SoC01 Lugha ya Kingereza itumike kama lugha ya kujifunzia kwa shule zote za serikali na binafsi kuanzi elimu ya awali

SoC01 Lugha ya Kingereza itumike kama lugha ya kujifunzia kwa shule zote za serikali na binafsi kuanzi elimu ya awali

Stories of Change - 2021 Competition

Msitari wa pambizo

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2014
Posts
3,098
Reaction score
5,451
Nimefanya kazi katika taasisi za elimu kwa miaka mingi sasa. Tatizo kubwa ambalo nimekuja kukutana nalo hasa kwa graduates wa nchi hii ni uwezo mdogo wa kupambania soko la ajira linapokuja suala la kushindana na nchi nyingine.

Tatizo kubwa hapa ni Lugha ya kufundishia. Kwa sasa shule za msingi za serikali zinatumia Kiswahili. Lakini mimi nadhani hoja hii imepitwa na wakati na nadhani Kingereza kitafaa zaid kwa hoja kuu zifuatazo;

1. Zamani Kiswahili ilikuwa lugha ya pili wakati lugha ya kwanza ikiwa ni lugha za maakabila. Lakini kwa sasa Kiswahili ni lugha ya kwanza kwa jamii nyingi sana

2. Uzoefu unaonesha shule zinazkotumia lugha ya Kingereza zinafanya vizuri si tu katika mitihani lkn pia hata products zao ni marketable

3. Ni kwa nini umfundishe mtoto Kiswahili kwa miaka 10 kisha ghafla bin vuuuup umrudishe kwenye Kingereza kwa miaka yote? Huyu mwanafunzi unayemfundisha Kiswahili unataka akifika form one ndio aanze kusoma Kingereza yale aliyokuwa akiyasoma kwa kiswahili. Akimaliza chuo kikuu atakwenda kufanya usaili na kufanya kazi kwa lugha ya Kingereza. Hapana

Mwisho. Lugha ya Kiswahili tunaipenda na tuna haja ya kuienzi. Kwa kubaki na Kiswahili kama somo inatosha kuienzi lugha hii. Lakini pia bado hatuna uwezo wa kujitegemea kiuchumi kwamba tunaweza kutunisha misuli kwamba ukitaka kufanya kazi na sisi tumia kiswahili.

Waingereza wanasema. I you can't beat them, join them.

Kwa kumalizia hata wanaoututungia sera za lugha ya kutumia kufundishia watoto wao wengi wako English medium.

Nguvu kazi tunayo tafadhari sana turudi kwenye matumizi ya Kingereza kama lugha ya kufundishia
 
Upvote 3
Back
Top Bottom