tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,040
"Serikali kwanza lazima ipunguze matumizi yasiyokuwa na lazima, vikao vya watumishi wa umma vya serikali sio lazima vifanyike kwenye kumbi binafsi au Hotel binafsi, tunaweza kutumia kumbi za shule, kumbi za Halmashauri, watu wabane matumizi, posho mbalimbali za viongozi wa serikali zipungue, hata posho za Wabunge zipungue, sio mishahara ila posho" -Lugete
Ni sehemu ya yale aliyozungumza Mchambuzi wa masuala ya Uchumi Legete Mussa Lugete alipokuwa akihojiwa na Jambo TV mapema leo, Ijumaa Novemba 21.2025, akishauri namna bora ya 'kufunga mkanda' kama nchi hasa katika kipindi hiki ambacho kuna wasiwasi wa kupungua kwa misaada au mikopo kutoka nje ya nchi kutokana na yale yaliyojitokeza nchini hivi karibuni.