Siku ina masaa 24, utafiti huo unasema lower middle (ambao umeniweka ndani yao) wanatumia masaa matatu, ina maana masaa mengine 19 mtu anayatumia kwenye mambo mengine. Na hapo nimeiweka unavyotaka kuamini kwamba hamna cha kujifunza kwenye mitandao ya kijamii, hivyo masaa matatu ndani ya masaa ishirini na nne ndio mtu anaharibu kwenye hii mitandao bila kujifunza chochote.
Hebu hapo ulipo waza nini unaweza kufanya ndani ya masaa kumi na tisa, ukiondoa masaa manane ya kulala, yanasalia kumi na moja, ukishindwa kufanya chochote ndani ya masaa kumi na moja, bora ufe.
Kwa mfano mimi hapa huamka saa tisa kila siku, nafanya shughuli zangu zote (ikiwemo kusoma, mazoezi, kazi) hadi saa saba mchana, kuanzia hapo nakua free kufanya chochote nitakacho hadi saa tatu usiku najilaza kitandani na kuisahau dunia.
Aina yangu ya kazi inahitaji full throttle energy, concentration and focus kwa masaa manne hadi matano, basi.