Tatizo liko wapi kwake! Yeye ametimiza wajibu wake! Nioneshe kosa lake? Baba yako amekulipia kila kitu shuleni mwisho wa siku unaleta ziro nyumbani! Ni kosa lako au la baba yako?
Elewa MO ni muekezaji! Mwekezaji yeyote anataka faida! Amewekeza Simba ili apate profit return! na anatoa pesa kadili ya makubaliano! Nyie wengine mnatimiza majukumu yenu?!
Viongozi wenu wanatimiza wajibu wao? Au wamekaa tu wanasubili pesa za MO zije wazitafune kwa kufanya ujanja wa kupata 10% ? Akija mwekezaji mwingine wakina Kajura,try again Abdala,na Mangungu ndio watatimiza wajibu wao vizuri?
Watanzania mmezoea na kulemazwa na ujamaa,mnapenda wengine wawajibike kwenye furaha yenu bila nyinyi kuwajibika kwa lolote