Ludovick Mwijage: The Dark Side of Nyerere's Legacy

Ludovick Mwijage: The Dark Side of Nyerere's Legacy

kama aliteswa na Nyerere pasipo sababu za kuteswa ana kila sababu ya kudai fidia ndani ya mahakama za ndani au za kimataifa.

Kama anasita kudai haki hii basi kuna kitu cha upande wa pili kinafichwa.

Wazee wa maumau Kenya wamedai fidia Uingereza na kulipwa fedha ndefu.
 
Kama habari hii ni kweli basi inakinzana na Mohammed said ambaye anadhani ni waislamu tu ndio walipata kiboko cha mwalimu Nyerere. Hii ndio mifano ilioachwa kusimuliwa na pengine mingi ipo.

Tukio lolote likisimuliwa upande mmoja linatupa mtihani wa kutafuta upande wa pili. Ni nini hasa kilipelekea haya kutokea.
 
Ulimwengu wa media siku zote huwa sio ulimwengu halisi.

Endapo tungekuwa hai miaka 50 ijayo.................Mjukuu wa Abdallah Zomba akiandika kitabu kitakachohusu maisha ya babu yake asipo- balance story ataituhumu serikali ya awamu ya nne kwa kumnyanyasa babu yake.
 
Habari hii sio ya kupuuzwa inatusaidia kumjua Nyerere pande zote mbili. Mtihani wetu ni kujua kwa nini huyu bwana aliangukia kwenye mikono ya Nyerere bila kutoka salama.

Tumekubariana kuwa hata mitume waliua wakati wa kueneza na kutangaza dini. Nyerere kama watawala wengine anaweza kufanya hayo ili kulinda mamlaka yake.

Hadi leo tunaona wasaliti wa mamlaka wanavyopata haki yao endapo itaonekana inafaa kufanya hivyo. Nani alitegemea nchi baba wa demokrasia USA ingeanzisha gereza la Guantanamo? Ni katika kulinda mamlaka.

JULIANA SHONZA atakapoandika kitabu juu ya Dk SLAA na CHADEMA kitaakisi yale yote yaliyomo kwenye tamko lake.
 
Why today this story is back? Is Mohammed Said a target? Why it is here this day..........
 
Kama habari hii ni kweli basi inakinzana na Mohammed said ambaye anadhani ni waislamu tu ndio walipata kiboko cha mwalimu Nyerere. Hii ndio mifano ilioachwa kusimuliwa na pengine mingi ipo.

Tukio lolote likisimuliwa upande mmoja linatupa mtihani wa kutafuta upande wa pili. Ni nini hasa kilipelekea haya kutokea.

Exactly lazima tujuzwe iweje amefanyiwa haya! Vinginevyo hii story sio kamili...inahitaji more inputs.Tunasahau sana kwamba a balance story wins more hearts than the cooked ones.
 
ni mimi tu au ila kitabu hakijaisha,ukurasa wa 27,story ndio ilikuwa inaanza kuwa nzuri
 
Sasa ukisoma na Kitabu NYERERE OF TANZANIA The first Decade 1961-1971(William E Smith) ndio undani wa mtu yule utaufahamu zaidi.Kwani utakua unaunganisha story zilizoachwa na bwana Ludovick
 
Ben ulikuwa unakitafuta nadhani umekipata
 
Last edited by a moderator:
Kama habari hii ni kweli basi inakinzana na Mohammed said ambaye anadhani ni waislamu tu ndio walipata kiboko cha mwalimu Nyerere. Hii ndio mifano ilioachwa kusimuliwa na pengine mingi ipo.

Tukio lolote likisimuliwa upande mmoja linatupa mtihani wa kutafuta upande wa pili. Ni nini hasa kilipelekea haya kutokea.

hii ni nchi yetu, mifano ilioachwa kusimuliwa pengine ipo.
 
KITABU KINACHOELEZEA YALIYOWAFIKA WAPINZANI TANZANIA...

Toka nchi yetu iwe huru miaka hamsini sasa hajatokea Mtanzania akaandika kitabu cha aina hii. Watanzania tunaogopa. Hofu hiyo imeenea miaka mingi na imetushika hata sisi wanahabari wenyewe

Mwandishi ni Mtanzania ambaye amekuwa mkimbizi toka alipoachiwa kizuizi alipofungwa na serikali 1983- 1985 anasema tafsiri ya kitabu kuja Kiswahili itakuwa tayari kuuzwa Afrika Mashariki (kwa bei nafuu kuliko ya sasa Majuu) mwezi Mei au Juni.
Kilichapishwa mara ya kwanza 1994 (Dark Side of Nyerere’s Legacy) na kampuni ya Wisdom House Publications kinapatikana kwenye AUDIO.

Kinapatikana:

+255 757 579305
+255 684 579305
wigotz@gmail.com
 
KITABU KINACHOELEZEA YALIYOWAFIKA WAPINZANI TANZANIA...

Toka nchi yetu iwe huru miaka hamsini sasa hajatokea Mtanzania akaandika kitabu cha aina hii. Watanzania tunaogopa. Hofu hiyo imeenea miaka mingi na imetushika hata sisi wanahabari wenyewe

Mwandishi ni Mtanzania ambaye amekuwa mkimbizi toka alipoachiwa kizuizi alipofungwa na serikali 1983- 1985 anasema tafsiri ya kitabu kuja Kiswahili itakuwa tayari kuuzwa Afrika Mashariki (kwa bei nafuu kuliko ya sasa Majuu) mwezi Mei au Juni.
Kilichapishwa mara ya kwanza 1994 (Dark Side of Nyerere's Legacy) na kampuni ya Wisdom House Publications kinapatikana kwenye AUDIO.

Kinapatikana:

+255 757 579305
+255 684 579305
wigotz@gmail.com

Teh, teh,..... wajasilia mali utawajua tu..... ona sasa wameanza kuweka na mawasiliano yao....

Mambo ya opportunism hayo....
 
Huyu L Mwijage ana kipaji kizuri sana cha uandishi..........

anaweza kuchuana na muandishi wa kitabu cha "NJAMA" almaarufu kama "WILLY GAMBA"
 
Mwalimu wangu proffessor Shazia Reuben Mnyuku aliwahi kunifundisha kuwa hakuna technolojia isiyokuwa na matatizo. (There is no rechnology with zero risk). Hivyo mi nadhani tusiangalie mapungufu bali tuchukue yaliyo ya faida na siyo mapungufu. Mapungufu tuyazingatie katika kuchukua tahadhari lakini yaliyo mema tuyaenzi. Japo kuwa Mwalimu alikuwa na mapungufu mengi, hapana shaka kazi aliyoifanyia hii nchi ni kubwa sana kulinganisha na haya mapungufu. Ndiyo maana nasema japo hatunaye bado yungali anaishi mioyoni mwa watanganyika na watanzania kwa ujumla. Nyerere ni alama ya Tanganyika na Tanzania.
 
Back
Top Bottom