Lugumi akabidhi jengo la ghorofa 7 kwa watoto

Tajiri wa kusini

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2022
Posts
1,079
Reaction score
2,947
WATOTO ZAIDI YA 800 WAJENGEWA GHOROFA SABA ZA KUISHI DSM

Watoto yatima zaidi ya 800 katika Mkoa wa Dar es Salaam wamejengewa ghorofa saba za kuishi ili kuhakikisha kundi hilo la watoto linaishi sehemu nzuri kwa ajili ya malezi yaliyo bora

Ghorofa hizo zimejengwa na Mfanyabishara nchini @lugumisaidi ambapo amekabidhi jengo moja la ghorofa nne eneo la Kinondoni Shamba Jijini Dar es Salaam huku majengo mengine yakitarajiwa kumalizika mwezi wa tatu mwakani.

Lugumi Amesema lengo ni kusaidia na kutatua changamoto kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu huku akijitolea kusomesha watoto zaidi ya 800 kuanzia ngazi ya elimu ya Msingi hadi Chuo Kikuu.

Akizungumza kwa niaba ya walezi wa watoto hao Bi Aisha amesema majengo hayo yatawasaidia katika kuokoa fedha za kodi ya pango ambazo zitatumika kwa ajili ya kutatua vitu vingine.

FB_IMG_1735221545353.jpg
 
Hivi mnomuita fisadi na kazi zake za kuirudishia jamii tabasamu zinaonekana mnafikiria nn?matajiri wangapi wanaweza kufanya haya? Sana wakijitahidi wanapeleka vitu vinavyoisha lakini makubwa kama haya ya kuacha legacy hawafanyi..aisee binadamu hatuna jema..Aisee Bwana lugumi kama wanavyokusema eti uliiba ukafisadi iba tena na tena urudishie jamii tabasamu
 
Fedha zetu serikali imeshindwa kuzitumia vyama ...bravo bro lugumi....karume aliweza kujenga...waliopo Sasa kipaumbele NI kukopa na kukaba Kodi..khokho kikohozi
 
Acha wivu
Sio wivu...huyu jamaa ametajirika kwa tenda za serikali...serikali inatoa wapi hela ? Ni kodi zetu zimechezewa...na ndio maana kwa akili za kimaskini kama zako utaona ni wivu..ila kwa serious people kama China huyu ungekuta alishanyongwa na kuzikwa kwenye kaburi ambalo halina jina...they are the reasons tunapata huduma mbaya, poor infrastructures na fake items just to make fcked up margins %
 
WATOTO ZAIDI YA 800 WAJENGEWA GHOROFA SABA ZA KUISHI DSM

Watoto yatima zaidi ya 800 katika Mkoa wa Dar es Salaam wamejengewa ghorofa saba za kuishi ili kuhakikisha kundi hilo la watoto linaishi sehemu nzuri kwa ajili ya malezi yaliyo bora

Ghorofa hizo zimejengwa na Mfanyabishara nchini @lugumisaidi ambapo amekabidhi jengo moja la ghorofa nne eneo la Kinondoni Shamba Jijini Dar es Salaam huku majengo mengine yakitarajiwa kumalizika mwezi wa tatu mwakani.

Lugumi Amesema lengo ni kusaidia na kutatua changamoto kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu huku akijitolea kusomesha watoto zaidi ya 800 kuanzia ngazi ya elimu ya Msingi hadi Chuo Kikuu.

Akizungumza kwa niaba ya walezi wa watoto hao Bi Aisha amesema majengo hayo yatawasaidia katika kuokoa fedha za kodi ya pango ambazo zitatumika kwa ajili ya kutatua vitu vingine.

View attachment 3185659
Ni sadaka nadhifu isiyo na mawaa
 
Back
Top Bottom