Lucci Laciano: Mwanamuziki wa Jamaica aliyejichora tatoo ya Rais Magufuli (PICHA)

Sasa sisi maskini wa hali ya chini tutanufaika vipi na hiyo picha?
 
Propaganda za kitoto kweli kweli, kumbuka hili ni jukwaa la GT na members wake wametapakaa dunia mzima, sasa kutuletea usanii wa Lumumba hapa ili upate kiki ya kumpaisha mfalume ni upuuzi.
 
weka picha yake halisi, siyo kutafuta kiki mitandaoni tu
 
Ina maana dudu baya imeshakuwa raia wa Jamaica? Mbona mleta uzi anadanganya sana... Nina mpango wa kuhama huku maana pameshakuwa napo Ni la udaku tuu
 
Mshamba flani kutoka kabila la washamba flani aki...... wa kwao.
 
Hamjui kwanini kajichora

Jamaica kumekua na gunzo la mtukufu kukimbia vikao vya kimataifa eti kisa lugha
Sasa huo ndio mjadala na hiyo kujichora ni kumbeza tuu hakuna sifa yoyote hapo
Angalia vizuri kilichochorwa ndipo utapata ufafanuzi wake
 
Kumbe habari za Magufuli zimeenea hadi Jamaika..
Ni wanaojiita UKAWA tu ndio wanajifanya hawaoni! Leo Bwana mmoja akihojiwa BBC anasema Magufuli amekosea Elimu Bure. Angeanza Mishahara ya Mwalimu huku wanafunzi wakiwa hawana madarasa na wanakaa chini. Tumemwelewa kwa kuwa Walimu ndio walikuwa washabiki na wapiga kura wake! Ila anamkubali JPM kwa mambo mengi!
 
Yaani nimeipenda hiyo ' Hatishwi na Matatizo ya Mpito bali anatishwa na matatizo ya muda mrefu' , wenye Almasi wengine kazi yao kumkashifu na kutaka kumrudisha nyuma uzuri ' Hatishiki na matatizo ya mpito' dah nimeipenda sana hii!
 
Hii ni picha ya mwaka huu ya Luciano



Tukumbuke Luciano ni a pure Rastafarian, hawa hawakati nywele na huamini mwili ni hekalu ambalo hutakiwi kulichafua na kitu chochote kisicho asili, vile vile hawaendani kabisa na utamaduni wa kujipiga tattoo.

Katika miaka yake yote Luciano hajawahi kuonyesha tattoo yoyote iweje leo hii ajichore tattoo ya Magufuli na kujipiga picha, iweje apingane na imani yeka ?

Hii picha yako ina mtu anayeonekana kujipiga tattoo kifua kizima, na kibaya zaidi haiendani na ukubwa halisi wa sasa wa Luciano ambaye ni mtu mzima (Miaka 51).

Hizo tattoo kuna maneno "Feza Gang" na DD


Hawa wanaonekana ni kikundi cha vijana wanaofanya muziki hapa bongo kutokana na account mbali mbali kwenye mitandao ya kijamii na logo yao ni kama inavyoonekana hapo chini. Kwa nini Luciano apingane na imani yake na kujichora tattoo za hiki kikundi?


Huu ni uchunguzi mdogo niliofanya, na kupuuza hii thread yenye lengo la kupotosha jamii. Zamani JF ilikuwa ni chanzo cha habari za kuaminika lakini kuna members wachache wanazidi kushusha uaminifu wa habari zinazoletwa hapa, Mods kama mnaiona hii post nawaomba mchukue hatua zinazostahili ili kutoshusha thamani ya JF na dhana ya kuwa hapa ni nyumbani kwa Great Thinkers.
 
uongo Wa kijinga mmmno kwa kipi cha kimataifa ivyo? Au kusimamia ishu ya madawati?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…