Tatizo Watanzania wazembe, Kiswahili chenyewe uandishi wao hutia kinyaa, Kingereza hawakijui kishawapiga chenga, lugha za asili ndio hawajui hata salamu, watu wanaishi ili siku ziende tu, hamnazo kabisa.
Watu wanaanza kufundishwa Kingereza sekondari, hapo unakuta hata msomi professa anaishia kutokujiamini na ze ze ze nyingi tu. Sema watoto wa wenye hela hupelekwa shule za kimataifa wanafundishwa kingereza wakiwa wadogo, ila wakirudi nyumbani wanawakuta wazazi ni wale wale wa ze ze ze, mtoto anakosa jinsi ya kuzoea lugha.
Watoto wa makajamba mitaani ndio hoi, wao huambiwa wagande kwenye Kiswahili eti ndio uzalendo. Kisha nafasi za kazi zikitangazwa humo kunakua na kigezo kwamba 'proficiency in English is a requirement'