutumia fedha zetu na mali zetu ilikufanikisha mambo yao nataka kuapa mbele ya Mungu alie tupa taifa hili kutoka mikononi mwa baba wa taifa hayati Mwl Nyerere nasema mbinu zenu ovu na za hatari ktk mustakabali wa amani yetu mtaenda nazo kaburini pasipo kutimia nchi yetu ipo imara na mataifa rafiki tena makubwa duniani wapo nasi kutulinda. mkumbuke wazalendo ni wengi kupita wasio na mapenzi mema na taifa hili mbinu zenu zote zipo wazi kama mtu alie uchi mbele ya watu nasema hamuwezi hamuwezi kutuaribia amani ya taifa hili watanzania tupo pamoja na serikali yetu na kama ni vita tupo tayari kuhakikisha tunakuwa na kizazi kitaogopa mambo maovu, idara zote za nchi zipo macho nasema hazilali mpaka mwisho wa taifa hili kama upo....
 
Ana nini huyu nae jogoo wa kuchora tu. Hawiki hadonoi mbwembwe nyiiingi kakalishwa chini. Huyu mzee atulie ajiuguze tu
 
Mzee Lowassa

Natumaini unaendelea kujikongoja baada ya a bitter defeat. Lakini nikukumbushe - haya pia yatapita. Mwisho wa siku yote yatapita.

Kumbuka -Jambo la muhimu kuliko yote kwa mtu yoyote ni familia. Bado unayo familia yako iliyo kuwepo na itakayokuwepo.

Kumbuka - Bwana ndio mchungaji wako hutapungukiwa na chochote

Madhumuni ya barua hii ni kukumbusha kile kitabu maarufu cha THE ART OF WAR BY SUN TZU.

Katika kitabu kile Tzu anaandika kuwa, you must know how to choose your battles and you must choose your battles carefully. Sio kila vita lazima upigani. Zingine ziache zipite.

Katika issue hii ya urais, you have won some battles and you have lost battles. But overall you are loosing the WAR.

Nakushauri uache sasa. Usiendelee kupigana. You are loosing the WAR!

Iache vita hii ipite Mzee.

Ushauri mzuri kwakweli.
 
you must know how to choose your battles and you must choose your battles carefully. Sio kila vita lazima upigani. Zingine ziache zipite.

Katika issue hii ya urais, you have won some battles and you have lost battles. But overall you are loosing the WAR.
 
Mwanasiasa Edward Ngoyai Lowassa ambaye yupo katika sintofamamu na chama chake CCM atazungumza na waandishi wa habari leo au kesho nyumbani kwake Masaki jijini Dar es salaam iwapo atawahi kumaliza kikao na familia yake.

Taarifa kutoka kwa marafiki wa karibu wa mtoto wa Lowassa Fredy Lowassa ambaye alikuwa kiungo muhimu katika kampeni zake za kuelekea Urais kwa tiketi ya CCM zinaarifu kuwa Lowassa alianza kwa kufanya mazungumzo ya kina na familia yake huku katika kikao hicho Watoto wake wote wakihudhuria lakini pia wakwe zake akiwemo Sioi Sumari na kukubaliana baadhi ya mambo.

mambo yanayodaiwa kukubaliwa na wanafamilia hao ni kwamba wawe tayari kumfuata katika chama chochote atakachoamua kuelekea, huku akishindwa kubainisha ni wapi atakapoelekea kwani alisisitiza kuwa hawezi kuhama au kutangaza uamuzi wowote pasipo kushauriana na marafiki zake wa karibu.

hivi sasa waandishi wa habari wamefika nyumbani kwake Masaki hata hivyo wameombwa kuondoka na kuwa na subira kwani Lowassa bado anafanya mazungumzo na marafiki zake muhimu. mashuhuda kutoka eneo la tukio wanadai moja kati ya magari ya watu waliopo Nyumbani kwa Lowassa yameonekana kuwa ni yavmwenyekiti wa ccm wanawake taifa Sophia Simba, Lawrance Kago Masha, Adam Kimbisa, Emmqnuel Nchimbi, Mwenyekiti wa vijana taifa ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Donge zanzibar Sadifa Khamis, Hussein Bashe, Absolomon Kibanda, Khamis Mgeja(mwenyekiti ccm Shinyanga) Msukuma(mwenyekiti ccm Geita), Na Mgana Msindai(mwenyekiti CCM Singida).

you must know how to choose your battles and you must choose your battles carefully. Sio kila vita lazima upigani. Zingine ziache zipite.

Katika issue hii ya urais, you have won some battles and you have lost battles. But overall you are loosing the WAR.
 
Si waanzishe chama chao? Yanini kujiunga na wengine wakati wao wanaamini wana nguvu na ushawishi?

wanataka wagombee sasa hv na kupitia process za kuandikisha chama kipya hawataweza kupata usajili wiki nne kabla ya kampeni kuanza
 
Watanzania wanasubiri kwa hamu kusikia raisi mtarajiwa kutoka #UKAWA atayetangazwa rasmi kesho .
Lowasa baada ya KUKATWA rasmi tunasubiri kuipasua ccm vipande-vipande Ushindi wa UKAWA utakuwa wa kishindo.
 
Ngoma inogile!
Mimi nasema Lowasa aende chama chochote isipokuwa vinavyounda UKAWA, hasa CHADEMA asijaribu. Na kweli akienda huko UKAWA utakuwa umemaliza kazi. Vita vitakuwa kati ya CCM Magufuli na (ACT, nk., yaani CCM Lowasa).
Namwombea afya njema, walau afike mwisho wa kampeni, na ashuhudie akipigwa chini kwa aibu hapo Oktoba.
Kwa maoni yangu, Lowasa ni past-tense. Magufuli na CCM yake wanaandaa kukusanya virago vyao ili waiache Ikulu salama. UKAWA ndiyo habari kwa sasa.

You must be joking...
 
CCM imemlea sana lowassa (kiislamu tunaita kusitiri). Alivyoona anasitiriwa kwa kufichiwa aibu ya maovu yake aliona anaogopwa mwisho wake akataka kukipanda chama kichwani. Amepata stahili yake. Atulie atubu madhambi yake ya kuchangia kuitia nchi umasikini. Hakuna aliye zaidi ya chama.
 
CCM lazima imeguke kwa stayle hii..Magufuli hawezi kupita kirahisi kama anavyodhani

Akienda UKAWA CCM wameisha, ila simshauri aende ACT kabisa maana wale bado sana.
 
Back
Top Bottom