Lowassa: Wakining'oa NEC nitaeleza ukweli kuhusu Richmond

Anatisha nyau ,hana uzalendo hata punje wa hovyo sana Lowassa,akibaki Nec au CCm kahongwa kwa hiyo hata sema angenyamaza kabisa kwa sababu halisaidii taifa hili
 
EL alisema wakimwaga mboga yeye atamwaga ugali. Aliahidi wakimuvua gamba yeye atawaonyesha watanzania mahali alipo BALALI. Hii ndio mimi naisubiri kwa hamu.

He!! Alitamka haya maneno??? Kazi ipo
 
Lakini atakuwa amechemka sana kusema sasa hivi wakati alinyamaza toka mwanzo??
Nini maana yake sasa katika hili??

Hapo ndipo utaona huyu jamaa hafai kuwa Rais
 

Kumbe hafai, kwanini asubiri mpaka ang'olewe. Basi subiri ang'olewe ili alitumikie taifa ipasavyo kwa kueleza mambo ya Richmond.
 

.... hathubutu kukata mti alokalia! Mengi mnayoamini ni porojo tupu. Mnachezewa na disinformation kibao. Mngetafakari malengo ya spinning inayofanywa miaka yote hii ni nini, kama si kuwapumbaza kwa kizingatia hadithi za kina alnacha kila siku badala ya kufanya kweli. Doing the rightful!
 

Mkuu kumbe ulishawahi kuwa na fikra za rais wa 2015 atoke CCM? Hadi ukamuwaza Lowassa? Anyway, si kwamba jamaa anazidi kujionyesha kwamba hastahili, hajawahi kustahili tangu mwanzo. Hata huyo swahiba wake ambaye hawajakutana barabarani hakuwahi kustahili kuwa rais. Ni uzembe tu wa watanzania mtu yeyote tu ali mradi tu apitie ccm anakuwa rais. Niliwahi kusoma mahala eti Emmanuel Nchimbi yule waziri wa habari na michezo naye anatajwa 2015. Nilichoka. Siku hizi kuna Membe na Wassira. Kwa sababu CCM kimewaoa watanzania mhuni tu anaweza kuzuka from nowhere wakati unabaki kushangaa ukasikia naye ni rais wetu, kisa kapitia CCM. Ni wakati wa kusema basi...CCM 2015 haipaswi kutoa rais. Tuwaze hivyo na tufanye hivyo kwa vitendo.
 
 
Hana uzalendo huyu mzee,kama ana uzalendo aseme.Kwa staili hii hata akipata Urais hatakuwa na jipya
 

Hii imekaa kitoto sana, chanzo T/Daima, mkakati wa kumuokoa Lowasa, kina Kibanda wameamua kutumia mbinu ya kitoto kuwatisha NEC wasimdhuru tajiri yao!!

Masikini, wamesahau kuwa aliambiwa apime mwenyewe, na kweli akapima akaona ana hatia kuliibia taifa, akajiuzulu!!! Hapo ndipo wenzake walipomtengezea kitanzi akajimaliza mwenyewe bila kujua, kilichobaki ni kutishia nyau!
 
Kama kweli ndani ya NEC wote wanajiona kuwa ni wasafi sidhani kama ingewachukua muda mrefu kiasi hiki kumsulubu Lowasa... hii ishu ya Richmond kuna jambo linafichwa na Lowasa amefanywa mbuzi wa kafara, tatizo kila mtu anaogopa kumuanza...

hajioni wasafi wanajijua kama wameisha chafuka sema kuchafuka kwao kuna tofautiana
 
Kama kuna ukweli wa hili ni vyema wamng`atue maana kamati teule imemhoji akaeleza uongo na kusema haya yote ni sbb ya uwaziri mkuu kana kwamba hakuwa na alijualo hapo sasa ndo patamu piga za uso!
 
Ushauri wangu aendelee kukaa kimya maana atazidi kuishusha hata hiyo hadhi yake kidogo iliyo bakia
 
hata akisema ukweli utakaom-implicate rais, bado yeye atakuwa mhalifu na hiyo haizuii kutiwa ndani na kisingizio kuwa yeye na rais ni sehemu moja ktk uhalifu huo haiwi utetezi hata kidogo na mwisho wa siku kifungo ni chake na si cha mtu mwingine. rais atashughulikiwa muda wake utakapoisha, kama bado kutakuwa na haja ya kufanya hivyo. kwa sasa yeye EL ashughulikiwe inavyopaswa ili 'liwe somo kwa wengine wote' na kuwa mwisho wa ubabe wa kinadharia na mikwara!
 
Ndicho nilichowambia Mkandara hicho,EL kashikilia kwenye kamali...Kutachimbika kama ni kweli,trust me!

Mwakyembe around or not,someone still holds the wild cards.

Kumbuka kulikuwepo na ripoti mbili na Mwakyembe aliitoa ile ya kumchafua EL...

Kwanini akubali kuchafuliwa wakati ukweli anaujua?
Hana nyimbo,
anataka urais na campaign kisha zianza makanisani.
Mdini no moja mbona msikitini haendi?
 
Mungu yupo kuwa tetea watanzania.hakuna jiwe wala punye ya mchanga itabakia. Lowasa huto ongoza taifa hili only mungu apange.
 
Wewe ni kada wa Lowasa. Amejitoa kafara aponye wengine? Mungu akakupige ububu? Yan watanzania tunahaha kwa uwozo huu nama cost? Mungu akawasamehe aise?
 
Hata hivyo ni ukweli mtupu kwamba kama aliyaficha hayo akiwa waziri mkuu na anataka kuyasema ili aupate urais,basibinafsi nina conclude kwamba mtu huyu ni hatari sana.

What if akiwa rais?Ataficha nini na atafanya hivyo kwa ajili gani?

Mhn mhn!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…