Elections 2015 Lowassa: Tusipopata mabadiliko CCM Wananchi watatafuta nje ya CCM

Hizi habari za mamvi kumwaga manyanga zimeshika kasi sanaa na lumumba moja haikai mbili haikai, matumbo joto sio la kuhara wala la kukata...maana sisikii akizumgumziwa mtia nia mwingine waliokatwa kama membe, sita...lowasa ananini..so ninaanza kuamini mamvi anaushawishi na anapendwa au?....yetu macho na masikio...
 
aje tu tumsafishe na maji ya victoria akiwa ccm alikuwa ameoga maji ya daraja la kwanza kutoka magomeni yaani janguani.
 
.. Katika Hali Ya Kujiamini Kabisa Nawapeni Taarifa Hii Kuwa Mzee Mtei Amekubali Rasmi Kujitaoa Muhanga Kwa Kumtoa Katika Kinyang'anyiro Dr. Slaa Kuwa Mgombea Wa Urais Kwa Tiketi Ya UKAWA.
Tangu lini Mzee Mtei akawa muamuzi wa mambo ya UKAWA?? Dharau za namna hii bila shaka ndizo zinazowakera members wengine wa UKAWA
 
Ikiwa hili litatokea si kweli kama Lowasa atakuwa amejimaliza kisiasa, bado ana ufuasi na "sympathizers" wengi, wapo ndani ya CCM bado mpaka sasa hawajakaa sawa na uteuzi wa JPM, na kwa vile tuhuma za ufisadi zidi ya Lowasa hazikuwahi kuthibitishwa katka chombo chochote cha Mamlaka hayo, basi Ukawa watakuwa na shoka ambalo mpini wake umetoka katka miti ya CCM, karibu ule utabiri wa Nyerere utatimia, Nionavyo!
 

Hakika ikiwa ndio wamekubaliana hivyo upinzani kushika nchi hii ni ndoto za mchana tena wakiwa wanatembea
 
Vijana mkumbuke watu wametengewa bilion 150 ili kuisambaratisha ukawa hata kwa maneno,yaani ukawa ni wajinga kiasi cha kumpa nafasi mtu ambaye anaweza kukatwa na nec tar 24/10/15 ?,,,vijana fungueni akiliiii,,haya ni maneno ya kipuuuuzi
 
Kwani hata akibaki ccm anakipi cha kujidai zaidi ya dhihaka. bora aende ukawa kuimarisha nguvu tuone mchuano mkali katika uchaguzi mwaka huu.
 
 
Ahamie tu mimi ninachotaka ni kuiondoa ccm madarakani hata kama jeshi likichukua nimechoka na serikali ambayo iko kama jiwe la mtoni kila siku maji yanalipitia lakini lina ukururutu
 
Mamvi anatuhuma za ufisadi jamani....hawezi kuwa mzembe hivyo msimdharau!! Anajua risk ya kwenda Chadema! Na CDM hawawezi kurisk pia kumkaribisha mtuhumia vibaya namna hiyo!!

Uzuri wake ni kwamba CCM hawawezi kumsema kwa ufisadi maana watakuwa wanajisema na wao maana walikuwa wote enzi Hizo.
 
Kumekuwa Na Mvutano Ambao Haujawekwa Wazi Kati Ya Vyama Vinavyounda UKAWA. Viashiria Vingi Vinaonyesha Hali Si Shwari Ndani Ya Umoja Huo Uliobeba Matumaini Ya Wananchi Wengi Waliochoshwa Na Mfumo Huu Uliopo.

Tatizo Kubwa Linaonekana Lipo Kwa Cuf/Lipumba Ambao Hawataki Kukubali Ukweli Kuwa Chadema Ina Nguvu Na Ushawishi Mkubwa Kwa Wananchi Wa Maeneo Mengi, Ni Ukweli Ulio Wazi Kabisa. Muda Umeenda, Ccm Wanazidi Kukata Mbuga Na Jembe Lao Magufuli, Na Kiukweli Huyu Mtu Anakubalika Na Kuzidi Kumpa Nafasi Ya Kuzunguka/ Kutajwatajwa Bila Ya Kujulikana Kwa Mgombea Wa Ukawa Ni Kuwapa Nafasi Ya Kufanya Kampeni.

Njia Ya Haraka Na Ya Uhakika Ni Kuachana Na Cuf Ambao Hawaaminiki Na Kukamata Fursa Kwa Kumuweka Lowasa Kuwa Mgombea Wa Uraisi Wa Chadema.

Hakuna Mwana Chadema Atakayehama Au Team Lowasa Ambao Ni Wengi Watakaoacha Kumuunga Mkono. Kikubwa Ni Kumpa Masharti Ili Kulinda Maslahi Ya Nchi Na Chama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…