Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wanasheria naomba msaada wenu kujua mwenyekiti wa tume ya uchaguzi anatangaza matokeo ya uchaguzi wa Tanganyika ama wa Tanzania ? Kama ni wa tanzania mbona uchaguzi wa Zanzibar ulishafutwa ??
Swali...
Je kuna uhalali wowote wa yeye kuendelea kutangaza matokeo wakati upande mmoja wa muungano umeshafuta matokeo yake ?? Ama haya matokeo anayoyatangaza ni ya uchaguzi wa Tanganyika tuu ??
Naomba msaada wenu wakuu maana uwelewa wangu ni mdogo kuhusu hili swala..
Jibu langu ni kwamba...ipo kasoro....lakini kasoro hizo zimefunikwa na technical part of the laws zinazo govern uchaguzi huu. nitajitahidi kuelezea ...lakini sina uhakika kam utaelewa...ukielewa vizuri...usipoelewa sio mbaya....jibu lipo kisheria zaidi(Na kwa mawazo yangu , linapingana na hali halisi ya znz)
Jibu ni hili kisheria
Nec wapo sahihi kutokusimamisha uchaguzi wa JMT kwa sababu
Sheria inayosimamia uchaguzi wa JMT ni tofauti na sheria inayosimamia uchaguzi wa znz.... kwa maana ya katiba ya 1977 na ya 1984
Sasa Kura za uraisi wa JMT zinasimamiwa na Nec na sio Zec.... na Nec wanasema kwa Kura za raisi wa JMT zilizopigwa znz hazina kasoro na zimesimamiwa na NEC na sio Zec na hazina malalamiko ( hapa ndipo sheria inapingana na facts at hand)
Kwa hiyo kura hizi hasihusiani kabisa kisheria na kura za znz. Kwamba...kura za uraisi wa zanzibar na wawakilishi wake ndio zinakasoro na Zec ndio yenye mamlaka nazo....wakati hizi za raisi wa JMT zimesimamiwa na NEC....na nec wanasema hazina kasoro....
Nimejitahadi kuelezea sijui kama umenielewa .
Jibu langu ni kwamba...ipo kasoro....lakini kasoro hizo zimefunikwa na technical part of the laws zinazo govern uchaguzi huu. nitajitahidi kuelezea ...lakini sina uhakika kam utaelewa...ukielewa vizuri...usipoelewa sio mbaya....jibu lipo kisheria zaidi(Na kwa mawazo yangu , linapingana na hali halisi ya znz)
Jibu ni hili kisheria
Nec wapo sahihi kutokusimamisha uchaguzi wa JMT kwa sababu
Sheria inayosimamia uchaguzi wa JMT ni tofauti na sheria inayosimamia uchaguzi wa znz.... kwa maana ya katiba ya 1977 na ya 1984
Sasa Kura za uraisi wa JMT zinasimamiwa na Nec na sio Zec.... na Nec wanasema kwa Kura za raisi wa JMT zilizopigwa znz hazina kasoro na zimesimamiwa na NEC na sio Zec na hazina malalamiko ( hapa ndipo sheria inapingana na facts at hand)
Kwa hiyo kura hizi hasihusiani kabisa kisheria na kura za znz. Kwamba...kura za uraisi wa zanzibar na wawakilishi wake ndio zinakasoro na Zec ndio yenye mamlaka nazo....wakati hizi za raisi wa JMT zimesimamiwa na NEC....na nec wanasema hazina kasoro....
Nimejitahadi kuelezea sijui kama umenielewa .
Kwa hiyo wakati wa upigaji kura Zanzibar katika kila kituo kulikuwa na maafisa wa ZEC na maafisa wa NEC na hao wa NEC walikuwa na vituo vyao ndani ya vituo kiasi kwamba dosari zilizojitokeza katika kura za Zanzibar hazikuweza kuzihusisha zile zinazohusu Rais wa Jamhuri?
Nimekuelewa mkuu... Ila huoni hapo kuna mgongano wa katiba pande zote mbili za muungano ??? Pili kama tume ya Zanzibar imesema Kulikuwa na udanganyifu ama uvurugaji wa matokeo uchaguzi huu kwa upande wa Zanzibar hauoni kuwa kutakuwa hakuna uhalali pia wa kura za rais ya JMT kwasababu kura zimepigwa na watu walewale ,siku ilele na kuhesabiwa na watu walewale ....embu nifafanunulie katiba yetu inasemaje hapa.
Nb
Mimi sijui sheria ni mkulima wa kawaida tu
Mtajibeba......
Magufuli anaapishwa kesho Uhuru stadium.
Haya yote yanayotokea ni dalili wazi za kuchoka kwa ccm. Madudu madudu tu.
N kulazimisha mambo kutawagharimu sana.
Hakuna ridhaaa ya wananchi kuongozwa na ccm.
Tangu Lubuva ameaanza kutangaza matokeo feki, sijakutana na zaidi ya watu 3 wanaofurahia au kushangilia.
Ninakutana na watanzania wanaosoneka kuwamba haki inapindishwa. Watanzania hawana raha kuona wanaongozwa na mtu mtu ambaye si chaguo lao.
Ndoa ya kulazimisha haina raha. Ni wawili wakubaliane.
ccm haina ridhaa ya watanzania wengi.
Hii ni hatari.
Hata huyo magufuli hatafurahia uraisi wake.
Hata wanaovaa manguo ya kijani nafsi zao zinawasuta kuwa wanafaulu mtihani kwa kuiba matokeo.
2+2=4 haiwezi kuwa 5 hata siku moja.
Majuto ni mjukuu. hilo ni lenu ccm.
Kwa uelewa wangu....Zec ni wakala wa Nec kwa uchaguzi wa raisi wa JMT kule zanzibar.....na hicho ndicho kinachoelezwa na Nec kwamba kura za raisi wA JMT kule zzb hazina shida...hayo ndo majibu yao.Kwa hiyo wakati wa upigaji kura Zanzibar katika kila kituo kulikuwa na maafisa wa ZEC na maafisa wa NEC na hao wa NEC walikuwa na vituo vyao ndani ya vituo kiasi kwamba dosari zilizojitokeza katika kura za Zanzibar hazikuweza kuzihusisha zile zinazohusu Rais wa Jamhuri?
Umefafanua vizuri sanaLubuver na tume yake sijui wanatoka Sengerema. Maana Kila mzanzibari alipiga kura tano, Sheha, Mwakilishi, Mbunge wa Muungano,Rais wa Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Muungano. Kura zote alipiga siku moja, kituo kimoja na kwa kadi moja. Sasa kama matokeo ya Sheha, Mwakilishi, Mbunge wa Muungano na Rais wa Zanzibar ni batili sasa yale ya Uraisi wa muungano yanaendeleaje kuwa halali kama baadhi ya dosari alizosema Jecha zilijitokeza vituoni?
ZANZIBAR: JE INAWEZEKANAJE KURA ZA RAIS WA ZANZ NA WAWAKILISH ZIWE BATILI NA ZILE ZA RAIS WA JMT NA MBUNGE ZIWE HALALI?
Katika uchaguzi wa Zanziba, utaratibu ni kwamba Watanzania Zanzibar wanapiga kura 5, yaani Rais wa Zanz, Mwakilishi na diwani. Pia wanapiga kura ya Rais wa JMT na Mbunge.
Kwenye kituo cha kupigia kura kuna meza 2. Moja ni ya tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) na nyingine ni ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Meza ya NEC ina watumishi wake na Meza ya ZEC ina watumishi wake.
Watumishi wa NEC wanaripoti moja kwa moja kwa NEC na watumishi wa ZEC wanaripoti moja kwa moja kwa ZEC,
Meza ya ZEC inashughulikia uchaguzi wa Rais wa Zanz, Mwakilishi na Diwani na Meza ya NEC inashughulikia uchaguzi wa Rais wa JMT na Mbunge,
ZEC wanaongozwa na katiba ya Zanzibar ya 1984 na NEC wanaongozwa na Katiba ya Tanzania ya 1987,
Pia vyama vya siasa wanaweka mawakala wa aina mbili, moja kwenye meza ya NEC na pili kwenye meza ya ZEC,
Hata katika kuhesabu kura hawa watu hawaingilian, ZEC na mawakala wao wanahesabu kura zao na NEC na mawakala wao wanahesabu kura zao.
Pia kuna ballot boxes tofauti. Zipo za ZEC na NEC.
Mzanzibar anapokwenda kupiga kura kwanza anakwenda kwenye meza ya ZEC, anatoa kitambulisho na anapewa kura tatu, Rais wa Zanz, Mwakilishi na Diwani. Anapiga kura na anapakwa wino kidole kimoja.
Baada ya hapo anakwenda kwenye Meza ya NEC anapewa kura 2, Rais wa JMT na Mbunge. Anapiga kura na kuzitumbukiza kwenye mabox ya NEC ambayo ni tofauti na yale ya ZEC.
Wakati wa kuhesabau hawa watu hawaingilini.
Kwa hiyo kasoro katila kura za ZEC, hasa kuongezeka kwa idadi ya wapiga kura tofauti na wale waliojiandikisha bila kuathili kura za NEC ni kutokana na kuingiliana katila majukumu yao.
Udanganyifu umefanyika kwenye meza ya ZEC ndiyo maana walibaini hizo kasoro walipokuwa wanahakiki lakini kwenye meza ya NEC hapakuwa na udanganyifu wowote ndiyo maana hapakuwa na kasoro zozote zilizobainika.
Swali; Anayepiga kura ZEC, ndiyo yule anayepiga kura NEC. Kwa nini idadi iongezeke ZEC halagu NEC idadi ya wapiga kura isiongezeke.
Jibu ni kwamba, siyo lazima udanganyifu ufanyike kwa kuongezeka kwa idadi ya wapiga kura, la hasha! Kuna uwezekano wa wapiga kura wakaingia na kura fake na wakafanikiwa kupiga kura zaid ya moja kwa upande wa viongozi wa Zanzibar lakini wanapokwenda meza ya NEC wasifanye huo udanganyifu.
Pili Watumishi wa ZEC wanaweza kutoa balot paper zaidi ya moja kwa mpiga kura kwa lengo la kufanya udanganyifu kwa lengo la kupendelea wagombea wa chama fulani, na watumishi wa NEC wasifanye huo idanganyifu,
Tatu udanganyifu unaweza kufanyika wakati wa kuhesabu kura na kwa upande wa ZEC wakaongeza idadi ya kura lakini upande wa NEC wasifanye hivyo.
KWA HIYO, kutokana na hayo, ni dhahiri kwamba KASORO ZILIZOJITOKEZA KWENYE MATOKEO YA UCHAGUZI WA ZEC HAZIJAATHIRI MATOKEO YA KURA ZA NEC.
swali,kama kura zilizopigwa visiwani zimefutwa atapatikana vipi raisi wa bara?