Elections 2015 Lowassa kuzungumza na wanahabari baada ya kumaliza kikao kizito na familia pamoja na marafiki zake

Elections 2015 Lowassa kuzungumza na wanahabari baada ya kumaliza kikao kizito na familia pamoja na marafiki zake

Umeandika kitu chenye maana sana ndugu. Hivi Lowassa anataka kutuambia kuwa ni yeye tu alikuwa anastahili kuteuliwa na CCM ili agombee urais? Nini hasa kinachomfanya yeye ajione kuwa anastahili kuliko wengine?? Au kuna mtu alimuambia baada ya Kikwete kumaliza muda wake ni yeye Lowassa ndio atapeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi mkuu?? Urais una nini?? Kwanini anang'ang'ania sana awe rais?????? Nani kamdanganya kuwa Watanzania wote wanamkubali???

CCM wanautaratibu wao wa kuchagua viongozi. Mimi naamini kabisa kama CCM wameona hafai kupeperusha bendera ya chama chao, basi wanazo sababu za msingi kabisa kuamua hivyo; na yeye Lowassa kama mtu mzima anapaswa kulitambua hilo. Waliochukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM hakuwa peke yake, walikuwepo watu wengine 37 na yeye wa 38. Kati ya watu hawa 37 alitegemea yeye tu peke yake ndio anasifa za kuwa mgombea urais??? Na hizo sifa alizonazo zakuwazidi wengine ni zipi hasa??? Huyu mzee akae pembeni atulie kimya.
 
Si waanzishe chama chao? Yanini kujiunga na wengine wakati wao wanaamini wana nguvu na ushawishi?

Watanzania wanasubiri kuona mwaga na kupata nuru kesho #UKAWA Julai 14


Acheni kujidanganya kwamba mtachukua nchi kirahisi.. Hata nyie wenyewe huo Ubunge tu mnaweza msiupate..

Kitu pekee kitakachotupeleka Ikulu kirahisi ni kushirikiana na Lowassa.. yeye anajua mbinu zote za CCM kuiba kura, yeye ana watu kule Usalama wa Taifa ambao ndio wapikaji wakuu wa ushindi wa CCM (mnajua wazi yuko na Apson ambao ameacha vijana wake pale TISS).. Narudia, tusitegemee Ikulu kirahisi bila kuigiwa CCM, nyomi za kwenye mikutano zisiwadanganye..
 
Washauri wa lowasa wamesha mshauri kumuunga mkono Magufuli na hakuna tamko litakalo kuwa kinyume na hicho..

Mrembo by Nature wala usijali Lowasa hawezi kusema against CCM na akisema atasema ana ungana na chama kumsindikiza Magufuli!

Kwanza angalia hiyo list hapo juu karibu wote hao marafiki zake walisha surrender na kukubali matokeao na bila shaka wamesha mshauri atangaze kumuunga mkono Magufuli usitegemee tofauti na hivyo! Hata hivyo Lowasa hawezi kukisumbua chama

Atulie anyolewe chezea 'mambo ya ndani ya chama wewe' hahaha unafinywa huku unachekeshwa
 
Last edited by a moderator:
Mzee Lowassa

Natumaini unaendelea kujikongoja baada ya a bitter defeat. Lakini nikukumbushe - haya pia yatapita. Mwisho wa siku yote yatapita.

Kumbuka -Jambo la muhimu kuliko yote kwa mtu yoyote ni familia. Bado unayo familia yako iliyo kuwepo na itakayokuwepo.

Kumbuka - Bwana ndio mchungaji wako hutapungukiwa na chochote

Madhumuni ya barua hii ni kukumbusha kile kitabu maarufu cha THE ART OF WAR BY SUN TZU.

Katika kitabu kile Tzu anaandika kuwa, you must know how to choose your battles and you must choose your battles carefully. Sio kila vita lazima upigani. Zingine ziache zipite.

Katika issue hii ya urais, you have won some battles and you have lost battles. But overall you are loosing the WAR.

Nakushauri uache sasa. Usiendelee kupigana. You are loosing the WAR!

Iache vita hii ipite Mzee.

Mwache apigane tukombolewe na wizi wa mali zetu, ikitokea akapambana na kuweka mambo hadharan ndio tutajua ukweli wa mambo ktk nchi hii. Haina haja ya kumzuia we need to know the truth
 
Mmmh
Kuna aliye msafi huko ccm?

Japo simtetei bt tuwe wakweli tu!Kati ya hao wanamnyooshea kidole au ht huyo swahiba ana usafi gani cha kuona huyo mwenzao hafai kiasi hicho?

Tina huko CHADEMA nani msafi? manake tuwe wakweli. kilichobaki ni angalau wanakoonesha uelekeo ambako ni huku CCM.
 
LOWASSA aka Lowahasa is past tense, amebaki mtupu maana Urais hata afanyeje hawezi kupata. Sana sana agombee ubunge, Unec anaweza kuenguliwa 2017. Akienda upinzani ndo anakuwa mufilisi kiakili. Chezea CCM wewee!!!!!!
 
kumbe mnajua kuwa chama chenu kinaficha waovu.sasa mnafanya nn huko mbona hamtoki na kwa kila amuungae mkono muovu kutimiza uovu wake nae ni muovu,au mmeamua kwa kiburi kuwaunga waficha uovu mkono?

hhahaha kwa vyama vya Tz kila kimoja kina uovu wake. huko kwenye SACCOS ndio zaidi. heri hata huku kwetu tunaruhusiwa kuwakataa kupitia ballot box
 
Mimi nasubiria lowassa hame tu na naomba Mungu atengeneze timu ya maangamizi na ukawa. Cha kufanya kwanza ni kuiweka sawa ile team yake ya ushindi ndani ya ccm, then ameguke nayo, baada ya hapo kuwe kuna collabo kali na ukawa ...

hata kama lowassa hatashinda urais, lkn nina uhakika ukawa watapata boost ya hali ya juu - kwenye ubunge, na kura za urais.Pamoja na hilo, ambacho ni cha muhimu zaidi ni ccm kuhenya kufa na kupona, hakuna landslide victory au zile za kupewa cake in a silver plate.

Tunataka ccm wajue kuwa hii ni nchi yetu wote na siyo yao.
 
Atulie anyolewe chezea 'mambo ya ndani ya chama wewe' hahaha unafinywa huku unachekeshwa
Lowasa anatakiwa kujua huo ukubwa na umaarufu wake ni akiwa CCM asidhani atakisumbua chama kabisa na yeye anajua fika kuwa anatakiwa kuwa mpole na ameshindwa akubali matokeo lasivyo atahama peke yake na chama kamwe hakiwezi kushindwa ata akihama!

Lowasa kamwe hawezi kuhama!
 
Lowasa ni kama Kambale na mto wake ni CCM, akihamia chama chochote ni sawana kambae kuhamia barbarani
 
Mzee tumechoka na hii post kwan Huyu magufuli hana kashfa nyingine ni hizhiz tu.....tumeshazichoka kama unanyngine leta kama huna kaa kimya...
Halafu naona kuna chuki binafsi, mbona hii post imeunganishwa na thread nyingine nyingi sana. Kwa nini? Lazima mod atakuwa team Lowasa.
 
hhahaha kwa vyama vya Tz kila kimoja kina uovu wake. huko kwenye SACCOS ndio zaidi. heri hata huku kwetu tunaruhusiwa kuwakataa kupitia ballot box
Kule kwenye saccos chama kimepanga kwenye nyumba ya mwenye chama ili pesa asipewe mtanzania mwingine! Watu huwa wanajiuliza kwanini chama hakijengi ofisi?
 
lowasa zika ccm kabisa ili ukawa tukamate nchi Kiulaini hawajathamini maumivu yako na wamekudhalilisha sana tifuA kabisa kama mbwai iwe mbwai tu dadekii
 
Punguza maneno mengi. Cc tupo tayari kuungana na lowassa. Nyinyi mmeshamkataa sasa acheni kumfatafata. Kumkataa mumkatae kisha mumzuie asihame. Shame on you. Lowassa Ni MTU pekee aliyekuwa na uwezo wa kuubadilisha mfumo mbovu uliowekwa na ccm. Acheni kumtisha. MTU anapendwa na wananchi mnasema amehonga. Nano mwenye uwezo wa kuhonga taifa? Tuko nyuma ya lowassa. Sijawahi kuwa nwana ccm lakini kwa hill am supporting lowassa. In fact mmemzalilisha na kumuita mla rushwa bila kumpeleka mahakani. Kwani mkapa hakuiba? Aliwezeje kumiliki mashamba na kiwanda cha miwa. Kikwete hakuiba? He mwinyi yuko safi?

Acha maneno yako wewe yasiyofaa, akisimama mtu sasa hivi akuita wewe ni jambazi utakaa tu kimya?? Au akisimama mtu sasa hivi akasema wewe ni shoga utakaa tu kimya??? Mimi binafsi siwezi kukaa kimya. Nitahakikisha nauthibitishia umma kuwa mimi siko kama anavyosema huyo mtu. Lowassa alipaswa kusimama imara na kujitetea kwa nguvu zake zote kuwa yeye sio Fisadi. Alikuwa waziri mkuu wakati anashutumiwa na sakata la Richmond, kama alikuwa hausiki alikuwa hana sababu ya kujiudhuru. Alichofanya wakati ule ni sawa na kuyakimbia matatizo au ni sawa na kukimbia vita. Na kwa kujiuzuru kwake nafasi ya uwaziri mkuu, ilikuwa ni kiashiria tosha kuwa yeye ni fisadi na alikuwa anahusika na Richmond. Angekuwa msafi asingeachia kazi, angesimama imara kabisa kujitetea tena kwa nguvu zake zote.

Unaposema taifa linamkubali, unakosea sana. Taifa gani linalomkubali Lowassa?? Tuko wengi sana tusiomkubali Lowassa. Tuna amini kabisa Lowassa ni Fisadi na mla rushwa. Lowassa ni fisadi anayevaa ngozi ya kondoo. Akiwa makanisani anachangia pesa nyingi sio sababu anauchungu, bali anatafuta umaarufu. Akiwa misikitini anatoa mamilioni ya pesa ili kutengeneza umaarufu. Acheni kutudanganya na Lowassa wenu bhana.
 
Back
Top Bottom