Ludewa yakabiliwa na uhaba wa walimu 400

Walimu wako mtaani wengi tyuuuh, wanapigana vikumbo na bahasha za kakhi mkononi, kutafuta shule binafsi.
Kazi ni kwao.
 
Walimu si ndio kada kandamizwa na mnawajaza mijini kwenye watu wengi wageuze matokeo kwetu mwanangu anadai walimu 3 wanafundisha kidato cha NNE Kiingereza walimu was sanaa wapo
 
hapo tatizo lipo kwa serikali kushindwa kuajiri walimu wa kutosha badala yake wanaajiri kidogo kidogo kitu ambacho kinafanya maeneo mengine yashindwe kupata walimu kabisa
 
Mawengi,ibihi, long time
Hatari sana huko! Kuna moto uliwahi kutokea mwaka kama sio 95 au 96, uliwazingira wakulima fulani waliokuwa wanalima kwa ushirikiano (mgowe kwa lugha ya eneo husika) ukawateketeza wote.
Miaka michache badae kama miwili kuna wazee kutoka huko wakaanza kupitia baadhi ya vijiji kukusanya madeni eti kuna baadhi ya watu walikopa mafuta yaliyosababishwa na moto ule na muda wa kulipa umepitiliza.
Kwa kipindi kile hadi majina ya wazee wadaiwa sugu yalijulikana.
 
Hii stori niliikuta 2006 pale Mawengi, nilipofika pale Ludewa niliambiwa kbs ukienda msibani usile mpk ukaribishwe.Nilitoa macho maana huku kwetu usipokula msibani ni balaa.
Kesi ya pili kuna jamaa alidaina miti ya mbao akadhinda kesi.Walipikutana kanisani yule aliyeshindwa kesi akampa salam kwa kuumpa mkono yule aliyeshinda akakataa.Basi wazee wakamwamwambia yameisa yale mpe tuu mkono mwenzako. Loih alipompa mkono ulivimba kuanzi begani mpk kidoleni.Jamaa alihangaika km mwezi kasani akawa haonekani, wale wazee waliolazimisha salam kuuliza kijana yuko wapi wakaambiwa abaumwa mbaya nyumbani.Kwenda kumuona akaanza kuwalaumu mmeona sasa mkono hauponi tiba zoote hamna kitu.Walimfata yule aliyeshindwa kesi na kumlazimisha ampomyeshe fasta mwenzie aaahh siku mbili tuu jamaa kapona.
 
Yaani mfumo wa central ajira nadhani una mapungufu makubwa.
 
Ludewa kuna ushirikina sana halafu pamekaa kushoto kweli kweli, iko mpakani
Kwa kipindi 2000 huko hadi mwenyekiti alijulikana, yaani unaumwa akipita mwenyekiti unamuuliza mbona nimetumia vidonge siponi vipi? Atakujibu km uligombana na nani mpk ukapewa hiyo homa.Ukaombe msamaha.
 
Ilikuwa ni utani tu.Don't take life so serious.
 
Moto si ajali tu km ajali zingine?
 
Waache kuloga walimu, mahakimu na watumishi wengine wa serikali
 
Acha bwana kule Ludewa kijijini kuna stori mooob na zoote za kutisha.
Inaonesha wewe jamaa ni muoga Sana hata kwa vitu vidogo.Kwanini uogope vitu visivyo na mbele wala nyuma? tena mambo ya kusimuliwa tu lkn unaogopa balaa!!!,acha hizo.Hujui kwa kuogopa huko unawatisha watu wasije kufanya kazi Ludewa?. Acha Watu waje Sisi Wana Ludewa ni wakarimu sana,ndio sababu watumishi wengi wakija huku huwa hawapendi kuhama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…