Lugha chafu, dharau na rushwa kwenye huduma za kijamii, hospitali, idara ya maji, TANESCO na ofisi nyingine za Serikali hata hili serikali mshindwa?

Lugha chafu, dharau na rushwa kwenye huduma za kijamii, hospitali, idara ya maji, TANESCO na ofisi nyingine za Serikali hata hili serikali mshindwa?

Usipojua matumizi ya tafadhali, samahani, boss, mkuu, kaka, dada, mama, mwananchi, au mwanasimba, nk, wewe unapandisha kibesi utaona stress za hao watumishi wanamalizia kwako.

Unakuta limtu hata halijakusalimia linauliza, nimemkuta mkuu, nalijibu tu kamtafute.
Kitanzania neno samahani,tafadhali lazma litumike baada ya salamu hata kwa watu wakorofi husema hvyo ni km liko automatic mdomoni..ila unaemwambia hivyo akipiga kimya na kuendelea na inshu zake hata ukirudia mara mbili mbili...utajisikiaje?

Pili wapo wale watakaoitikia lakin upande wa huduma utapigwa chenga weee,mpaka utoe kitu kidogo ndio utapata huduma kwa haraka..
 
Nilishasema na ninasema tena mbona hamuwi specific kuwa ni ofisi gani na ikibidi jina la mtumishi mwenye mwenye mwenendo usiofaa au uliokukera.? Msiseme kijumla jumla hivi kwani inaonekana kama ni umbea tu na uzushi.Wapo watumishi wa umma wenye uadilifu na wanaotoa huduma kwa viwango vya juu pasipo kudai rushwa wala kutengeneza mazingira ya rushwa.Nasema wapo tena sio kidogo, wapo.Fake ID ikufanye basi kuongea kwa uwazi, kwani gharama anayoilipa Maxcence Mello ni kubwa sana kwa kutofichua real ID za members huku halafu mtu unakuja na umbea badala ya ushahidi.
Hilo la kusema ofisi gani kuna thread za wizara mbili kubwa ziko hapa jamii forum nlishawatumia namba za wahusika wanaowahujumu na kuwapa location na namna ya kuwakamata waohujumu ofisi zao..
Ila cha ajabu wanaomba namba yangu inbox tuwasiliane kwa kina,

Ajabu wakati nilitegemea kwa zile detail nlizowapa zilikuwa zimeshiba simu inayotumika kupigia madili nje ya ofisi ilisajiliwa kwa jina la mwanamke na misheni zao jinsi wanavyoziendesha WALA HAMNA KILICHOFANYIKA na majamaa yanapiga fedha kila siku mpaka leo..

Ile ofisi ukitaka jambo lako la halali subiri miezi mitatu na kuendelea
Ila ukitaka kwa siku tatu tu Toa MLUNGULA..
Na uzuri ile ofisi na pacha wake nchi nzima malalamiko ni yale yale mtandaoni kwa watu wote
 
Kwanini haya masuala yamerudi kwa kasi kwa hawa watoa huduma?

Mbona mengine hata hayaitaji fedha kutasimamia lakini wananchi wanakumbana na hii janga la kudharauriwa, kunyanyapaliwa, kukejeli, kutojaliwa na wala kutoheshimiwa... na ukitaka ukwepe hayo yote basi TOA RUSHWA..

Tunaenda wapi sasa kama nchi, mbona watumishi ni wale wale ambao kuna kipindi walionekana wameanza kustaarabika?
Tuje na piece work system inayoondoa uhakikisho wa usalama wa ajira (guaranteed job security). Unafanya kipande cha kazi unalipwa unaaga mazima, nyuma yako mwingine anachukuwa nafasi yako. Yule wa kwanza aliyemaliza na kuaga, kesho tena njaa inamsukuma kurudi kuomba kazi kwa unyenyekevu. Heshima kwa mteja itahakikishwa.
 
Jiwe hakuimarisha mifumo ya uongozi, alikuwa ni one man show! Alijijenga yeye tu! Hivyo hali imerudi vile kwa kuwa na hili mkalitazame pia!
Afrika nzima viongozi ni one man show ndiyo watengeneze individual legacy ya kuwapa publicity not collective legacy. Hata angetengeneza mfumo bado ungebadilishwa tu. Angalia mifumo aliyotengeneza kwy sekta kadhaa imebadilishwa e.g. madini, elimu, utumishi wa umma (wakiwemo vyeti feki), vetting kwenye teuzi na ajira, mapato, safari nje ya nchi, usalama wa chakula, hifadhi ya vyanzo vya maji, maeneo ya malisho ya mifugo, kuhamia makao makuu ya nchi (kila ijumaa watumishi wanarudi Dar. Ukiwafuata Dodoma unaambiwa wako Dar, baghosha!) nk nk.
 
Mama alisema hivi na hapa namnukuu: .."nidhamu kwa watumishi iliyokuwepo awamu ya Tano ilikuwa nidhamu ya woga, Mimi nataka watumishi wawe na nidhamu yao ya asili bila kuogopa Simba wa Yuda..."
Kwahiyo mkuu mleta mada huko alipo mama anafurahi sana kuona watumishi wakiwa katika nidhamu gao " natural!
Na bado tu, subiri muone matokeo ya form four ya shule za umma maana ya darasa la saba tumeyaona!
Nidhamu ya asili ya watumishi wa Tz ni upigaji, rushwa ikiwamo ya ngono, kutokuwajibika, kubambika kesi/kashfa, udanganyifu kwy ripoti, undugunization, ulimbikizaji kazi (work backlogs) na mengine kama hayo. Sasa mama anataka hii asili ya watumishi ndiyo iendelee as if na yeye akifanyiwa hayo ataridhika.

Theory X ya Douglas McGregor inafafanua vizuri niliyoyasema.

JPM alipambana kushamirisha Theory Y lkn hakufika mwisho.

Tuachie kizazi cha 10 kuanzia sasa ndicho kitacholeta mabadiliko, sisi acheni tuangamie tu.
 
Naunga mkono hoja...watoa huduma kutoa huduma kwa kuangalia atafaidika nini kwa muhudumiajwi(mteja) hii ndio imejenga hali ya kutojali,kutoheshimiana na uvivu makazini

Toa rushwa mfano ya laki n.k ona wanavyokuchangamkia na kukimbizana na files zako siku mbili wamekamilisha kila kitu..

Sasa hapo inamaana watoa rushwa watapewa kipaumbele haijalishi kaja muda gani..nyie wengine endeleeni kusubiri mpaka tuwamalize mabosi zetu(watoa rushwa ndio huuitwa ma BOSI)
 
Omba radhi wewe kiumbe usiyekuwa na shukrani. Ujumuishi huu kwa sekta ulizoainisha hauleti tija.
Inaonekana upo na kasoro ya kutoona jema na awamu hii.
 
Naunga mkono hoja...watoa huduma kutoa huduma kwa kuangalia atafaidika nini kwa muhudumiajwi(mteja) hii ndio imejenga hali ya kutojali,kutoheshimiana na uvivu makazini

Toa rushwa mfano ya laki n.k ona wanavyokuchangamkia na kukimbizana na files zako siku mbili wamekamilisha kila kitu..

Sasa hapo inamaana watoa rushwa watapewa kipaumbele haijalishi kaja muda gani..nyie wengine endeleeni kusubiri mpaka tuwamalize mabosi zetu(watoa rushwa ndio huuitwa ma BOSI)
Neno..mabosi zetu(watoa rushwa)
 
Siku akija mitaa na kujionea kinachoendelea au kukisikia anaweza vunja baraza la mawaziri na kutimua makatibu wakuu wa wizara na wakuu wa idara nyingi sana
Hiyo siku ndio atajua kazungukwa na wanafki na atajua kwanini mtangulizi wake alipendwa na wananchi wengi
 
Back
Top Bottom