Lugha chafu kwa wanandoa

mmmh! Hasara ilioje? Embu pata picha sasa maneno kama haya mnayaongea na watoto wanasikia achilia mbali majirani ambao watawasindikiza kwa vicheko vya dharau ikimaanisha nyinyi nyote mnajidhalilisha. Laiti kama mmoja angejishusha na ugomvi ukaishia chumbani wala hakuna ambae angesikia.

kugombana kupo ila yahitaji wehu wawili ili kuweza kuupeleka ugomvi wao nje ili kupata mashabiki.

Hi tabia ipo huku uswahilini kwetu. Yaani ugomvi haujaisha bila kupangiwa foleni na watu!! Halafu baadae unakuwa wimbo wa kitaa!

Aminia....! Halafu na kale kakilio flani hivi ka kwikwi ka kugushi tu, akigeuka hapo kukuangalia mwenyewe jicho nyanya!!

Nimetoka kuangalia movie moja sasa hivi inayohusu maugomvi ya ndoa divorce na misukule. Kuna jamaa ameongea point ambayo ameniacha natafakari. Alikuwa anamshauri mume (as a friend) aliyeng'ang'ania anataka divorce kuwa ndoa si love ni sacrifice. Maana jamaa alikuwa anasema anataka divorce kwani there is no love.

Anyway kutokana na hiyo movie na mimi nasema if you can't sacrifice then don't marry. Kwa sababu hilo la kuambiwa una roho mbaya sioni kama ni kubwa sana kwenye ndoa; ndoa zina mambo makubwa zaidi ya hayo ila yanabebeka kama uko tayari ku sacrifice. Hivi mnataka kunambia wadau hilo neno ni la hajabu kulisikia. Wakati mwingine laweza kutumiwa kirahisi kuonyesha kuwa umekataa kutoa msaada fulani. Kuna watu wanatukana bwana hilo la kusema roho mbaya sioni kama ni issue.

Kwa wapenzi wa movie unaweza kuiangalia hiyo movie ina fundisho sana kwa wale wanaofikiria divorce na kwa nini watu hawawezi kuacha wenza wao 100% Inaitwa "The Perfect Man" You can watch it online freely kupitia www.letmewatchthis.com

Nakubaliana na wewe mia kwa mia. Kuna dada aliolewa na Prof mmoja prof mwenyewe alikuwa geologist wa kwanza kwanza kwa hiyo pesa kwake ilikuwa si tatizo. Basi huyo mdada walikuwa wakigombana na mumewe mume anamkatia ticket ya ndege aende Nairobi aka refresh two weeks. Akirudi mapenzi yanaanza upya kwa kuwa wanakuwa wamemisiana.

Sasa kwa walala hoi na majukumu ya kazi hiyo vacation ya now and then utaiweza wapi?
Huyu dada alikuwa mfanyabiashara tu that's why aliweza kuwa anazurura.

Actually huwa inashauriwa wana ndoa wapeane space kwa mda hivi
inasaidia sana....

simple formula is never to deal with marital issues when u ar upset! its not like u ar going anywhere yet! so take ur time, think it through. unaweza ukagundua wala hamna issue ama ukaona perspective ya mwenzio kwenye hiyo issue na ukajicheka mwenyewe. na wakati wa kujicheka nadhani ni vizuri uka0share na mwenzio kuhusu ulivyokosea kimtazamo, like 'unajua juzi ilivyotokea hivi nikadhani vile na kukwazika sana. bt come to think of it, aisee i am sorry i doubted u!nimegundua u have my best interest at heart etc' itaongeza ustahimilivu na kuaminiana. lakini kama anavyosema mj1, kuna issue inafika bottom line unajikuta u just loose it! ila muhimu pia,kama mmegombana na hamjafikia sulkuhisho huko chumbani na mwenzio aka-storm out,usimfuate. ndo space anayoongelea the boss japokuwa kama una kazi ambayo ina committment and say kids at skul huwezi kuwa free tu anytime u want!

...lol,...I can't wait to provoke you nisikie hicho kishindo, ha hahahhhaa...
Eti utaruka kwenye gari yenye mwendo kasi, weeee.....mimi ukiniudhi nafungasha vinguo vyangu kwenye kimfuko cha rambo nakutishia kuondoka!

Mrembo mme uliyemchagua hawezi kuwa na roho mbaya, vinginevyo umemchoka
Labda kweli ana roho mbaya...na kumwambia sio tatizo maana akijua anavyoonekana kwa mwenzake anaweza kujirekebisha...tatizo ni walivyofikishiana ujumbe mpaka mwanainterijensia wa JF akauleta jamvini.

hiyo lugha nzuri hivyo hao wanapenda an kabisa tena sana mpendwa uwe na amanai kwanzawezekana binti ama wifi/shemeji yako ana wivu sana,,
ushauri we we wala usiingilie kesho wanakuita msaliti hao ndoa hazina ndugu mpwa...ninao ushahdi wa dadangu na kakae mpaka leo akuna anaekanyaga kwa mwenzake kisa alijitosa maneno kwa wifie loh alisoma namba

Maisha ya ndoa ni kitendawili kigumu. twashauriwa tuwe makini tufanyapo maamuzi coz ndoa ndio maisha yetu tuishio kila siku!

...lol,...I can't wait to provoke you nisikie hicho kishindo, ha hahahhhaa...
Eti utaruka kwenye gari yenye mwendo kasi, weeee.....mimi ukiniudhi nafungasha vinguo vyangu kwenye kimfuko cha rambo nakutishia kuondoka!

Ah Mbu mpaka ifikie hapo, utakuwa kweli umedhamiria!
Ufungashe, mwe! hapo utaniweza maana na uwoga nlonao ntakuwa mpole tu......ila ndo isiwe fimbo ya kila siku maana ntakuwa sugu sitatishika tena!.............hiyo ya virago nayo ah......kuna watu wamebobea!

Wadau wote mmechangia vizuri sana lakini ukweli unabaki pale pale kuwa maneno yasiyo na busara kwa wapenzi ni dalili ya kuchokana na kusababisha chuki na dharau. HONEY AU MPENZI hata siku moja haiwezi geuka ghafla kuwa nyuki,nyigu au adui na bado ikawa amani moyoni ipo.

Kiukweli hizo ni dalili za mmojawapo kuchoshwa na tabia za mwingine. Kama kuna kosa ni vizuri kusubiri wakati wa amani na furaha sana na kuliingiza tatizo katika mjadala kwa upole na upendo. Ninaamini mwenza mwenye tatizo ataelewa tu hata kama atakaa kimya lakini ujumbe utafika kwa njia nzuri ya kumfanya atafari sana bili kurusha neno chafu.

mmmmmmmmmmm sijui ukweli nini ngoja tuendelee kuona watu wanachangia nini

hujasema bro wako nae alisema nn, kwa kweli maneno ya kurushian a huwa yanabomoa sana nyumba hasa sie wanawake tuna midomo sana, mpaka mume anaogopa kurudi home, kwa kweli mie sipendi kabisa manenomaneno, ni bora hata nipigwe kwenzi

Pole sana ndugu yangu. Ugomvi katika ndoa ni vitu vya kawaida mno ila kwako wewe unayeona bora upigwe kwenzi nakupa pole. Maana ugomvi wa kwanza kwenzi, ugomvi wa pila kibao, wa tatu vibao viwili, wa nne vibao vitano, wa sita vibao vitano na teke, wa saba ngumi na mateke, wa nane ngumi mateke na stool, wa kumi yote hayo na kulala barazani, need I say more?
Maneno yanaumiza na hayafai ila uzuri wake kila mmoja ata-express anavyojisikia. Itappendeza iwapo wataambiana chumbani na yakaisha huko tusijue. But not always itafanyika hivyo.
Ndoa zinahitaji akili ya ziada kwa kweli. Msomane na mjuane vizuri.

Ndoa ni mfumo wa maisha ambao watu wawili wamekubaliana kuufuata. Si vile jamii inavyotaka au kutafsiri bali ni vile wao wenyewe wanavyojua inafaa. Kuna zile ndoa utakuta watu wanapingana wazi wazi lakini chumbani ni tabasamu tele..lakini utakuta kuna zile nyumba ambazo zina siri kubwa na utulivu lakini chumbani na moyoni kuna waka moto'.

Kwa upande wa pili, nakubaliana na "nyumba kubwa" hapo juu ya kuwa ndoa ni vile tunavyojitoa muhanga 'sacrifice' yaani ili ku-match na ku balance equation na wenza wetu tunakubali kupoteza baadhi ya vitu na tabia zetu ..yaani ni level ya tolerance ya kukubali kupoteza vile vitu ambavyo hatuendani navyo.(opportunity cost). Kama uvumilivu huu uko ndani ya uwezo wetu..basi tunaendelea vizuri..lakini kama uvumilivu huu utavuka uwezo wetu ..basi hata jamii itajua..kuna tatizo, kwani dalili za mvua ni mawingu kwa mfano ni kama pale ambapo mmoja wa wanandoa anapoanza kutafuta sehemu ya kupooza makali ya uvumilivu, wengine wanaangukia kwenye nyumba ndogo na kuna wengine wanakesha kwenye maombi ili kumwomba mola atumie nguvu zake kupunguza makali ya majaribu ya uvumilivu.

Mimi naamini sisi kama jamii hatuwezi kuhukumu upendo wa wana ndoa kutokana na ku-observe jinsi wenye nyumba wanavyopeana maneno makali, au wanavyoweza toa siri zao nje. Siri ya kitandani itabaki kitadani. Maisha na utaratibu waliojiwekea ni wao na hata siku moja hautofanana na jinsi vile mimi au wewe tunavyotaka. Labda tu kama wao wenyewe kwa sauti zao watakuja mbele ya jamii na kusema wameshindwa kuvumiliana na si kabla ya hapo.

lol! yaani siku hizi eti kuna wanaume wanazo hizi za kufunga virago! ati akiudhiana na mkewe huyoo na kafurushi kwa mamake! anaacha mke na mtoto! japo wanasema akikua ataacha,ila mweeh!
..ila ndo isiwe fimbo ya kila siku maana ntakuwa sugu sitatishika tena!.............hiyo ya virago nayo ah......kuna watu wamebobea!

Hi tabia ipo huku uswahilini kwetu. Yaani ugomvi haujaisha bila kupangiwa foleni na watu!! Halafu baadae unakuwa wimbo wa kitaa!

Nadhani hutokea sana kwa wanandoa watoto (ndoa za utotoni)kwa wanandoa ambao hawajapevuka sawa sawa ki'fikra na ki'maisha. Wakati mwingine tabia za wanandoa huwa kama tatizo!

<br /
Mimi namwambia yeye afungashe aondoke aniache na wanangu.

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…