Lucky Dube: Miaka kumi(10) tangu auawe


Nje ya jukwaa, alikua na unyenyekevu na mtu wa aibu sana. Ikija kwenye show, makamuzi yake ni balaa. Aliwahi kupiga 3 hours non stop show na mziki wake unatumia nguvu sana.

Pia alikua na uwezo wa kuimba sauti ndogo sana nyembambaaa...utaisikia kwenye Remember me, Its not easy, How will I know n.k
 
Nimeona video moja ya muandaaji wa matamasha ya Reggae toka enzi za Bob, anasema siku ya kwanza Dube anapiga kwenye tamasha hilo huko Jamaica, mambo yalisimama wakatisha tiketi, walinzi n.k wote waliacha kazi zao wakakimbilia jukwaani kumwangalia! Anasema hawakuwahi kuona show yanguvu vile Jamaica!!
RIP Lucky Dube
 
daaah Dubeeeeee, i like your muziq to the fullest,, rest in peace and not in piece rasta
 
Kwangu mimi wakati nakuwa nilikuwa nikiambiwa cheza reggae basi lazima uniwekee kaseti ya Lucky Dube, ukiweka mwengine sichezi nakwambia hiyo sio reggae.

Hadi leo hii icon wangu wa musiki huu anabakia kuwa Lucky Dube hao wengine mi siwajui.
 
nimependa ulivoweka source big up sana mkuu bandiko limekaa vyema
 
Hiyo ngoma inaitwa Never Leave you, Mkuu, pia kuna wimbo aliurudia ninadhan hata Mariah Carey nae aliufanya pia unaitwa I want to know what love is.,
Bro wangu alikuwa na album ya Dube ilikuwa na nyimbo nyingi tu za mapenzi, jina la album limenitoka kidogo. Jamaa alikuwa vizur sana man.
 
Kweli kabisa, alikuwa ni mwanamuziki wa kipekee zaidi. Ndiye mwanamuziki niliyemhusudu kipindi cha utotoni kuliko nilivyomhusudu Bob Marley.
daah kwakweli hata mimi nilimuelewa zaidi Dube kuliko Bob...hapo kwenye "kutovuta ganja" sikubaliani na wewe mkuu!! kwa message alizokuwa ana portray kwenye jamii haiwezekani kwamba alikuwa hali ganja!! mtu wa kawaida ambaye hali majani hawezi kufikiria au kuandika mashairi kama aliyokuwa anaandika dube,tukubaliane tu kuwa alikuwa anakula ganja japo alikuwa hakubali moja kwa moja au kukataa moja kwa moja pindi akihojiwa!! tafuta ngoma yake inaitwa "rastaman's prayer", kaisifia sana ganja humo(mie sili ganja though).

saying all these,to me,Lucky Phillip Dube was a prophet
Ingzebier,Negusta Negust.R.I.P Rasta
 
msh
m
Mshikaji alikua ni bonge la Great Thinker
 

Yote yawezekana Tobinho, ila katika majibu yake mbalimbali kwa maswali aliyoulizwa, alisema hatumii ganja. Kuhusu wimbo Rastaman's Prayer' toka album ya 'Trinity' iliyotoka mwaka 1995,... kwa nilivyomuelewa Dube, si kwamba alikuwa akisifia ganja/marijuana ama bangi, no, alikuwa anaelezea namna gani wanadamu tunavyomuomba Mungu kwa mahitaji yetu mbalimbali, naye (Mungu) bila hiyana hujibu maombi yetu. Mfano wanasiasa huwa wanatumia uongo zaidi na ahadi za kufikirika ili wapate nafasi wanazozihitaji, mataifa makubwa nayo huwakandamiza mataifa madogo kwa manufaa yao, ila yote haya huwa hayawezekani bila kupiga goti kwa Mungu; Wale wanaovuta bangi pia humuomba Mungu kuistawisha, unaona jinsi alichokuwa anamaanisha! Angalia hiyo mashairi hapo chini kisha uchambue. Ila pia inawezekana aliona majibu ya anatumia au kutokutumia ganja hayakuwa muhimu zaidi kwa watu. Inawezekana pia alikuwa anatumia na baadaye akaacha kutokana na labda kuwa muumini wa dini ya Kikristo ya 'shembe" ambayo yeye Dube alikuwa muumini wake.

"There comes a time
In everyman's life where he's got to face
The truth no matter what
We are coming to you father
With our sins and everything
To thank you

Those that smoke marijuana
Wanna thank you father
For making it grow internationally
They wanna thank you lord
Even though police cut it down
Sometimes they burn it down
But it grows again
Thank you father

We wanna thank you father
For everything you've given us

Nations that oppress other nations
Wanna thank you father
Even though it's painful to be oppressed
But they thank you...
For making them strong

Politicians thank you father
For making them to be able
To lie with a straight face
While the nation cries
They wanna thank you lord
 

Yah....alirudia wimbo wa mwanamuziki aitwaye Foreigner, wimbo unaitwa 'I Wanna Know What Love Is'. Uko vizuri kaka. Respect.
 
Chini ya kapeti ni kuwa huyu LUCKY kuna mtu alimwua baada ya kuhama kwenye bendi yake, akaenda anzisha yake....

Sasa mabest zake wakaijua hiyo siri ya kifo cha jamaa, ndo wakalipiza kisasi kwa kumlima shaba lucky dube
 
Chini ya kapeti ni kuwa huyu LUCKY kuna mtu alimwua baada ya kuhama kwenye bendi yake, akaenda anzisha yake....

Sasa mabest zake wakaijua hiyo siri ya kifo cha jamaa, ndo wakalipiza kisasi kwa kumlima shaba lucky dube

WitnessJ, dunia ina maneno mengi sana. Hata kifo cha Peter Tosh, wapo waliosema kuwa familia ya Bob Marley ilihusika kutokana na kile kilichodaiwa kuwa, Peter angekuja kumfunika Bob Marley. Kuhusu huyo inayesemekana aliuwawa kwa mpango wa Dube, bila kuumauma maneno niseme kuwa uwezo wa Lucky Dube, hadhi ya Lucky Dube ilikuwa juu kuliko baadhi ya watu tunavyofikiri. Kwa hiyo isingekuwa rahisi kwa Dube kufanya mpango huo wa kumuua mtu ambaye kiukweli hakuwa na uwezo kama wake Dube. Dunia ina maneno sana ambayo usipokuwa makini, utakuta unayakubali hata kama si ya kweli. Kwa Afrika, mtu ambaye alikuwa level sawa na Lucky Dube ni Alpha Blondy toka Ivory Coast. Na kuhusu huyo unayesema aliuwawa, ukweli ni kwamba, hajauwawa ila alipata cerebral malaria sababu iliyopelekea kupoteza sauti. Senzo yupo hadi kesho ni uvumi ambao si tu ulianzia Tanzania, bali nje ya Tanzania. Angalia hii video: https://www.facebook.com/video.php?v=1063954897023421
 
RIP Dube. Reggae Strong, Together as One, I have got you baby, beautiful woman, Prisoner, Remember me, Rastafar, Taxman,War and Crime,different colors.
 
Na siku jamaa kafa Dube kahojiwa kasema hausiki ...akaongezea kuwa kama kweli kahusika kumuua jamaa na yeye basi auliwe!

So alivyouliwa kweli watu wakasema KARMA hiyoooo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…