Lowassa: Wakining'oa NEC nitaeleza ukweli kuhusu Richmond

Lowassa: Wakining'oa NEC nitaeleza ukweli kuhusu Richmond

Lowasa bana, anazeeka vibaya sana; anatuambia kuwa anasiri kubwa ya ukweli wa Richmon, na anajua kuwa tunachokifaham sisi Watanzania wa kawaida kuhusu Richmond ni uwongo wa maksudi! Kwa kitendo chake cha kuwaficha watanganyika ajue ni kushiriki uhalifu! Tukilegeza kamba huyu jamaa atakuja kuwa raisi wa Tanganyika Miaka michache ijayo, na nina hakika ataendeleza siasa na utendaji wa kulindana kimakundi kama anavyofanya Mkweere! Simwamini hata kidogo huyu mzee.

Mkuu, suala la kulindana kimakundi kwa viongozi wetu wa ki-siasa mbona liko wazi! Utamaduni wa kulindana ni jadi yao. Huyu EL hana jipya la kujihaminisha kwa watanzania, hivyo vi-bomu vyake alivyokumbatia eti atavilipua endapo atashughulikiwa, sidhani kama ni def.
Mechanism kwake. Lets wait and see!
 
Lowasa bana, anazeeka vibaya sana; anatuambia kuwa anasiri kubwa ya ukweli wa Richmon, na anajua kuwa tunachokifaham sisi Watanzania wa kawaida kuhusu Richmond ni uwongo wa maksudi! Kwa kitendo chake cha kuwaficha watanganyika ajue ni kushiriki uhalifu! Tukilegeza kamba huyu jamaa atakuja kuwa raisi wa Tanganyika Miaka michache ijayo, na nina hakika ataendeleza siasa na utendaji wa kulindana kimakundi kama anavyofanya Mkweere! Simwamini hata kidogo huyu mzee.

Mkuu huyo ndiye Raisi ajae,tupo Jf na tutakuja kusema tena,kuwa Lowasa ndiye Raisi ajaye kama macho yako hayaoni maandalizi basi hata kusoma uelekeo nako huwezi?
 
Mimi porojo za namna hii uwa zinanikera sana siku hzi..yaani mtu anatuambia kuwa wakinifanya hivi au vile nitasema ukweli!!! Kwanini asituambie ukweli kama yeye ni mzalendo? anategemea nini kwa utoto huu anaofanya? Maana haya ni maneno ya mtoto mdogo anayetishiwa na mama yake kuwa usiponiambia ukweli nitakupa pipi halafu huyo mtoto akakubali kufanya kusema hili kukwepa adhabu hii...shit!!
 
Kwa hiyo hasemi ukweli kwa sababu yuko NEC.....Huu uongo mwingine hauna hata kipimo..

Ndo hapo sasa...kwanini anafikiri anastahili kuwaongoza watanzania wote wakati yeye anatumikia baadhi ya watu wachache tu, kwa kuuficha huo ukweli?
 
Kwa hiyo wakimnyima ulaji huko nec ndio atakua mzalendoeeee!!!????
Aisee naona hawa magamba wanazidi kutudharau watanzania......
Wote wezi wakubwa si yeye wala hilo kundi lake!
Wako kwa interest zao tu na si wazalendo!!
 
Ujue kuna viapo watu wanaap wanaposhika nafasi kama ya Lowassa, kuna kitu anakifahamu na alifaham mchezo mzima na huenda hakuhusika sababu yeye si mwenyekiti wa baraza la mawaziri, mwenyekiti ni Dr Kikwete eleweni ipo namna na yeye aliamua kujiuzuru ili kujitwisha huo msalaba waliomuandalia tuwe makini wana JF,

Mwakyembe alisema anataka kusema ukweli hivi majuzi kilichompata si mnakijua? nawashauri tafakarini someni alama EDO hausiki na Richmond yupo anayehusika 100% ila kwa kuwa EDO kavumilia hadi kawaachia u PM, wakimng'oa CCM atakuwa na haki kusema nakutoa vielelezo, sasa akisema watamuua!

Mkiambiwa rais dikteta mnakataa kamuulizeni mwakyembe!
 
mimi kwa upande wangu na maoni yangu Namkubari Lowasa kwani ukiachana na sokoine nadhani ni mmoja wa mawaziri wakuu ambaye amejaribu kuwa na misimamo ya wazi ktk mambo yaliyo na msingi,
Na ni mtu ambaye anaweza pia kupewa nchii hii na kuifanyia mema zaidi tofauti na tufikiliavyo sisi wachache humu JF
Nimejaribu kupitia vijijini na baadhi ya miji bado watu wanamwona Lowasa kama ni mtu mwenye uwezo wa juu ktk uongozi na anafaa kuliongoza Taifa hili

Hapa jf tupo kama elfu kadhaa hivi lakini ni wachache sana wanaojihusisha na upigaji kura,wapiga kura waliowengi hawaijui Jf wala mtandao wowote ule wa kijamii na hao ndio wanaomwona Mh Lowasa kuwa anafaa na wangependa wampe nafasi kuiongoza nchi hii

Nawaomba WanJF mjaribu kupita Vijijini na miji mingine mpate habari juu ya mvuto wa huyu mh ni Tofauti sana na Tupigavyo kelekele humu JF
 
ukweli gani mpya tena zaidi ya aliousema Dr Mwaktembe " hili halita saidia kitu "

Mbona hata akina Mwakwembe kwenye ripoti yao walihitimisha kwa maneno haya quote "kama tungalimwaga yote tunayoyajua na vithibitisho vyake kuhusu ufisadi wa Richmond basi kusingekungalikuwa na atakayesimama, lakini ushahidi upo wa zaidi hapa tulipohitimisha na ni busara yetu tumeona tuisitiri serikali" end of the quote. Hivyo basi wanakiri kuwa wangemwaga kila kitu hata Mkulu pale Magogoni angalitumbukia baharini akaishia kama alivyoishia Lowasa. Hivyo basi Lowasa yuko sahihi kabisa kuwa Wa-Tanzania hawajui yote kuhusu kashfa ya Richwond. Bali Lowasa alibeba msalaba wote ili kuisitiri serilkali na ndio kikubwa kinachomla roho kwani anaona hata aliyem-save hana shukrani. Habari ndo hiyo.
 
Muerevu akikwambia upumbavu na anajua wewe ni mwerevu na wewe ukaukubali anakudharau! LOWASA KADANGANYE WATOTO WA KUKU WANAOAHDIWA KUNYONYA DAILY NA MAMA HANA MATITI. Pumbavu zako
 
kwani bado kuna ukweli tusioujua?



hahaa samora kwa unafkiri wewe unaujua ukweli!!??
pole ndugu yangu.......
magamba wote wanahusika na richmond ila nadhani EL alitolewa sadaka
lol
utamuamini nani!!?? wakati magamba wote ni vigeugeu???
ukigusa maslahi ya mtu tu ndio anasema ukweli.......usipogusa wanaendelea kulindana!
 
Wakati makundi mawili hasimu yale yanayomuunga na kutomuunga Lowassa yakitunishiana misuli kuhusu kuvuliwa gamba kwa kutumia kashfa ya richmond, lowassa amenukuliwa na watu wake wa karibu akisema huu utakuwa wakati mwafaka kwake kusema kila ukweli anaoujua kuhusu richmond.

Chanzo: Tanzania Daima

kama ni kweli ana ukweli anaoujua halafu hataki kuusema basi si mzalendo wa kweli. Kwa nini anawajua waovu halafu anawaficha?
 
Kwa maana hiyo CCM ni genge la majizi,wako humu kwa kuwa kuna kitu kinawafanya wawe wamoja, UFISADI. Kwa hiyo wanapohitilafiana namna ya kuifisadi nchi ndiyo wanaanza kutoleana siri za ndani. Kwa move hii Lowasa anajitambulisha kwamba ni mwiba kwa watanzania ambao tunaendelea kupata madhila yatokanayo na sakata la Richmond ambalo yeye Lowasa alikuwa key player. Najua anachotaka kusema ni kuwa hili dili lilikuwa la JK, yeye alipewa tu jukumu la kusimamia utekelezaji, na kama ni hivyo jee ataaminika? Tukirudi nyuma ktk sakata la Richmond, Dr. Mwakyembe aliwahi kusema bungeni kuwa report waliyotoa wamei-waterdown ili kulinda heshima ya serikali, na ni report hii iliyomuangusha Waziri mkuu na baadhi ya mawaziri, kwa mantiki ya Mwakyembe ni nani mkubwa zaidi ya WM aliyekuwa analindwa kama siyo bosi wa Lowasa? Hiyo ndiyo turufu ya Lowasa anayotishia nyau, jee itamsaidia kwa sasa?
 
Maslahi ya hiki chama cha CCM yanaitesa nchi!Kila mtu ameona huko kuna ULAJI,kinachofanyika ni mtu ku2mia Ignorance of ze poor kuwanyonya wengne!Lowasa amechelewa kutweleza ukwel,alipokuwa akijiuzulu alipaswa KUPASUA ukwel huo!
 
Source ya hii taarifa ni ipi? Hao watu wake wa karibu ni akina nani?
 
Hee kumbe kila mbunge wa CCM aligawiwa hela za richmond kufanikisha kampeni jimboni mwake huu ilikuwa ni fund rising strategy ya chama.. makubwa then wote mafisadi
 
kwani bado kuna ukweli tusioujua?

yes, soma hiyo post kabla yako khs report ya mwakyembe ..inamaanisha wapo wengi kwenye hilo sakata ambalo huenda hata mzee wa magogoni nae anahusika kwa asilimia zote
 
Back
Top Bottom