Lugha za kuepuka pindi upandapo daladala.

Lugha za kuepuka pindi upandapo daladala.

Joined
Dec 11, 2010
Posts
3,321
Reaction score
6,330
Nitakupa, atakupa mbele, hujapewa mbele, utapewa nyuma, nitakupa nikikaa vizuri, ngoja isimame nikupe, subiri asimamishe nikupe, hivi nilivyo kaa nita kupaje, utapewa tulia, nikupe mara ngapi, nimempa huku mbele, msimpe huko nyuma, si nimekuambia simamisha hapo mbele, mbona nisha kupa?

Kiswahili kimepanuka na kila kikipanuka tafsiri yake pia hupanuka na wakati mwingine hata kuleta ukakasi.
 
Mkuu huu ni ukakasi wakutosha!
Lugha inakwenda mbali sana hii.
 
Na sijui tutumie maneno gani mbadala?

Mkuu cha msingi ni kuto tumia maneno au nahau zitakazo leta ukakasi. Mfano "utapata nauli yako subiri", "usiwe na wasiwasi gari ikisimama nitakupatia nauli yako".
 
Karibu kwenye "mbinu za Kiswahili" upate kudadavua na "wazee" wenzio.
 
Kama una mawazo ya bwan'Chuchu hata mtu asemeje utaona lugha ya kuepuka tu.
 
Hapo umenena ila tatizo vijana hawataki kutumia maneno mbadala ili kuondoa ukakasi
 
wewe mwenyewe mud umeshabebesha kasoro, subiri daladala ikisimama, bado mulemule, kikubwa kukaa kimpya tu! unapohisi maneno yanayotaka yakutoke huna hakika na lugha inayotaka ikitoke, kaa kimya tu, si utalipa bana? muda wake wa kumpa, no kutoa nauli utatoa, no utalipa nauli. sawa mohamedi?
 
'kuna mtu atakupa nyuma' dah, kweli haya maneno haya mmh! Si mnajua mawazo..
 
Naona tabu ni maneno : kupewa, mbele, nyuma, kusimama, kukaa vizuri. Kaaz kweli kweli!
 
kweli bana kuna dalili za umombasa humo

Mkuu kwa jinsi teknohama inavyo kuwa kwa kasi ule wigo wa kusema kiswahili au maneno fulani niya mahali fulani au yanatumika sana mahali fulani ni kujidanganya.

Mfano Uchagani nako siku hizi kumekuwa kama pwani, taarabu mpaka kwenye baa za vitochi.

Cha msingi hapa ni kujuzana ukakasi unapoweza kutokea. Umombasa, uunguja, upemba, uzanaki, ukurya au hata udigo sio wakati wake kuufikiri maana tayari tuna kifo cha muda, mipaka, umbali na nafasi. Hii inapelekea kuishi kama tuko kijijini (rejea definition ya globalisation)
 
"We konda vipi kwani nimekwambia sikupi?" Yaani ni ngumu kuepuka wakati mwingine pale konda anapokugongeagongea chenji huku akisema in a rude way "hapo dada fungua changu?" hasa wewe kwa kuhamaki utajibu hivyo ukijua fika neno nauli lishawakilishwa kwenye mgongano wa chenji na kauli ya konda
 
makonda wengine hupenda tu kujibu kwa makusudi
hivyoo
au kukuuliza 'umekaa vibaya'?lol
 
makonda wengine hupenda tu kujibu kwa makusudi
hivyoo
au kukuuliza 'umekaa vibaya'?lol

Haswaa! Lakini ni burudani ukichukulia wengine wana mahasira ya kijinga kwangu mimi i will probably laugh it off na kumzidishia raha kabisa kwa kumjibu "yaani nimekaa vibaya mnoo hata kutoa kipochi siwezi".....lol
 
Nitakupa, atakupa mbele, hujapewa mbele, utapewa nyuma, nitakupa nikikaa vizuri, ngoja isimame nikupe, subiri asimamishe nikupe, hivi nilivyo kaa nita kupaje, utapewa tulia, nikupe mara ngapi, nimempa huku mbele, msimpe huko nyuma, si nimekuambia simamisha hapo mbele, mbona nisha kupa?

Kiswahili kimepanuka na kila kikipanuka tafsiri yake pia hupanuka na wakati mwingine hata kuleta ukakasi.
Maana halisi ya neno inategemea mahali neno lilipozungumziwa, umri wa wazungumzaji na mahusiano baina ya wazungumzaji hao.
 
Back
Top Bottom