Elections 2015 Lowassa kuzungumza na wanahabari baada ya kumaliza kikao kizito na familia pamoja na marafiki zake



Mzee Lowasa hana cha kusubiri CCM. Wao ccm kama wangekuwa wanamthamini wasingemfanyia kitu walichomfanyia. Vyama vya siasa viko vingi hapa Tanzania sio lazima kubaki ccm. Option 1. Namshauri mzee wetu Lowasa yeye pamoja na wafuasi wake wajiunge ACT. Akijiunga ACT ataisaidia UKAWA kushinda uchaguzi mkuu ujao kwani atazipunguza kura za CCM na hivyo kuwapa UKAWA nafasi ya kushinda na hivyo atakuwa amelipa kisasi kwa ccm. Option 2: namshauri mzee Lowasa ili kulipa kisasi kwa ccm yeye pamoja na wafuasi wake wapigie kura UKAWA katika uchaguzi mkuu wa October 2015. Option 3: Mzee Lowasa na wafuasi wake wasipige kabisa kura katika uchaguzi mkuu ujao October 2015. Hivyo kupunguza kura za ccm. Unyama Unyama tu!! UKAWA wakishinda uchaguzi huu CCM na Lowasa wote watakuwa bila bila
 


Mzee Lowasa hana cha kusubiri CCM. Wao ccm kama wangekuwa wanamthamini wasingemfanyia kitu walichomfanyia. Vyama vya siasa viko vingi hapa Tanzania sio lazima kubaki ccm. Option 1. Namshauri mzee wetu Lowasa yeye pamoja na wafuasi wake wajiunge ACT. Akijiunga ACT ataisaidia UKAWA kushinda uchaguzi mkuu ujao kwani atazipunguza kura za CCM na hivyo kuwapa UKAWA nafasi ya kushinda na hivyo atakuwa amelipa kisasi kwa ccm. Option 2: namshauri mzee Lowasa ili kulipa kisasi kwa ccm yeye pamoja na wafuasi wake wapigie kura UKAWA katika uchaguzi mkuu wa October 2015. Option 3: Mzee Lowasa na wafuasi wake wasipige kabisa kura kabisa katika uchaguzi mkuu ujao October 2015. Hivyo kupunguza kura za ccm. Unyama Unyama tu!!
 

Option namba 2 is the west!
 
Ushauri mzuri sana huu. Hicho kitabu ni kizuri sana nielekeze namna au wapi kwa kupitata
 
Mzee EL anhitaji washauri na si wapambe kama hao alokuwa akiwatumia wakashindwa kumshauri na badala yake wakamlia pesa na kumdanganya. Mzee ni mzoefu sana wa siasa na yuko kwenye game miaka mingi sana, iweje akaingizwa kwenye mtego wa kitoto namna hiyo? Kiukweli hatakiwi kumtafuta mchawi hapa bali ni kujilaumu mwenyewe.
Sio rahisi kwa mkongwe kama Lowasa,mtu alieitwa na kupewa adhabu na chama chake kwa kuanza kampeni mapema, ashindwe kuepuka adhabu nyingine kwa kuanzisha mikakati ya kupelekwa na wapambe badala ya kujituliza na kufanya mambo yake kisayansi! Ningefikiria mtu mzoefu kama Lowasa kwa kutuhumiwa huko na kama kweli alikuwa serious na kuutafuta uraisi,angefanya mambo yake kwa unyenyekevu wa hali ya juu ili asiwape mahasimu wake mwanya wa kumjadiri kirahisi km ilivyotokea. Angeachana na kutangaza nia kwa mbwewmbwe, angechukua fomu kimya kimya bila mbwembwe, angetafuta wadhamini bila misafara ya kuamusha hisia za watu.....wadhamini 450 tanzania nzima hata asingehangaika kihivyo!
Aliwapa urahisi wa kumkata.....kwa sasa the game is over,aachane na wapambe,akubari kushindwa, anyamaze kimya kama alivyoamua wakati wa Richmond, akikurupuka atajikuta anapata aibu na hasara zaidi ya hiyo. Amkaribishe Mungu wetu wa mbinguni ampe faraja, hekima na maamzi ambayo hayatamuumiza yeye na familia yake. Uongozi na madaraka si lazima ki siasa,yaweza kuwa Mungu kamuandalia mamlaka nyingine na utawala tofauti na huo wa kisiasa!!!!

Ni maoni yangu tu kwa ajili ya mzee na familia yake.
 
Lowassa ni sawa na nyangumi ailyetolewa kwenye maji (CCM) hata afurukute vipi hatapata uwezo kama akiwa majini.
 

kale kakundi ka watu 30 kalikoongozwa na JK si ndio kalimchagua magufuli
 
unachekesha wewe, mwenzio anataka yeye ndo awe rais halafu wewe unataka awapigie wengine? thubutu.

 
jamaa alikuwa na morali wa kimasai. kwa hiyo usishangae zile mbwembwe. lakini hakutarajia kwa kutegemea Kikwete angemlinda. kumbe kikwete ana yake moyoni. wasiwasi wangu ni kuwa huenda kikwete ana mengi sana moyoni juu ya jamaa. ila aliamua tu kuwa kimya. mfano ishu ya richmond lowasa alitaka kuitumia kisiasa na kuifanya kuwa ni kikwete aliyecheza dili. lakini ukisoma ripoti ya mwakyembe inaonesha jinsi jamaa alivyokuwa akiwaamrisha akina Dr. Ibrahim Msabaha kwenye dili lake. Kikwete yaelekea hakutaka kumuumbua kakaa kimya likini jamaa katumia loophole hiyo. 2010 kundi laki lilitaka kumtoa Kikwete kwenye uenyekiti wa chama, sikiliza hata hutuba ya makongoro wakati akitia nia mwaka huu, Kikwete kimya. yaelekea kundi lake pia lilikuwa likijaribu kuyumbisha hat serikali ya Kikwete, Kikwete kimya.
ilipofika sasa kuchuja majina, jina la lowasa halikuenda hata kwenye cc. liliishia kwenye kamati ya maadili. kwa Kikwete alijua kabisa kukabidhi nchi kwa lowasa, ni kuiacha kwenye mikono isiyo salama.



 
Kama CCM wanajua maovu ya lowasa basi pia lowasa anajua yao ngoma ngenge
 

Una fikra ndefu sana!Safi sana ,wakifuata huu ushauri utawasaidia.
 
Siku zote huwa nasema Tanzania hamna kabisa upinzani wa kweli, yaani wote ni wasaka tonge tu na kutaka kujilimbikizia mali. Sasa juzi kati tu UKAWA hawa hawa ndio walikuwa wanasema Lowassa siyo muadilifu, Lowassa mwizi, Lowassa fisadi kisha leo mnataka kuungana naye tena, duh! Hii mbona imekaa kimaigizo zaidi.
Ili UKAWA waonyeshe kweli wana nia nzuri na sisi wananchi, basi waachane na huyu bwana ambaye ameshindikana hadi CCM. Amini usiamini kama upinzani utaendelea kufanya ujinga kama huu, basi wategemee CCM kuendelea kutawala hii nchi milele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…