MCHANGO WA MBUNGE WA JIMBO LA KISESA, MHE. LUHAGA JOELSON MPINA (MB) AKICHANGIA KUHUSU MAKADIRIO YA
MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA NISHATI KWA MWAKA 2023/2024 BUNGENI DODOMA TAREHE 1 JUNI 2023
Changamoto kwenye mradi wa LNG:
(i) Hakuna taarifa ya kufanyiwa mapitio ya PSA katika vitalu na 1, 2 na 4 vinavyokwenda kutumika katika mradi wa LNG licha ya Serikali kusimamisha mazungumzo hayo mwaka 2019 baada ya kubaini kuwa Country’s Gas Production Sharing Agreement zilikuwa na kasoro na kulifanya taifa lisinufaike vya kutosha na akiba ya gesi asilia iliyopo. PSA hizo zilikuwa zinawanufaisha makampuni ya kigeni yanayokuja kuwekeza.
Je, Government Negotiation Team (GNT) imefika hitimisho ya vipengele vya mikataba wa HGA na vitalu na 1, 2 na 4 kwa ajili ya mradi wa LNG kwa kutumia nyaraka gani au PSA zipi ili kulinda maslahi ya taifa katika mkataba huo na kama Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan alivyoagiza na kusisitiza wakati wa kusaini makubaliano ya awali.
(ii) Usiri wa majadiliano katika vipengele vya mikataba unaondelea katika mradi wa LNG unaleta hofu kubwa kuhusu vigezo na masharti ya mikataba inayokwenda kuingiwa na ni kinyume na kifungu cha 16 (1) cha Sheria ya The Tanzania Extractive Industries (Transparency and Accountability) Act 2015 ambacho kinataka miradi leseni, vipengele na mikataba kuwekwa wazi kwenye tovuti na kutangazwa kwenye vyombo vya habari.
TEITI mko wapi? Uvunjifu mkubwa wa sheria kiasi hiki unafanyika.
(iii) Majadiliano yamejikita katika kundi dogo la GNT, hadi vipengele vya mikataba vinakamilika na mikataba kuanza kuandaliwa kwa ajili ya kusainiwa hapakuwa na ushirikishwaji mpana wa wananchi, kwa mkataba mkubwa kama huu wa LNG, GNT ilitakiwa kufanya public hearing kwa kushirikisha watu wenye taaluma mbalimbali na Bunge kabla ya kufika hitimisho la majadiliano ya vipengele vya mkataba.
(iv) Kwa kuwa mkataba uko hatua za mwisho kuingiwa ni lini Bunge litashirikishwa ili kukidhi matakwa ya Kifungu cha 12 cha The Natural Wealth and Resources (Permanent Sovereignty) Act No.5 of 2017.
(v) Serikali imeingia mkataba na Kampuni ya Baker Botts LLP ya Uingereza kama mshauri elekezi katika masuala ya teknolojia, kifedha na masoko ya kimataifa ili kuuza gesi iliyogundulika kwa misingi ya ushindani na kulinda maslahi ya taifa lakini wakati huo mmoja wa wabia Kampuni ya Shell nayo inatoka Uingereza hapa tunawezaje kuzuia mgongano wa maslahi (Conflict of Interest)
Tunakwenda kuingia mkataba mkubwa wa kuvuna raslimali za taifa za gesi asilia katika Mradi wa LNG tukiwa na mambo mengi ambayo hayajawekwa wazi na pia USIRI MKUBWA unaondelea unaweza kupelekea kwenda kuingia mikataba mibovu itakayoligharimu taifa letu.
Nchi yetu haina rekodi nzuri katika eneo la mikataba ya raslimali za nchi na hivyo waheshimiwa wabunge lazima tuwe makini sana tunapofanya maamuzi.