Intelligence Justice
JF-Expert Member
- Oct 23, 2020
- 3,443
- 4,006
Kifo cha Rais wa Awamu ya 5 Dokta John Pombe Joseph Magufuli kina utata uliopitiliza na ni lazima uchunguzwe kwa sababu zifuatazoMagufuli aliugua kwa matatizo ya moyo yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu tangu akiwa Chuo Kikuu UDSM
Jenerali mstaafu Venance Mabeyo alieleza kwa uwazi mkubwa kuwa Magufuli aliugua akapelekwa hospitali ya Muhimbili baadae hali yake ikawa mbaya ikabidi wamhamishie Mzena ambapo ndipo umauti ulipomkuta, sijaona utata wowote hapo,
labda utata angeweza kuhoji kwenye chain ya utoaji taarifa baada ya Rais kufa, japo sioni ni utata wa kuundiwa tume, ila utata huu ulilletwa na serikali ya Magufuli iliyokuwepo kipindi hicho, ambaye Magufuli mambo mengi nyeti aliachwa yasimamiwe na jeshi mfano ni lile la kupora korosho za wakulima na la kupora fedha za bureau de change, hili halihitaji tume
Jingine lenye utata labda ni usiri wa kuugua kwa Magufuli, lakini hili linafahamika kuwa Magufuli alikuwa akiendesha serikali yake kwa usiri, propaganda na denial, hadi anafariki alikuwa akisema ugonjwa wa Corono ulikwishaondoka nchini kwa maombi, Maalim Seif ambaye alikuwa Makamu wa Rais Zanzibar alipougua hadi kufa serikali haikusema lolote alipokuwa akiugua
Mkapa alipougua Serikali haikusema chochohe hadi akafa
Linganisha na kipindi hiki cha Samia ambapo Mwinyi alipougua tulipewa taarifa
Mpina anataka kuaminisha wananchi kuna utata kifo cha Magufuli ila hakurejra chochote chenye utata katika hiyo hotuba yake.
Pia soma Luhaga Mpina: Kuundwe Tume ya kuchunguza 'Utata' wa kifo cha Hayati Magufuli
1. Si kawaida na kinyume na sheria kiongozi mkuu wa nchi anaugua kimya kimya wananchi oambao ni wapiga kura wa jimbo lake la uchaguzi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanafichwa kutaarifiwa
2. Kauli za viongozi mbalimbali serikali kumshutumu na kumshushia hadhi kwa mambo ambayo wenyewe binafsi zao walikuwa hawayapendi ama waliondolewa madarakani kwa makosa yao ya kiutendaji hivyo kuonesha chuki zao hadharani ili wananchi wawaunge mkono kupitia hisia za huruma kwamba kiongozi wao mkuu alikuwa ni katili
3. Watu mbalimbali walisherehekea kifo chake tena hadharani kwa kupongezana kwenye baa au hafla walizoziandaa kujifurahisha kwamba walikuwa wamebanwa kufanya mambo yao bionafsi yaliyo kinyume na maslahi ya taifa
4. Kauli ya mkuu wa majeshi mstaafu kwamba CDF, IGP na DGIS walishirikishwa kikamilifu kuanzia hatua za mwanzo za kuugua, kifo na mzozo wa ndani kwa ndani kuhusiana ni nani amrithi hapo kuna sintofahamu imejificha ambayo wanannchi wanataka kuifahamu na aliyeshiriki kwa uovu achukuliwe hatua
5. Kuenguliwa viongozi wengi wenye misimamo na uwajibikaji kwa manufaa ya wananchi kisha wakarejeshwa madarakani viongozi walioondolewa kwa tuhuma mbalimbali za kimaadili na kiharifu
6. Tarehe sahihi ya kifo cha Dk John Magufuli ni ya utata na sio tarehe 17 Machi 2021 kama ilivyotangazwa na Makamu wa Rais wa kipindi hicho maana wengine wanasema ilikuwa tarehe 6 au 10 Machi 2021 kipi kiaminike?
7. Ugonjwa unaotajwa kuwa chanzo cha kifo chake hauingii akilini kwa sababu kama alikuwa na chombo wezeshi kuishi kimefungwa mwilini kingewezekana kubdilishwa au kuhuishwa mapema kabla maana ni lazima kitoe taarifa ya ujulisho huo (alert notification). Wengine wanadai ni korona wakati wengine wanaenda mbalimbali zaidi wakidai alidungwa sindano isiyo salama kwa afya yake. Nani aaminike wakati daktari aliyekuwa akimhudumia alitengwa na daktari aliyekuwa akisemekana alikuwa hampendi JPM ndiye alichukua jukumu la uangalizi wa afya yake?
A: Mwisho hili suala la kuchunguza kifo cha JPM inawezekana serikali ikapuuza lakini halitakoma kuibuliwa kila mara kwa sababu mazingira ya kifo chake na hadhi ya cheo cha Urais ni kubwa sana kuchukuliwa juu juu ni kujidanganya.
B: Uchunguzi wa kifo cha JPM itakuwa ndio rejea sahihi na inayofumua kila kitu kifuate mkondo ili kupata ukweli kama upotevu wa baadhi ya wananchi kwa hisia ya kushughulikiwa kisiasa.
C: Usalama wa taifa ujikite kuhakikisha usalama wa taifa, rasilimali na maboresho ya kiuchumi bila kuegemea upande wa serikali pekee wakati humo ndio kuna watumishi kadhaa wasio waaminifu wanajinufaisha binafsi.
D: Chama cha mapinduzi kijiepushe kushughuulikia kinidhamu wananchi wanaojitoa mhanga kueleza mambo yaliyojificha yanayowaumiza wananchi na kuhujumu rasilimali za umma
Mwisho Paul Christian Makonda asisakamwe kwa chuki za baadhi ya wanaccm na wapinzani wasiompenda kwa kufichua uovu wao kwani kufanya hivyo kunaondoa uhalali wa kujinasibu kwamba demokrasia inajengwa na kunawilishwa wakati katika uhalisi kuna unafiki mwingi umetamalaki.