Dah, nakuhakikishia mtu akitengeneza muv ya hii mambo mpaka Rais atakapopatikana october itauza mbaya.
Tunaamini mzeee wetu ana maamuzi magumu tunayasubiria. Ila ajue akienda ACT hawezi chomoka atakuwa amejimaliza kisiasa kabisa, maana hao bado sana. Na CCM watapita kirahisi sana.
Kama anampango wa kuiangusha CCM ajiunge tu na UKAWA, maana wana nguvu kubwa bado wakipata nguvu nyingine kidogo CCM chali,,
Mzee Lowasa hana cha kusubiri CCM. Wao ccm kama wangekuwa wanamthamini wasingemfanyia kitu walichomfanyia. Vyama vya siasa viko vingi hapa Tanzania sio lazima kubaki ccm. Option 1. Namshauri mzee wetu Lowasa yeye pamoja na wafuasi wake wajiunge ACT. Akijiunga ACT ataisaidia UKAWA kushinda uchaguzi mkuu ujao kwani atazipunguza kura za CCM na hivyo kuwapa UKAWA nafasi ya kushinda na hivyo atakuwa amelipa kisasi kwa ccm. Option 2: namshauri mzee Lowasa ili kulipa kisasi kwa ccm yeye pamoja na wafuasi wake wapigie kura UKAWA katika uchaguzi mkuu wa October 2015. Option 3: Mzee Lowasa na wafuasi wake wasipige kabisa kura katika uchaguzi mkuu ujao October 2015. Hivyo kupunguza kura za ccm. Unyama Unyama tu!! UKAWA wakishinda uchaguzi huu CCM na Lowasa wote watakuwa bila bila