UKAWA KUINGIA IKULU KUPITIA LOWASA STRIKER HATARI.
Baada ya CCM kuibua striker hatari Magufuli ni zamu ya UKAWA kumtumia stiker Lowasa kuwapatia ushindi wa uhakika. Kuingia kwa Magufuli katika kinyanganyiro kwa uraisi bila shaka ni dalili mbaya kwa UKAWA tumaini la watanzania.
Ili UKAWA washinde ni heri wamchukue Lowasa. Siasa za kuingia ikulu mwaka huu ni aina ya siasa za Kenya. Ni lazima vyama vya upinzani viungane ili kuiondoa CCM madarakani.
Tatizo la nchi hii ni mfumo wa CCM, ili kupata katiba mpya, nchi ya Tanganyika, tume huru ya uchaguzi, unafuu wa maisha ni lazima CCM iondoke madarakani. Mpatieni Lowasa kipindi kimoja tu cha urais atakuwa amesaidia kuiondoa CCM madarakani na kuizika kabisa ndipo UKAWA mtajitawala kabisa na joka kuu mtakuwa mmelimaliza.
Kupitia Lowasa, UKAWA watapata wabunge wengi kabisa baadhi yao kutoka CCM, na hivyo kuidhoofisha CCM. Lakini pia UKAWA waungane na ACT ili kazi ya kuizika CCM imalizike na ndipo muanze kujipanga upya.
Kuhusu ufisadi, kutokana na mfumo CCM watanzania wengi hakuna usafi wa kutosha. UKAWA mtakataa mafisadi kwani ninyi mmefanya ufisadi mngapi watu wamekaa kimya? Hata CCM kuna mafisadi lakini bado wanaendelea kuishi nao. Tatizo ni mfumo. Mfumo ukibadilishwa matatizo yaliyopo yatakuwa historia.
Katika mapendekeza ya uongozi wa serikali ya ukawa. Rais Lowasa. VP Duni, PM mbowe, spika Slaa, AG Lissu, Fedha Zitto, Ujenzi na Bandari Mbatia. Mambo ya nje Lipumba. Nafasi badi ni nyingi sana. Shirikiane kwanza mtapata kila kitu. Kizuri kula na ndugu yako.
Majimbo mtakayofaidi 1. Kigoma yote. 2. Arusha yote. 3. Kilimanjaro yote. 4. Dar es salaam. 5. Mbeya. 6. Manyara.7. Pemba yote. Majimbo ambayo Mtakayogawana nusu kwa nusu na CCM ni . 1. Mwanza, shinyanga, tabora, tanga, iringa, morogoro, mtwara, Ruvuma, njombe, katavi, simiyu, Mara. Mtakayopigwa sana na CCM ni Geita, Dodoma, singida, pwani
Hatimaye Tanzania mpya itapatikana. Msiipuuze nguvu ya Magufuli. Umoja ni nguvu. Hima hima UKAWA CHUKUA NCHI KUPITIA LOWASA.