Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Niko kijijini kabisa huku ndanindani. Nimekuja kumzika bibi yangu aliye fariki akiwa na miaka 97 lakini akiwa bado mrembo na nguvu zake.
Kilichonuogopesha na kunishangaza, mimi wakati nakua, tulikiwa hatujui Kiswahili, tunabonga tu lugha yetu ya asili, huku tukisimuliana hadithi za Masala Kulangwa na Shing'weng'we, Kalukalanje, Ng'wanakapolo na simulizi nyingine nyingi.
Michezo yetu ilikuwa ya kiasili kabisa kutokana na mazingira yetu, mashindano ya nyimbo, kulima, kuendesha baiskeli na mitumbwi.
Shule tulivishwa bango shingoni kwa kushindwa kuongea Kiswahili. Na hata mtu asiyejua kuongea lugha ya Kibujibuji na kuongea Kiswahili pekee alioneka kama ametoka sayari ya Pluto huko.
Leo niko kijijini, watoto hawajui tena Kibujibuji, wanaongea Kiswahili, hata kanisani mahubiri sio ya kilugha tena. Hata lile bango lilioandokwa ungea Kiswahili tu tulilokuwa tukivishwa shingoni halijulikani hata lilikopotelea.
Kwa heshima na taadhima, naiomba wizara yenye dhamana ya kutunza tamaduni zetu iliangalie hili.
Sio lugha tu inayopotea inayopotea kwa kasi, ila pia vyakula vyetu, matambiko, aina ya malezi na kila kitu chetu kinapotea kwa kasi.
Tuendako tutakuja kuwa taifa lisilo na mila na tamaduni, kila kitu chetu kitapotea na tutatawaliwa kiutamaduni na mataifa makubwa