Lugha chafu, dharau na rushwa kwenye huduma za kijamii, hospitali, idara ya maji, TANESCO na ofisi nyingine za Serikali hata hili serikali mshindwa?

Kitanzania neno samahani,tafadhali lazma litumike baada ya salamu hata kwa watu wakorofi husema hvyo ni km liko automatic mdomoni..ila unaemwambia hivyo akipiga kimya na kuendelea na inshu zake hata ukirudia mara mbili mbili...utajisikiaje?

Pili wapo wale watakaoitikia lakin upande wa huduma utapigwa chenga weee,mpaka utoe kitu kidogo ndio utapata huduma kwa haraka..
 
Hilo la kusema ofisi gani kuna thread za wizara mbili kubwa ziko hapa jamii forum nlishawatumia namba za wahusika wanaowahujumu na kuwapa location na namna ya kuwakamata waohujumu ofisi zao..
Ila cha ajabu wanaomba namba yangu inbox tuwasiliane kwa kina,

Ajabu wakati nilitegemea kwa zile detail nlizowapa zilikuwa zimeshiba simu inayotumika kupigia madili nje ya ofisi ilisajiliwa kwa jina la mwanamke na misheni zao jinsi wanavyoziendesha WALA HAMNA KILICHOFANYIKA na majamaa yanapiga fedha kila siku mpaka leo..

Ile ofisi ukitaka jambo lako la halali subiri miezi mitatu na kuendelea
Ila ukitaka kwa siku tatu tu Toa MLUNGULA..
Na uzuri ile ofisi na pacha wake nchi nzima malalamiko ni yale yale mtandaoni kwa watu wote
 
Tuje na piece work system inayoondoa uhakikisho wa usalama wa ajira (guaranteed job security). Unafanya kipande cha kazi unalipwa unaaga mazima, nyuma yako mwingine anachukuwa nafasi yako. Yule wa kwanza aliyemaliza na kuaga, kesho tena njaa inamsukuma kurudi kuomba kazi kwa unyenyekevu. Heshima kwa mteja itahakikishwa.
 
Jiwe hakuimarisha mifumo ya uongozi, alikuwa ni one man show! Alijijenga yeye tu! Hivyo hali imerudi vile kwa kuwa na hili mkalitazame pia!
Afrika nzima viongozi ni one man show ndiyo watengeneze individual legacy ya kuwapa publicity not collective legacy. Hata angetengeneza mfumo bado ungebadilishwa tu. Angalia mifumo aliyotengeneza kwy sekta kadhaa imebadilishwa e.g. madini, elimu, utumishi wa umma (wakiwemo vyeti feki), vetting kwenye teuzi na ajira, mapato, safari nje ya nchi, usalama wa chakula, hifadhi ya vyanzo vya maji, maeneo ya malisho ya mifugo, kuhamia makao makuu ya nchi (kila ijumaa watumishi wanarudi Dar. Ukiwafuata Dodoma unaambiwa wako Dar, baghosha!) nk nk.
 
Nidhamu ya asili ya watumishi wa Tz ni upigaji, rushwa ikiwamo ya ngono, kutokuwajibika, kubambika kesi/kashfa, udanganyifu kwy ripoti, undugunization, ulimbikizaji kazi (work backlogs) na mengine kama hayo. Sasa mama anataka hii asili ya watumishi ndiyo iendelee as if na yeye akifanyiwa hayo ataridhika.

Theory X ya Douglas McGregor inafafanua vizuri niliyoyasema.

JPM alipambana kushamirisha Theory Y lkn hakufika mwisho.

Tuachie kizazi cha 10 kuanzia sasa ndicho kitacholeta mabadiliko, sisi acheni tuangamie tu.
 
Naunga mkono hoja...watoa huduma kutoa huduma kwa kuangalia atafaidika nini kwa muhudumiajwi(mteja) hii ndio imejenga hali ya kutojali,kutoheshimiana na uvivu makazini

Toa rushwa mfano ya laki n.k ona wanavyokuchangamkia na kukimbizana na files zako siku mbili wamekamilisha kila kitu..

Sasa hapo inamaana watoa rushwa watapewa kipaumbele haijalishi kaja muda gani..nyie wengine endeleeni kusubiri mpaka tuwamalize mabosi zetu(watoa rushwa ndio huuitwa ma BOSI)
 
Omba radhi wewe kiumbe usiyekuwa na shukrani. Ujumuishi huu kwa sekta ulizoainisha hauleti tija.
Inaonekana upo na kasoro ya kutoona jema na awamu hii.
 
Nadhan mh. rais ataanza kujua wanaomsifia sn wana malengo gani?
 
Neno..mabosi zetu(watoa rushwa)
 
Siku akija mitaa na kujionea kinachoendelea au kukisikia anaweza vunja baraza la mawaziri na kutimua makatibu wakuu wa wizara na wakuu wa idara nyingi sana
Hiyo siku ndio atajua kazungukwa na wanafki na atajua kwanini mtangulizi wake alipendwa na wananchi wengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…