Lucky Dube: Miaka kumi(10) tangu auawe

Lucky Dube: Miaka kumi(10) tangu auawe

Binafsi nilikuwa naamini Dube anatumia marijuana ama pombe kutokana na fujo zake kwenye jukwaa, na nilikuja kustaajabu zaidi pale alipoalikwa kwenye ile Big Brother Africa kuwatembelea washiriki wa Big Brother Africa (enzi za akina Mwisho Mwampamba). Dube alipokaribishwa glass ya pombe, alikataa kabisa kwa unyenyekevu na kusema huwa hatumii. Kitu kingine ambacho all rastas have in common, ni kwamba alikuwa mnyenyekevu sana licha ya umaarufu na mafanikio makubwa.

Nje ya jukwaa, alikua na unyenyekevu na mtu wa aibu sana. Ikija kwenye show, makamuzi yake ni balaa. Aliwahi kupiga 3 hours non stop show na mziki wake unatumia nguvu sana.

Pia alikua na uwezo wa kuimba sauti ndogo sana nyembambaaa...utaisikia kwenye Remember me, Its not easy, How will I know n.k
 
Nimeona video moja ya muandaaji wa matamasha ya Reggae toka enzi za Bob, anasema siku ya kwanza Dube anapiga kwenye tamasha hilo huko Jamaica, mambo yalisimama wakatisha tiketi, walinzi n.k wote waliacha kazi zao wakakimbilia jukwaani kumwangalia! Anasema hawakuwahi kuona show yanguvu vile Jamaica!!
RIP Lucky Dube
 
daaah Dubeeeeee, i like your muziq to the fullest,, rest in peace and not in piece rasta
 
Kwangu mimi wakati nakuwa nilikuwa nikiambiwa cheza reggae basi lazima uniwekee kaseti ya Lucky Dube, ukiweka mwengine sichezi nakwambia hiyo sio reggae.

Hadi leo hii icon wangu wa musiki huu anabakia kuwa Lucky Dube hao wengine mi siwajui.
 
Lucky Dube anatimiza miaka 10 tangu auwawe kwenye eneo la Rosettenville, Johannesburg, Afrika Kusini. Hii ilikuwa tarehe 18/10/2007.

Dube aliyeuwawa akiwa na umri wa miaka 43, alizaliwa sehemu inayojulikana kama Ermelo, Transvaal (kwa sasa Mpumalanga) mwaka 1964, Augusti, 3. Wazazi wake walitengana kabla ya kuzaliwa kwake na aliishi na mama yake ambaye alimpa jina la LUCKY kwa maana ya bahati; hii ni kutokana na mimba kadhaa kuharibika, hivyo kuzaliwa kwa Lucky Dube ilionekana kama ngekewa au bahati.

Pamoja na ndugu zake wawili Thandi na Patrick, Dube alitumia muda wake mwingi wa utotoni akiishi na bibi yake aliyejulikana kwa jina la Sarah wakati mama yake alipokwenda kazini. Mwaka 1999 kwenye moja ya interview yake, Dube alimuelezea bibi yake kama 'kipenzi chake kikubwa' ambaye alifanya kazi kubwa ya kumlea, na kumkuza Dube.

Kuanza Muziki

Katika umri wa utotoni, Dube alifanya kazi kama mtunza bustani na kadiri alipokuwa akikua, aligundua kuwa kipato alichokuwa akikipata hakikutosheleza kuilisha familia yake, ndipo Dube alianza shule. Katika mazingira ya shule alijiunga na kikundi cha muziki kilichoitwa The Skyway Band. Alijifunza na kufuata imani ya kirasta akiwa shule, na alipofikisha umri wa miaka 18 Dube alijiunga na kundi la muziki la binamu yake lililojulikana kwa jina la The Love Brothers, ambalo lilipiga muziki wa Kizulu aina ya mbaqanga. Akiwa na kundi hilo, waliweza kuingia mkataba na kampuni ya muziki Gallo Music, kampuni kubwa kabisa huko Afrika Kusini.

Dube, alivutiwa zaidi na muziki wa Jimmy Cliff na Peter Tosh toka Jamaica, na ndipo safari yake ya kuimba muziki wa reggae ilipoanzia. Mwaka 1984, alirekodi album yake ndogo ya reggae iliyokwenda kwa jina la Rastas Never Die, hata hivyo album hiyo haikufanya vizuri sokoni ambapo iliuza nakala 4000 (elfu nne) tu ukilinganisha na mauzo yaliyofanyika kwenye muziki wa mbaqanga ambapo aliuza hadi nakala 30,000 (elfu thelathini). Akiwa mwenye shauku kubwa ya kupiga vita ubaguzi wa rangi (ant-apartheid), kupitia muziki na tungo zake mbalimbali, serikali ya kibaguzi ya wakati huo ilipiga marufuku album yake mwaka 1985 kutokana na mashairi ambayo yalionekana kuikosoa serikali ya kibaguzi. Hakukata tamaa, kwani mwaka huo huo wa 1985 aliendelea kuimba muziki wa reggae na aliweza tena kurekodi album yake iliyoitwa Think About The Children iliyompa mafanikio makubwa kwa kuuza nakala na kufikia hadhi ya mauzo ya platinam na kumpaisha na kuwa moja ya wanamuziki maarufu zaidi huko Afrika Kusini na nje ya Afrika Kusini.

Mafanikio

Dube aliendelea kutoa album za reggae ambapo mwaka 1989 alishinda tuzo ya OKTV kwa album ya Prisoner, tena akashinda tuzo kutokana na album ya Captured Live (iliyotokana na onesho la moja kwa moja). Mwaka uliofuata alitoa album ya House of Exile. Mwaka 1993 album yake ya Victims, iliuza zaidi ya nakala milioni moja duniani kote. Mwaka 1995 alipata mkataba wa kurekodi na Motown moja ya makampuni makubwa kabisa nchini Amerika, ambapo Trinity ndiyo album ya kwanza kurekoodiwa na kampuni hiyo.

Mwaka 1996, alitoa album mjumuisho iliyokwenda kwa jina la, Serious Reggae Business, ambayo ilifanya awe muuzaji bora na kutajwa kama mwanamuziki mwenye mafanikio makubwa wakati wa utoaji wa tuzo za World Music Awards kadhalika kama mwanamuziki bora wa kimataifa kwenye tuzo za Ghana Music Awards. Album zake tatu zilizofuata zilifanya ashinde kwenye tuzo za South African Music Awards. Album yake ya hivi karibuni, Respect, ilisambazwa na kampuni ya Warner Music. Dube amezunguka dunia aki-perform na wanamuziki kama Sinéad O'Connor, Peter Gabriel, Celine Dion, Ziggy Marley na Sting. Mwaka 1991 aliweza kushirki tamasha kubwa zaidi la reggae sunsplash huko Jamaika ambapo aliombwa arudie tena kutokana na umahiri wake na upekee wa aina yake kama mwanamuziki toka barani Afrika.

Kifo chake

Mnamo tarehe 18/10/2007, Lucky Dube aliuwawa jijini Johannesburg kwenye kitongoji cha Rosettenville muda mfupi baada ya kuwashusha watoto wake wawili karibu na nyumba ya ndugu yake. Dube alikuwa akiendesha gari yake ya kifahari aina ya Chrysler 300C, ambayo waporaji walikuwa wakiitaka. Wauaji hao, katika kujitetea, walidai hawakujua na kugundua kuwa aliyekuwa akiendesha gari hiyo alikuwa Lucky Dube bali walijua alikuwa ni Mnigeria. Watu watano walikamatwa kuhusiana na mauaji hayo na walipatikana na hatia hivyo walihukumiwa kifungo cha maisha tarehe 31 Machi 2009. Wengine wawili walifanya jaribio la kutoroka lakini walikamatwa na wote wanatumikia kifungo cha maisha.

Hadi umauti unamfika, Dube alirekodi album 22, na ni moja ya wanamuziki wenye mafanikio makubwa zaidi toka barani Afrika. Katika uhai wake, pia aliwahi kufanya ziara nchini Tanzania mwaka 1997 na kumtania mtangazaji maarufu sana wakati huo wa kituo cha televisheni cha CTN Rahma Azizi kuwa alimpenda na angependa amuoe na kwenda naye Afrika Kusini. Tofauti na wanamuziki wengine wa reggae, Lucky Dube hakuwa mtumiaji wa marijuana au bangi tofauti na uchangamfu wake mkubwa jukwaani, ila kama ilivyo kwa wanamuziki wengine wa reggae hasa wenye imani ya kirasta, Lucky Dube alikuwa mtu mkarimu sana kwa jamii na mtu aliyejishusha licha ya umaarufu wake mkubwa duniani kote na licha ya mafanikio makubwa aliyokuwa nayo.

Lucky Dube atakumbukwa zaidi kwa nyimbo zake kama vile, Together As One, Prisoner, Reggae Strong, Different Colours One People, Remember Me, My Brother My Enemy, Serious Reggae Business, Reggae Strong For Peace, God Bless The Women, Trinity, The Way It Is, Victims, na nyinginezo nyingi.

Makala hii imetafsiriwa na imeandaliwa kwa msaada wa: mtandao wa wikipedia Lucky Dube - Wikipedia
Picha kwa msaada wa mtandao.
View attachment 611411
nimependa ulivoweka source big up sana mkuu bandiko limekaa vyema
 
Kwenye nyimbo za mapenzi kuna nyimbo kama Romeo en Julieth, I got you babe, its not easy etc. Lakini kuna wimbo wake wa Take chance.
We were only 18 years old, didn't know much about many things.
The only this we know, that we love each other.
You were a millionaire's daughter, I was a grave digger's son. They told you to stay away from me, they told me to keep away from you.
Look at now, we are living our dreams, which goes to say, love is thicker than blood.
Hiyo ngoma inaitwa Never Leave you, Mkuu, pia kuna wimbo aliurudia ninadhan hata Mariah Carey nae aliufanya pia unaitwa I want to know what love is.,
Bro wangu alikuwa na album ya Dube ilikuwa na nyimbo nyingi tu za mapenzi, jina la album limenitoka kidogo. Jamaa alikuwa vizur sana man.
 
Kweli kabisa, alikuwa ni mwanamuziki wa kipekee zaidi. Ndiye mwanamuziki niliyemhusudu kipindi cha utotoni kuliko nilivyomhusudu Bob Marley.
daah kwakweli hata mimi nilimuelewa zaidi Dube kuliko Bob...hapo kwenye "kutovuta ganja" sikubaliani na wewe mkuu!! kwa message alizokuwa ana portray kwenye jamii haiwezekani kwamba alikuwa hali ganja!! mtu wa kawaida ambaye hali majani hawezi kufikiria au kuandika mashairi kama aliyokuwa anaandika dube,tukubaliane tu kuwa alikuwa anakula ganja japo alikuwa hakubali moja kwa moja au kukataa moja kwa moja pindi akihojiwa!! tafuta ngoma yake inaitwa "rastaman's prayer", kaisifia sana ganja humo(mie sili ganja though).

saying all these,to me,Lucky Phillip Dube was a prophet
Ingzebier,Negusta Negust.R.I.P Rasta
 
Lucky Dube anatimiza miaka 10 tangu auwawe kwenye eneo la Rosettenville, Johannesburg, Afrika Kusini. Hii ilikuwa tarehe 18/10/2007.

Dube aliyeuwawa akiwa na umri wa miaka 43, alizaliwa sehemu inayojulikana kama Ermelo, Transvaal (kwa sasa Mpumalanga) mwaka 1964, Augusti, 3. Wazazi wake walitengana kabla ya kuzaliwa kwake na aliishi na mama yake ambaye alimpa jina la LUCKY kwa maana ya bahati; hii ni kutokana na mimba kadhaa kuharibika, hivyo kuzaliwa kwa Lucky Dube ilionekana kama ngekewa au bahati.

Pamoja na ndugu zake wawili Thandi na Patrick, Dube alitumia muda wake mwingi wa utotoni akiishi na bibi yake aliyejulikana kwa jina la Sarah wakati mama yake alipokwenda kazini. Mwaka 1999 kwenye moja ya interview yake, Dube alimuelezea bibi yake kama 'kipenzi chake kikubwa' ambaye alifanya kazi kubwa ya kumlea, na kumkuza Dube.

Kuanza Muziki

Katika umri wa utotoni, Dube alifanya kazi kama mtunza bustani na kadiri alipokuwa akikua, aligundua kuwa kipato alichokuwa akikipata hakikutosheleza kuilisha familia yake, ndipo Dube alianza shule. Katika mazingira ya shule alijiunga na kikundi cha muziki kilichoitwa The Skyway Band. Alijifunza na kufuata imani ya kirasta akiwa shule, na alipofikisha umri wa miaka 18 Dube alijiunga na kundi la muziki la binamu yake lililojulikana kwa jina la The Love Brothers, ambalo lilipiga muziki wa Kizulu aina ya mbaqanga. Akiwa na kundi hilo, waliweza kuingia mkataba na kampuni ya muziki Gallo Music, kampuni kubwa kabisa huko Afrika Kusini.

Dube, alivutiwa zaidi na muziki wa Jimmy Cliff na Peter Tosh toka Jamaica, na ndipo safari yake ya kuimba muziki wa reggae ilipoanzia. Mwaka 1984, alirekodi album yake ndogo ya reggae iliyokwenda kwa jina la Rastas Never Die, hata hivyo album hiyo haikufanya vizuri sokoni ambapo iliuza nakala 4000 (elfu nne) tu ukilinganisha na mauzo yaliyofanyika kwenye muziki wa mbaqanga ambapo aliuza hadi nakala 30,000 (elfu thelathini). Akiwa mwenye shauku kubwa ya kupiga vita ubaguzi wa rangi (ant-apartheid), kupitia muziki na tungo zake mbalimbali, serikali ya kibaguzi ya wakati huo ilipiga marufuku album yake mwaka 1985 kutokana na mashairi ambayo yalionekana kuikosoa serikali ya kibaguzi. Hakukata tamaa, kwani mwaka huo huo wa 1985 aliendelea kuimba muziki wa reggae na aliweza tena kurekodi album yake iliyoitwa Think About The Children iliyompa mafanikio makubwa kwa kuuza nakala na kufikia hadhi ya mauzo ya platinam na kumpaisha na kuwa moja ya wanamuziki maarufu zaidi huko Afrika Kusini na nje ya Afrika Kusini.

Mafanikio

Dube aliendelea kutoa album za reggae ambapo mwaka 1989 alishinda tuzo ya OKTV kwa album ya Prisoner, tena akashinda tuzo kutokana na album ya Captured Live (iliyotokana na onesho la moja kwa moja). Mwaka uliofuata alitoa album ya House of Exile. Mwaka 1993 album yake ya Victims, iliuza zaidi ya nakala milioni moja duniani kote. Mwaka 1995 alipata mkataba wa kurekodi na Motown moja ya makampuni makubwa kabisa nchini Amerika, ambapo Trinity ndiyo album ya kwanza kurekoodiwa na kampuni hiyo.

Mwaka 1996, alitoa album mjumuisho iliyokwenda kwa jina la, Serious Reggae Business, ambayo ilifanya awe muuzaji bora na kutajwa kama mwanamuziki mwenye mafanikio makubwa wakati wa utoaji wa tuzo za World Music Awards kadhalika kama mwanamuziki bora wa kimataifa kwenye tuzo za Ghana Music Awards. Album zake tatu zilizofuata zilifanya ashinde kwenye tuzo za South African Music Awards. Album yake ya hivi karibuni, Respect, ilisambazwa na kampuni ya Warner Music. Dube amezunguka dunia aki-perform na wanamuziki kama Sinéad O'Connor, Peter Gabriel, Celine Dion, Ziggy Marley na Sting. Mwaka 1991 aliweza kushirki tamasha kubwa zaidi la reggae sunsplash huko Jamaika ambapo aliombwa arudie tena kutokana na umahiri wake na upekee wa aina yake kama mwanamuziki toka barani Afrika.

Kifo chake

Mnamo tarehe 18/10/2007, Lucky Dube aliuwawa jijini Johannesburg kwenye kitongoji cha Rosettenville muda mfupi baada ya kuwashusha watoto wake wawili karibu na nyumba ya ndugu yake. Dube alikuwa akiendesha gari yake ya kifahari aina ya Chrysler 300C, ambayo waporaji walikuwa wakiitaka. Wauaji hao, katika kujitetea, walidai hawakujua na kugundua kuwa aliyekuwa akiendesha gari hiyo alikuwa Lucky Dube bali walijua alikuwa ni Mnigeria. Watu watano walikamatwa kuhusiana na mauaji hayo na walipatikana na hatia hivyo walihukumiwa kifungo cha maisha tarehe 31 Machi 2009. Wengine wawili walifanya jaribio la kutoroka lakini walikamatwa na wote wanatumikia kifungo cha maisha.

Hadi umauti unamfika, Dube alirekodi album 22, na ni moja ya wanamuziki wenye mafanikio makubwa zaidi toka barani Afrika. Katika uhai wake, pia aliwahi kufanya ziara nchini Tanzania mwaka 1997 na kumtania mtangazaji maarufu sana wakati huo wa kituo cha televisheni cha CTN Rahma Azizi kuwa alimpenda na angependa amuoe na kwenda naye Afrika Kusini. Tofauti na wanamuziki wengine wa reggae, Lucky Dube hakuwa mtumiaji wa marijuana au bangi tofauti na uchangamfu wake mkubwa jukwaani, ila kama ilivyo kwa wanamuziki wengine wa reggae hasa wenye imani ya kirasta, Lucky Dube alikuwa mtu mkarimu sana kwa jamii na mtu aliyejishusha licha ya umaarufu wake mkubwa duniani kote na licha ya mafanikio makubwa aliyokuwa nayo.

Lucky Dube atakumbukwa zaidi kwa nyimbo zake kama vile, Together As One, Prisoner, Reggae Strong, Different Colours One People, Remember Me, My Brother My Enemy, Serious Reggae Business, Reggae Strong For Peace, God Bless The Women, Trinity, The Way It Is, Victims, na nyinginezo nyingi.

Makala hii imetafsiriwa na imeandaliwa kwa msaada wa: mtandao wa wikipedia Lucky Dube - Wikipedia
Picha kwa msaada wa mtandao.
View attachment 611411
msh
Mkuu ukisoma haya mashairi utagundua kitu

Lucky Dube Lyrics

"Good Things"

There will be a time in your life
When you'll need me the most
But I won't be there
There will be a time in your life
When you won't need me at all
I won't be there
But while I've got the chance
I'm gonna tell you what I know
About this world we're living in
It may seem so beautiful
From where you are
It may look so innocent
In your eyes
But let me tell you
It's not a bed of roses

[Chorus: x3]
Good things come to those
Who got out and made them happen
They don't come to those who wait

I can sit here and teach you
Every trick in the book
But at the end of the day
It is your life

[Chorus: x3]
Good things come to those
Who got out and made them happen
They don't come to those who wait

You don't have to worry
The future is in your hands
[Till fade]
m

Mshikaji alikua ni bonge la Great Thinker
 
daah kwakweli hata mimi nilimuelewa zaidi Dube kuliko Bob...hapo kwenye "kutovuta ganja" sikubaliani na wewe mkuu!! kwa message alizokuwa ana portray kwenye jamii haiwezekani kwamba alikuwa hali ganja!! mtu wa kawaida ambaye hali majani hawezi kufikiria au kuandika mashairi kama aliyokuwa anaandika dube,tukubaliane tu kuwa alikuwa anakula ganja japo alikuwa hakubali moja kwa moja au kukataa moja kwa moja pindi akihojiwa!! tafuta ngoma yake inaitwa "rastaman's prayer", kaisifia sana ganja humo(mie sili ganja though).

saying all these,to me,Lucky Phillip Dube was a prophet
Ingzebier,Negusta Negust.R.I.P Rasta

Yote yawezekana Tobinho, ila katika majibu yake mbalimbali kwa maswali aliyoulizwa, alisema hatumii ganja. Kuhusu wimbo Rastaman's Prayer' toka album ya 'Trinity' iliyotoka mwaka 1995,... kwa nilivyomuelewa Dube, si kwamba alikuwa akisifia ganja/marijuana ama bangi, no, alikuwa anaelezea namna gani wanadamu tunavyomuomba Mungu kwa mahitaji yetu mbalimbali, naye (Mungu) bila hiyana hujibu maombi yetu. Mfano wanasiasa huwa wanatumia uongo zaidi na ahadi za kufikirika ili wapate nafasi wanazozihitaji, mataifa makubwa nayo huwakandamiza mataifa madogo kwa manufaa yao, ila yote haya huwa hayawezekani bila kupiga goti kwa Mungu; Wale wanaovuta bangi pia humuomba Mungu kuistawisha, unaona jinsi alichokuwa anamaanisha! Angalia hiyo mashairi hapo chini kisha uchambue. Ila pia inawezekana aliona majibu ya anatumia au kutokutumia ganja hayakuwa muhimu zaidi kwa watu. Inawezekana pia alikuwa anatumia na baadaye akaacha kutokana na labda kuwa muumini wa dini ya Kikristo ya 'shembe" ambayo yeye Dube alikuwa muumini wake.

"There comes a time
In everyman's life where he's got to face
The truth no matter what
We are coming to you father
With our sins and everything
To thank you

Those that smoke marijuana
Wanna thank you father
For making it grow internationally
They wanna thank you lord
Even though police cut it down
Sometimes they burn it down
But it grows again
Thank you father

We wanna thank you father
For everything you've given us

Nations that oppress other nations
Wanna thank you father
Even though it's painful to be oppressed
But they thank you...
For making them strong

Politicians thank you father
For making them to be able
To lie with a straight face
While the nation cries
They wanna thank you lord
 
Hiyo ngoma inaitwa Never Leave you, Mkuu, pia kuna wimbo aliurudia ninadhan hata Mariah Carey nae aliufanya pia unaitwa I want to know what love is.,
Bro wangu alikuwa na album ya Dube ilikuwa na nyimbo nyingi tu za mapenzi, jina la album limenitoka kidogo. Jamaa alikuwa vizur sana man.

Yah....alirudia wimbo wa mwanamuziki aitwaye Foreigner, wimbo unaitwa 'I Wanna Know What Love Is'. Uko vizuri kaka. Respect.
 
Chini ya kapeti ni kuwa huyu LUCKY kuna mtu alimwua baada ya kuhama kwenye bendi yake, akaenda anzisha yake....

Sasa mabest zake wakaijua hiyo siri ya kifo cha jamaa, ndo wakalipiza kisasi kwa kumlima shaba lucky dube
 
WitnessJ, dunia ina maneno mengi sana. Hata kifo cha Peter Tosh, wapo waliosema kuwa familia ya Bob Marley ilihusika kutokana na kile kilichodaiwa kuwa, Peter angekuja kumfunika Bob Marley. Kuhusu huyo inayesemekana aliuwawa kwa mpango wa Dube, bila kuumauma maneno niseme kuwa uwezo wa Lucky Dube, hadhi ya Lucky Dube ilikuwa juu kuliko baadhi ya watu tunavyofikiri. Kwa hiyo isingekuwa rahisi kwa Dube kufanya mpango huo wa kumuua mtu ambaye kiukweli hakuwa na uwezo kama wake Dube. Dunia ina maneno sana ambayo usipokuwa makini, utakuta unayakubali hata kama si ya kweli. Kwa Afrika, mtu ambaye alikuwa level sawa na Lucky Dube ni Alpha Blondy toka Ivory Coast. Na kuhusu huyo unayesema aliuwawa, ukweli ni kwamba, hajauwawa ila alipata cerebral malaria sababu iliyopelekea kupoteza sauti. Senzo yupo hadi kesho ni uvumi ambao si tu ulianzia Tanzania, bali nje ya Tanzania. Angalia hii video:
 
RIP Dube. Reggae Strong, Together as One, I have got you baby, beautiful woman, Prisoner, Remember me, Rastafar, Taxman,War and Crime,different colors.
 
WitnessJ, dunia ina maneno mengi sana. Hata kifo cha Peter Tosh, wapo waliosema kuwa familia ya Bob Marley ilihusika kutokana na kile kilichodaiwa kuwa, Peter angekuja kumfunika Bob Marley. Kuhusu huyo inayesemekana aliuwawa kwa mpango wa Dube, bila kuumauma maneno niseme kuwa uwezo wa Lucky Dube, hadhi ya Lucky Dube ilikuwa juu kuliko baadhi ya watu tunavyofikiri. Kwa hiyo isingekuwa rahisi kwa Dube kufanya mpango huo wa kumuua mtu ambaye kiukweli hakuwa na uwezo kama wake Dube. Dunia ina maneno sana ambayo usipokuwa makini, utakuta unayakubali hata kama si ya kweli. Kwa Afrika, mtu ambaye alikuwa level sawa na Lucky Dube ni Alpha Blondy toka Ivory Coast.
Na siku jamaa kafa Dube kahojiwa kasema hausiki ...akaongezea kuwa kama kweli kahusika kumuua jamaa na yeye basi auliwe!

So alivyouliwa kweli watu wakasema KARMA hiyoooo...
 
Back
Top Bottom