Elections 2015 Lowassa kuzungumza na wanahabari baada ya kumaliza kikao kizito na familia pamoja na marafiki zake


Mkuu kwa maana halisi na nyepesi ni kuwa jpm ni mtuhumiwa nambari moja wa kufuja mali za serikali?
 
Hongereni wale mlioshinda kule Dodoma, lakini pia poleni sana WANA WA EMAMNUEL NCHIMBI, KINGUNGE NGOMBALE MWIRU, SOFIA SIMBA NA ADAM KIMBISA.Faida za kuwa maarufu wa asili na maarufu wa kutengeneza zimejidhihirisha kwa kile kilichotokea Dodoma. Ni matokeo ya kuwa na hamu ya kweli ya kuwatumikia wanancgi na hamu ya kutengeneza ambayo hapana shana huambatana na matamanio ya kupita kiasi ya madaraka.
Nudgu zangu kuna taarifa ya kuwepo kwa Mkutano baina ya Edward Ngoyai Lowassa na wana Habari, nia na madhumuni kwa mujibu wa chanzo cha habari ni Lowassa kutaka kufukisha ujumbe kwa wafuasi wake kile anachodhani ni kutotendewa haki na vikao vilivyompa ushindi John Pombe Maghufuli kuwa mgombea wa Urais kupitia CCM hapo mwezi Oktoba, 2015.

Maswali yangu kwa Lowassa ni machache tu, anishawishi labda mimi na hata wengine ambao wanataka kuaminishwa kuwa bila Lowassa mchakato ule haukuwa na maana.
1. Lowassa anataka kutuambia kwamba Vikao vilivyofikia uamuzi wa John Pombe Maghufuli kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM si halali?
2.Kati ya Wagombea 37 walioachwa wakiwemo Makamu wa Rais, Mohamed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pindd na Waziri Mkuu msaafu(siyo aliyejiuzulu), Fredrick Tluway Sumaye, yeye ndiye alikuwa na sifa zote kwa maana ya uadilifu, uzoefu ndani ya chama na mwenye kuweka maslahi ya Chama na Taifa mbele kwanza na siyo maslahi binafsi kuliko wenzake?
3. Ni ukweli usiopingika kwamba Lowassa ndiye aliyetumia pesa nyingi kwenye mchakato huu kuliko wagombea wenzake inawezekana kabisa kiasi alichotumia kikawa zaidi ya mara 50 ya kiasi alichotumia John Pombe Maghufuli. Je hilo ndilo tatizo?
4. Haya yaliyotokea halisha wakuta aliyekiwa Katibu Mkuu wa Umoja wa nchi kuru za Afrika, OAU wakati huo, Dr. Salim Ahamed Salim, Makamu na Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee john Samwel Malecela na hata Rais wa Sasa Jakaya Mrisho Kikwete. NIni cha ziada alichokuwa nacho Lowassa mpaka aanze kulalamika na tofauti ya waliomtangulia ambao kimsingi waliona CCM ni taasisi na siyo mali ya mtu na hivyo busara ikatawala na maslahi ya chama na Taifa kwa ujumla vikatawala? Lowassa ni mwadilifu, ni mchapakazi kuliko hao wazee, enzi za utumishi wao?

Lowassa aache kutudanganya bwana, angekuwa msafi kiasi hicho angekuwa lulu kwa wapinzani, kwa Chadema ambao kwenye Orodha ya Mafisadi walioisoma pale Mwembe Yanga jina lake limo au hata ACT ambako kauli mbiu yao ni "MUHIMU SIYO MADARAKA, BALI UZALENDO", Chama ambacho sharti moja wapo la kuwa mwanachama wake ni lazima ukataje mali ulizo nazo, LOWASSA atatumia siku ngapi kutaja mali zake ili awe na uhalali wa kiwa mwanachama wa kweli wa ACT kama kweli wanamaanisha? Mrema ni mfano mzuri wa mwadilifu aliyetoka CCM kwenda NCCR tukaona athari zake kwa CCM na siyo Lowass ambaye ameanza kwanza na kupoteza kabisa na kupoteza Kauli mbiu ya baadhi ya vyama kwa kufadhili mikutano ikiwa ni hatua ya kujitengenezea mazingira ya kukubalika lakini baada kuyafunika macho ya viongozi wa vyama hivyo kwa UTANDO wa buibui ili wasahau kuwa nao walikuwa wapingaji wakubwa wa ufisadi wake huko nyuma.
 

Hana ubavu wa kukihama hilo lichama. Akijaribu tu ndo mwanzo wakuanza kumulikwa na biashara zake zilizo nyuma ya pazia. Akubalianae na matokeo. Bado hata akilazimisha kukihama chama ndo atajichoresha zaidi yatafumuka na yauvunguni,na ule umati wengine ilikuwa upepo na ushabiki tu.
 
Wana jamvi tunaomba kwa walio eneo la mkutano wa mh Edward lowasa na media,atujuze kinachoendelea kwani siasa siyo chuki.
Naona mnasubiria Meli air port
 
Naona bado haamini Cinema ilivyoisha, anaendelea kungojea boti at the airport
 

ccm ni km freemason tu ukiwakiuka wanakumeza
 
Ili kuinusuru CCM ilitakiwa wamshauri asigombee kabisa kwa sababu yote haina ahueni kwa CCM ama angepitishwa, au alivyotemwa.
 
Mkutano wa nini? mtaelewa tu kuwa mkutano ni wa nini ? mwaka huu kura hazitaibika
 
Golden chance ya Lowasa ilikuwa ni vikao vya CCM na vingemkubali basi angetimiza ndotoye ta urais .Sasa kwa kuwa kakosa huko asifanye kosa la kuhama. Atajutia maamuzi hayo mpaka anakufa .Yeye atulie, apewe uwaziri na astaafu kwa heshima. In business tunashauri mtu uwe na calculated risk sasa yeye Ali invest beyond calculated risk. Si Kila mshindani hushinda, kama amefeli vikaoni vya CCM huko kwa plan B au C ataangukia pua pia. Loss is common in any investment, learn from it and move forward.
 
Punguza maneno mengi. Cc tupo tayari kuungana na lowassa. Nyinyi mmeshamkataa sasa acheni kumfatafata. Kumkataa mumkatae kisha mumzuie asihame. Shame on you. Lowassa Ni MTU pekee aliyekuwa na uwezo wa kuubadilisha mfumo mbovu uliowekwa na ccm. Acheni kumtisha. MTU anapendwa na wananchi mnasema amehonga. Nano mwenye uwezo wa kuhonga taifa? Tuko nyuma ya lowassa. Sijawahi kuwa nwana ccm lakini kwa hill am supporting lowassa. In fact mmemzalilisha na kumuita mla rushwa bila kumpeleka mahakani. Kwani mkapa hakuiba? Aliwezeje kumiliki mashamba na kiwanda cha miwa. Kikwete hakuiba? He mwinyi yuko safi?
 
Haamini kilichotokea...ila Mwenyezi Mungu ametuhurumia. Huyu jamaa na yule aliyeanza ku practise urais wote wangetuyeyusha tu. Bora amechukua huyu arrogant atupige ngumi tufanye kazi na kujenga Taifa.
 
Lowasa hataweza kuhama ccm kamwe! Anajua mambo mengi aliyoyafanya na wanayofanya huko ccm ya kufichiana! Kudhubutu kuhama ndo mwisho wake utafika kisiasa. Lakin maombi yangu ahame ccm ili maandiko yatimie.
 
Enemy of my enemy is my friend.Upinzani una kila Sababu ya kushirikiana na Lowassa.
 
Nadhani sio vizuri kum-discourage mtu ambaye ana ndoto na anaona inawezekena. Muache apigane. Akishinda je? Na akishindwa tume ndo itasema Lowassa umepoteza, sisi wa pembeni tumwache apigane, sio vizuri kuingilia ndoto za watu. Imagine dying without trying your dream, na hali ulikuwa na uwezo wa kuipigania? Mi nadhani mumwache aamue mwenyewe kwamba hapa nimeshindwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…