Elections 2015 Lowassa kuzungumza na wanahabari baada ya kumaliza kikao kizito na familia pamoja na marafiki zake

Elections 2015 Lowassa kuzungumza na wanahabari baada ya kumaliza kikao kizito na familia pamoja na marafiki zake

Wakuu heshima mbele..Mh Lowassa akubali tu kushindwa..life is a bitch.Naamini kabisa watanzania wengi kabisa bado wataendelea kumheshimu na kumkumbuka kama kiongozi shupavu na jasiri.abaki ccm na ajaribu kukiimarisha chama chake ambacho ndicho kimemkuza,kimemjengea jina,kimempa umaarufu na kimempa utajiri..asijaribu kuacha mbachao kwa msala upitao.Asijaribu tena kupambana na serekali.ni vita ambavyo kamwe hataviweza.Mungu ambariki kamanda Lowassa na kumpa hekima na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi..

Umeandika hivi kama unampa ushauri mzuri Lowasa kumbe unaogopa iwapo ataamua kuikacha CCM na kuongeza nguvu upande mwingine ili CCM ishindwe.
 
Wakuu heshima mbele..Mh Lowassa akubali tu kushindwa..life is a bitch.Naamini kabisa watanzania wengi kabisa bado wataendelea kumheshimu na kumkumbuka kama kiongozi shupavu na jasiri.abaki ccm na ajaribu kukiimarisha chama chake ambacho ndicho kimemkuza,kimemjengea jina,kimempa umaarufu na kimempa utajiri..asijaribu kuacha mbachao kwa msala upitao.Asijaribu tena kupambana na serekali.ni vita ambavyo kamwe hataviweza.Mungu ambariki kamanda Lowassa na kumpa hekima na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi..

WEWE MCCM UNAOGOPA CHAMA CHAKO KUSAMBARATIKA, MTUMIE MESEJI LOWASA UMBEMBELEZE ASIYAFANYE HAYo
 
mmh!!!
Ya kweli haya!!

Hatma ya uhai wa CCM upo kwa huyu bwana.

Inawezekana na isiwezekane....one broadcast inaweza kubadili kila kitu, serikali yao ya ccm haijaanza jana au juzi......!!! Mshaurini awe mwangalifu. Mrema alichemka yeye ataweza kuadhirika zaidi na hasa hao waliojiweka wazi kuwa timu yake.
 
Mwanasiasa Edward Ngoyai Lowassa ambaye yupo katika sintofamamu na chama chake CCM atazungumza na waandishi wa habari leo au kesho nyumbani kwake Masaki jijini Dar es salaam iwapo atawahi kumaliza kikao na familia yake.

Taarifa kutoka kwa marafiki wa karibu wa mtoto wa Lowassa Fredy Lowassa ambaye alikuwa kiungo muhimu katika kampeni zake za kuelekea Urais kwa tiketi ya CCM zinaarifu kuwa Lowassa alianza kwa kufanya mazungumzo ya kina na familia yake huku katika kikao hicho Watoto wake wote wakihudhuria lakini pia wakwe zake akiwemo Sioi Sumari na kukubaliana baadhi ya mambo.

Mambo yanayodaiwa kukubaliwa na wanafamilia hao ni kwamba wawe tayari kumfuata katika chama chochote atakachoamua kuelekea, huku akishindwa kubainisha ni wapi atakapoelekea kwani alisisitiza kuwa hawezi kuhama au kutangaza uamuzi wowote pasipo kushauriana na marafiki zake wa karibu.

Hivi sasa waandishi wa habari wamefika nyumbani kwake Masaki hata hivyo wameombwa kuondoka na kuwa na subira kwani Lowassa bado anafanya mazungumzo na marafiki zake muhimu. mashuhuda kutoka eneo la tukio wanadai moja kati ya magari ya watu waliopo Nyumbani kwa Lowassa yameonekana kuwa ni yavmwenyekiti wa ccm wanawake taifa Sophia Simba, Lawrance Kago Masha, Adam Kimbisa, Emmqnuel Nchimbi, Mwenyekiti wa vijana taifa ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Donge zanzibar Sadifa Khamis, Hussein Bashe, Absolomon Kibanda, Khamis Mgeja(mwenyekiti ccm Shinyanga) Msukuma(mwenyekiti ccm Geita), Na Mgana Msindai(mwenyekiti CCM Singida).

===================

UPDATE: 12:40hours

Lowassa kaahirisha kuongea hadi taarifa zaidi itakapotolewa
.

Kama Lowassa angekuwa na akili timamu, kwenye kikao hicho cha waandishi wa vyombo vya habari alipaswa kuwasuta wapambe wake wote wanaotumia mgongo wake kujipatia fedha zake wakati wanajua afya pekee haimruhusu kugombea uongozi wa Taifa hili mbali na ufisadi ambao Baba wa taifa alimuambia waziwazi mnamo 1995. Ungekuwa ni wakati mwafaka wakuwatosa akina Mgheja, Emmanuel Nchimbi, Sofia Simba, Bashe, Lawrence Masha, Apson mwang'onda na akina Ramadhani Madabida. Hawa ni wanafiki ambao wanajua huyu fisadi hana nafasi kwenye nchi hiii lakini wanamdanganya ili amalize fedha zake alizotuibia. Bora akalee vijukuu vyake tu huko Monduli
 
Ngoma inogile!
Mimi nasema Lowasa aende chama chochote isipokuwa vinavyounda UKAWA, hasa CHADEMA asijaribu. Na kweli akienda huko UKAWA utakuwa umemaliza kazi. Vita vitakuwa kati ya CCM Magufuli na (ACT, nk., yaani CCM Lowasa).
Namwombea afya njema, walau afike mwisho wa kampeni, na ashuhudie akipigwa chini kwa aibu hapo Oktoba.
Kwa maoni yangu, Lowasa ni past-tense. Magufuli na CCM yake wanaandaa kukusanya virago vyao ili waiache Ikulu salama. UKAWA ndiyo habari kwa sasa.

Kwa UKAWA hii ya Sacco's. Bado sana
 
huo mwisho unatangazwa kwa wote au ni kwa wadogo tu.maana ikiwa ni fumua uovu na wizi sioni wa kubaki pale hata yy mwenyewe.na nnaamini hanauwezo wa kuwafumua waovu wakubwa km mjomba na mkaa hapa na mawaziri wengi waovu.sana sana ataishia kuwaonea tu hawa wa chini.lkn acha picha iendelee tuombe uzima na mungu atulinde salama

haujui magufuli,waulize makandalasi wa kichina na mbwembwe zo za ubalozi walipoiba pesa za ujenzi wa uwanja wa taifa na barabara ya Arusha alichowafanya ndo utajua magufuli akisema anamaanisha,huyu ni nyerere wa pili,

 
haujui magufuli,waulize makandalasi wa kichina na mbwembwe zo za ubalozi walipoiba pesa za ujenzi wa uwanja wa taifa na barabara ya Arusha alichowafanya ndo utajua magufuli akisema anamaanisha,huyu ni nyerere wa pili,


mkuu majizi waliopo ccm wananguvu zaidi ya huto tu michina.hata kikwete mlisema hivi hivi na kumpa jina la jk mpya mara mjeda.lkn yako wapi.magufuli hafanyi yake anafanya chama kinachoagiza na chama kilishashikwa namajangili.akikaza shingo yanamkuta ya mwakye.
 
Mwanasiasa Edward Ngoyai Lowassa ambaye yupo katika sintofamamu na chama chake CCM atazungumza na waandishi wa habari leo au kesho nyumbani kwake Masaki jijini Dar es salaam iwapo atawahi kumaliza kikao na familia yake.

Taarifa kutoka kwa marafiki wa karibu wa mtoto wa Lowassa Fredy Lowassa ambaye alikuwa kiungo muhimu katika kampeni zake za kuelekea Urais kwa tiketi ya CCM zinaarifu kuwa Lowassa alianza kwa kufanya mazungumzo ya kina na familia yake huku katika kikao hicho Watoto wake wote wakihudhuria lakini pia wakwe zake akiwemo Sioi Sumari na kukubaliana baadhi ya mambo.

Mambo yanayodaiwa kukubaliwa na wanafamilia hao ni kwamba wawe tayari kumfuata katika chama chochote atakachoamua kuelekea, huku akishindwa kubainisha ni wapi atakapoelekea kwani alisisitiza kuwa hawezi kuhama au kutangaza uamuzi wowote pasipo kushauriana na marafiki zake wa karibu.

Hivi sasa waandishi wa habari wamefika nyumbani kwake Masaki hata hivyo wameombwa kuondoka na kuwa na subira kwani Lowassa bado anafanya mazungumzo na marafiki zake muhimu. mashuhuda kutoka eneo la tukio wanadai moja kati ya magari ya watu waliopo Nyumbani kwa Lowassa yameonekana kuwa ni yavmwenyekiti wa ccm wanawake taifa Sophia Simba, Lawrance Kago Masha, Adam Kimbisa, Emmqnuel Nchimbi, Mwenyekiti wa vijana taifa ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Donge zanzibar Sadifa Khamis, Hussein Bashe, Absolomon Kibanda, Khamis Mgeja(mwenyekiti ccm Shinyanga) Msukuma(mwenyekiti ccm Geita), Na Mgana Msindai(mwenyekiti CCM Singida).

===================

UPDATE: 12:40hours

Lowassa kaahirisha kuongea hadi taarifa zaidi itakapotolewa
.
Kwa list hii msitegemee Lowasa atasema anapingana na maamuzi ya CCM zaidi ya hapo mtegemee akisema ata muunga mkono Lowasa na kusema amevunja kundi na kussuport CCM kupitia Magufuli!

Kama kuna mtu anasubili kuona na kusikia Lowasa anahama chama huyo amechanganyikiwa kabisa na wapinzani mwaka huu mnayo kazi si kitoto kama mlitegemea kupata mbereko ya Lowasa mmenoa!

Lowasa nje ya CCM ni sawa na samaki nje ya maji!
 
CCM imemlea sana lowassa (kiislamu tunaita kusitiri). Alivyoona anasitiriwa kwa kufichiwa aibu ya maovu yake aliona anaogopwa mwisho wake akataka kukipanda chama kichwani. Amepata stahili yake. Atulie atubu madhambi yake ya kuchangia kuitia nchi umasikini. Hakuna aliye zaidi ya chama.

Mmmh
Kuna aliye msafi huko ccm?

Japo simtetei bt tuwe wakweli tu!Kati ya hao wanamnyooshea kidole au ht huyo swahiba ana usafi gani cha kuona huyo mwenzao hafai kiasi hicho?
 
WEWE MCCM UNAOGOPA CHAMA CHAKO KUSAMBARATIKA, MTUMIE MESEJI LOWASA UMBEMBELEZE ASIYAFANYE HAYo

kwani ni ugonvi nendeni kwake muandamane ili aende mnakotaka kumpeleka,ila nakumbusha rais ni mpango wa mungu na mungu akikupanga kuwa wewe utakuwa rais hakuna mwanadamu wa kubadilisha lowasa tangu 1995 unaangaika wewe sio ,na mungu hapendi,na hata kama unamuomba mungu lkn yeye hajataka,

 
Akihama CCM kwanza kesi ya Richmond inafufuliwa na CCM, kesi itaendeshwa na hukumu kutolewa ndani ya wiki moja, kisha ataswekwa ndani akampe kampani Mramba na Yona. We chezea chama dola. Na yeye alikuwa huko huko


Ha ha ha ha akawape kampani Daniel na Basil... na ile ule usemi waziri mkuu mstaafu itakuwa WAZIRI MKUU ALIYEFUKUZWA kwa kuliingizia Taifa hasara ya mamilioni! Na hapo waanika mpk maradhi yake ajaribu aone
 
Ccm wana mbwa anaitwaq "TRA" huyo akisakiziwa kwako uchomoi! Na yeye ni mfanyabiashara. Wanaweza wakamtumia Takukuru pia. Afute ndoto ya uraisi labda kama anataka kuama agombee ubunge na hicho chama kipya ajihakikishie ubunge wa Monduli hapo ndio naye amwage mboga.
 
Another thread about Lowassa baada ya kukatwa na ku retire.

Kwa lipi la mno saaaana alilolifanya kwa mwaka mmoja na nusu akiwa Waziri Mkuu ????

Lipi la ajabu hilo la kukumbukwa, kupiga marufuku machimbo ya kokoto Kunduchi? Na bado baadae kokoto zikaendelea kuchimbwa.
 
Updates za JPM hizi hapa """1. Nyumba za Serikali
Kwa hakika hili ni doa kubwa sana kwa Magufuli. Ni katika kipindi alichokuwa Waziri wa Ujenzi (awamu ya 3) alishawishi kwa nguvu na msukumo mkubwa sana mpaka kufanikiwa uuzaji wa nyumba za serikali.

Hii hatua ya Magufuli halina tofauti na kile alichokiita CAG Professor Assad “Political Entrepreneurship”. Professor Assad mara baada ya kuingia madarakani alisema wazi kwamba mradi wa Magufuli wa kuuza nyumba za serikali ni ufisadi mkubwa sana. Professor Assad alizidi kusema ya kwamba alichokifanya Magufuli yalikuwa kwa manufaa yake binafsi na ilikuwa ni “personal political entrepreneurship”.

Katika uamuzi huo, Magufuli alienda mbali zaidi mpaka kugawa bure baadhi ya nyumba kwa ndugu zake na mahawara zake. Kwa mfano Dada Kabula ambaye ni mmiliki hewa wa Kebby’s Hotel iliyopo Mwenge/Bamaga jijini Dar es Salaam. Dada Kabula ambaye hajawai kuwa mtumishi wa umma tokea awamu ya kwanza mpaka leo hii Ocampo ninaposhusha huu uzi alifanikiwa kuhongwa nyumba mbili zenye Plot No. MSM/201 na Plot No. MK/521 (Mikocheni na Msasani).

Kwa hatua hiyo Magufuli aliliingiza serikali hasara kubwa sana, na hayo machungu mpaka leo hayajaisha na serikali bado linaendelea kubeba mzigo. Katika kipindi hiki tumeshuhudia watumishi wengi (Majaji, na watendaji wakuu, makatibu wakuu) wamekuwa wakiishi hotelini, huku gharama za vyumba zikiwa za hali ya juu sana almost dola 1200-1500 kwa mwezi ambayo ni sawa na Millioni 27 kwa mwezi; kwa mwaka ni Millioni 324 kwa mtumishi moja.



2. Ujenzi wa Barabara
Eneo hili ni sehemu nyingine ambayo Magufuli amekuwa akijipatia fedha haramu. Baadhi ya wafuasi wake wamekuwa wakijaribu kusema kwamba ni TANROADS ndiyo wahusika wakuu katika barabara na siyo Magufuli. Ingawa hoja yao siyo ya kweli na haina mashiko.

Kiutaratibu na sheria barabara utakiwa kuwa na upana (width) wa 6.5m ila imegundulika barabara nyingi kipindi hichi cha Magufuli zimekuwa zikijengwa kwa 5.7m to 6m na siyo 6.5m, je fedha za hizo baki 0.5m to 0.8m zinakwenda wapi, ni wazi fedha hizo uingia mifukoni mwa Magufuli na washirika wake wa Tanroads. Vile vile ni kipindi kirefu sasa Highway Economic Assessment ya miradi ya barabara imekuwa hazifanyiki kitu ambacho kinapelekea barabara zetu nyingi kuwa chini ya viwango. Utafiti wa Ocampo unaonyesha kwamba barabara kuwa chini ya viwango ni swala la makusudi ambapo waziri na wasimamizi wa miradi husika wanakula na kugawana fedha za miradi….


3. Sakata La Bomoa Bomoa
Ni jambo la wazi ya kwamba sheria zimetumgwa ili zifuatwe, lakini kuwa na ubinadamu au utu ni zaidi ya sheria. Ni Magufuli huyu huyu alipigwa stop na Mh. Rais pale alipoona Magufuli anakiuka wazi haki za binadamu. Ubomoaji wa nyumba zilizopo pembezoni mwa barabara umekuwa hauzingatii “UTU”. Ni jambo la wazi wanaanchi wengi waliobomolewa nyumba zao mpaka sasa wako katika hali ngumu ya maisha na hawana uelekeo baada ya kufanyiwa unyama usiyothimilika na Magufuli.

Either wataalamu wengi pale wizarani katika mahojiano wanasema Magufuli hana tabia ya kufata sheria na utaratibu, wakitolea mfano swala la kuvunjwa kwa jengo la TANESCO (Ubungo) na jengo la Millenium Towers. Kwa hakika ni jambo jema sana kuwa na Rias kama JK aliyediriki kumpiga stop Magufuli, hivyo basi ni wazi anapaswa apate mtu wa juu yake katika kufanya maamuzi, ila yeye ndiyo akiwa mtoa maamuzi walai nchi tutaipoteza (Tafakari kwa kina).


4. Shelly Ya Mwanza
Tukizidi kukumbuka sakata la Shelly ya Mwanza ndipo tunazidi kujua jinsi gani Magufuli ni mtu wa kukurupuka na mtu mwenye chuki. Kwa chuki zake binafsi kipindi cha awamu ya 3 akiwa waziri wa ujenzi aliamuru kuvunjwa kwa Shelly ya bwana Mansoor (mbunge wa Kwimba) iliyopo maeneo ya madaraka misheni jijini Mwanza. Baada ya ukiukwaji huo wa sheria bwana Mansoor alienda mahakamani na kisha kushinda kesi na hukumu kutolewa kwamba serikali imlipe Mansoor mabillioni ya fedha, sababu kubwa zikiwa ni chuki na kisasi cha Magufuli……

5. Magufuli ni mtu mwenye kiburi, majivuno na hashauriki
Sifa zingine pekee za Magufuli ni mtu mwenye kiburi, majivuno na hashauriki kitu ambacho ni hatari sana kwa ustawi wa Taifa. Hayo mambo yamepelekea hata utendaji kazi wa watumishi wa chini kuwa mgumu sana. Watumishi chini ya wizara yake wanasema Magufuli ni mtu mwenye majivuno sana, ni mtu mwenye chuki na ni mtu asiyepokea ushauri wa mtu yeyote yule zaidi ya mke wake na Kabula…

6. Umiliki wa Kebby’s Hotel
Kebby’s Hotel ni hoteli iliyopo Mwenge/Bamaga upande wa kulia kama unaenda posta/mjini. Kwa muda mrefu mmiliki wa hoteli hiyo amekuwa akijificha katika mgongo wa mtu mwingine ila ukweli ni kwamba mmiliki halali wa hoteli hiyo ni John Pombe Magufuli na siyo Dada Kabula.

Umiliki wa Hoteli kubwa kama Kebby’s ambayo kulala ni zaidi ya dola 60-90 inaonyesha wazi kwamba Magufuli ni fisadi wa kimya kimya kama yule jamaa mwingine aliyepiga za Escrow na vibali vya sukari au yule aliyechimbia fedha za Ghadafi kwenye mahandaki.

7. Kuvunja Ndoa
Katika maandiko Matakatifu, Kumbukumbu la Torati 27: 14 imeandikwa alaaniwe yule amtamaniye mke wa nduguye au jirani yake. Ila kinyume na hayo maandiko Matakatifu Magufuli amediriki kumtamani mke wa jirani yake mpaka kupelekea kuvunja ndoa ya mtu.

Dada Kabula ambaye ni mmiliki hewa wa Kebby’s Hotel, awali alikuwa mke wa Januarius Maganga ambaye ni mtumishi mwandamizi katika makampuni ya IPP Media. Swali la kujiuliza kama Magufuli kadiriki kuvunja ndoa ya mtu angali ni waziri wa kawaida tu, je akiwa Rias itakuwaje? Jibu nafkiri unalo…. Na sitaki unipe jibu.

Nyerere katika moja ya hotuba zake aliwahi kutolea mfano sakata la waziri mdogo wa Uingereza aliye onekana na kimada barabarani. Kwa tamaduni za hao wenzetu huo ulikuwa ukosefu mkubwa wa maadili mpaka ikapelekea kufukuzwa kazi na waziri mkuu wa wakati huo.

8. Magufuli Hakifahamu Chama Vizuri
Ni jambo la wazi na ukweli usiopingika kwamba Taifa linatafuta Rais bora na kwa upande mwingine CCM kinatafuta mtu mwenye uwezo wa kushika kofia mbili kwa pamoja.

Magufuli ana utamaduni wa kutumia chama pale anapoitaji madaraka, ila pale tu anapoyapata hayo madaraka anakuwa ajiusishi na mkakati wowote wa kujenga chama. Historia inaonyesha Magufuli hajawahi kushika wadhifa au nafasi yoyote ile ndani ya chama, wanachama wa CCM wanauliza kwamba watamkabidhi vipi mtu asiye na background nzuri kwenye chama? Vile vile historia inaonyesha hajawahi kuchangia hata senti tano katika shughuli zozote zile zenye lengo la kujenga chama.

9. Sakata La Samaki
Katika muendelezo wa kukurupuka katika maamuzi, Waziri Magufuli mwaka jana tena aliliingiza Taifa na serikali kwa ujumla katika hasara nyingine. Ambapo serikali iliamuriwa na mahakama ilipe kiasi cha shilling Billioni 2.8 na kurudiha meli husika baada ya kukiuka sheria za kimataifa pale alipokamata Meli yenye vibali halali na iliyokuwa inafanya shughuli zake kihalali.

Sasa kama ni waziri wa kawaida anadiriki kuvunja sheria za kimataifa, Je akiwa Rais si ni wazi anaweza kulipelekea Nchi ikatengwa na jumuiya za kimataifa….. we need to think kwa umakini sana wakuu…..



10. Sakata La Kivuko
Dhana ya ubinadamu siyo kuvaa nguo au kulala kwenye nyumba bali ubinadamu ni pamoja na kuwa na hekima, busara na kauli nzuri kwa binadamu wenzako; cha kushangaza Magufuli alidiriki kutumia lugha iliyotafsiriwa kama tusi kubwa sana na wananchi wa Dar es Salaam, pale alipoowambia wapige mbizi wakitaka kwenda Kigamboni. Ni jambo jema kwa kiongozi kuwa na msimamo ila msimamo wake uendane na lugha nzuri, ya uungwana na ya ubinadamu. Ni wazi kauli hiyo iliwauzinisha sana na kukasirisha wananchi wengi Dar es Salaam. Ubinadamu na utu ni kitu cha bure na siyo cha ulazima, hivyo ilitegemewa Magufuli awe na kauli nzuri na yenye hekina na busara kwa wananchi husika.

11. Magufuli ni Mtu wa Visasi vya Hatari
Magufuli siyo mtu wa kawaida kabisa, ndani yake amejaa chuki na visasi. Ni mtu wa visasi vya ajabu, hii inanikumbusha alipogombea ubunge 1995 na bwana Ernest Nyororo. Baada ya kushindwa katika kura za maoni ila baadaye alipoteuliwa bila uwoga alianza kumshughulikia Nyororo mpaka ikampelekea Nyororo akapata shinikizo la moyo. Kumbuka Nyororo ni ndugu yake wa damu sasa sisi wengine itakuwaje, ni wazi hili jambo linaitaji tafakari ya kina. Kama ndugu yake anaweza kumshambulia kiasi hicho iweje watu wa kawaida….. Leo Ocampo nikiwa naandika huu uzi sisiti kusema ya kwamba hata hao viongozi wanaotaka Magufuli apitishwe naomba niwaambie kwa chuki na kisasi cha Magufuli kuna siku atawabadilikia tena sana sana. Huko mbeleni naomba msije mkasema Ocampo hakutuambia….. Nina hakika asilimia zaidi ya 100 Magufuli ana chuki na viongozi waandamizi wa sasa, chuki hiyo anasubiri kuilipiza muda ukifika….

NB: Je kuna Magufuli Mwingine au ni huyu huyu?...............

Asanteni
Ocampo four"" mwaka huu wataisoma number ...

Mzee tumechoka na hii post kwan Huyu magufuli hana kashfa nyingine ni hizhiz tu.....tumeshazichoka kama unanyngine leta kama huna kaa kimya...
 
Back
Top Bottom