View attachment 394510
Baada ya kuona mwaliko wa Edward Lowassa kwenye Uzinduzi wa chama kipya nchini Kenya cha Jubilee Party hapo jumamosi tarehe 9 September nimejiuliza maswali mengi sana bila kupata majipu!!
1: Hivi ni nchi gani Dunia ambayo ilishawai kufanya kitendo ambacho Kenya wanakifanya cha Kutengeneza chama ndani ya chama wakati hivyo vyama unavyovivunja ndivyo unavitumia kutawala?
2: Rais aliyepo madarakani kuanzisha chama kipya cha siasa ambacho atakitumia katika uchaguzi ujao hiki nacho ni kituko kingine ambacho sijawai kiona kokote Duniani!!
Kama kuna mtu alishaona hii kitu kokote duniani aseme!
3: Lowassa anaalikwa kwenda kwenye uzinduzi huo kama nani hasa
Mimi ninavyojua waalikwa uwa ni Mwenyekiti wa chama ,Karibu wa chama, Au kiongozi mkuu wa chama ( Chifu)
3: Sasa huyu ndugu yetu Lowassa anaenda kama nani huko ni mjumbe tu wa Kamati kuu anaenda kukiwakilisha chama tena nje ya nchi?
4: Sasa kwa nini tusiamini Maneno kwamba Lowassa aliinunua chadema?