Luhaga Mpina amlipua Waziri Makamba, amtuhumu kwa Uhujumu Uchumi. Atoa wito kwa TAKUKURU kumchukulia hatua

Huku kuna ujinga mwingi sana, kundi kundi la vipofu limeibuka kumtetea huyu mama kama vile ni malaika wao, kila hoja utakayoweka kumpinga watakujibu "wewe ni sukuma gang kubali mungu wenu ameshakufa hatarudi" au wengine watasema "bora huyu kuliko yule"

Kwao kama vile bado tunaishi last year January, hawajui tuko mwaka mwingine na changamoto nyingine, wao wamekomaa tu na marehemu kama maroboti mpaka aende mtu kuya-update ndio yaanze kuhoji yanayotokea sasa.

Hizi taka zimejaa humu siku hizi zikinijibu utumbo wao nawapa na "like" kabisa ili niendelee kuwatia moyo kwenye kazi yao ya kipumbavu waliyochagua kuifanya.
 
Hili ni jambo ambalo watanzania wengi tunapaswa kulikemea, linaonekana wazi kabisa...kuna vitendo vya chini kwa chini kwa manufaa ya wajinga fulani huku wanaoteseka ni Watanzania..
Achana na kizazi cha kishetani hiko hakijui hata kufikiria. Mtu anakupa mfano wa bei ya mafuta ya US na hapa anaacha kukupa mfano za wa Zanzibar. Anasahau Marekani, nchi za ulaya na urusi wanaoneshana ubabe lazima bei zichangamke. Ukimuuliza kwann bei ya Zanzibar haijapanda kama huku anakosa majibu ya msingi. Abood ameongea point sana jana bungeni kama walimsikiliza. Vijana wajaribu kuacha ku deal na jiwe, jiwe tayari ni marehemu so wao wawe wanawaza tuliyonayo na yanayoendelea
 
Anatetea kwa kutunga tuhuma za uongo? Kwamba Waziri Makamba ndio anaweza hujumu mradi wa maslahi ya Nchi? Na Ili iwaje?

Acha upuuzi,ndio nakwambia nyie sukuma gang mtampoteza na huyu mliyemtanguliza kuwa condom

Mtapoteza wangapi…

Mwambie boss wako ajibu hoja…nchi sio ya baba yake hii….
 
Kuna Waziri ana mamlaka ya kufuta tozo bila kibali cha Cabinet?
 
Kwani uongo kuwa mnaompinga ni suku gang?
 
Laana ya kushangilia kifo cha Magufuli haitawaacha salama, walidhani kuongoza ni jambo rahisirahisi kama kujibatiza jina la kigogo2014 huko twita.
Binafsi nilishangilia na bado nashangilia sana kifo cha yule nyapara
 
Amemlipua nini?
 
Watu wanataka umeme, kama hakuna umeme utashambuliwa tu hii siyo nchi ya mama yako

Mpina anatakiwa apigwe risasi kama Lisu, abambikiwe kesi au atekwe. Enzi za Magufuli ulikuwa ukihoji mambo ta serikali hayo ndio yalikuwa malipo yake.
 

πŸ‘‡πŸ’πŸ’πŸ’
Your browser is not able to display this video.
 
Duuuuh!
 
πŸ‘‡πŸ’πŸ’πŸ’
Your browser is not able to display this video.
 
wakulane tu kwani wao si ndio walisema watanzania hawana akili hata wakifanywa nini
 
Huyo Mpina na CCM yake na wabunge wake na katiba yao na washirika wao wote ni wanafiki.
Mwaka mzima Sasa Kuna Wabunge 19 bungeni wanakwapua pesa za Kodi za wananchi kinyume Cha Sheria na katiba ya nchi. Mbona hakuona kuwa ni uhujumu uchumi?
Mbona hakusema kuwa spika ajiuzulu ?
Kipi chema kuwapunguzia watanzania Bei ya mafuta au kuacha wabunge wezi 19 kuiba fedha za umma wakati tozo zinaongezeka na Bei ya mafuta kupanda.

Fukuzeni wabunge 19 na warudishe fedha walizoiba wakishirikiana na spika Kisha tumbane Waziri Mkuu na Waziri wa fedha ili watuambie Kwa Nini mpaka Sasa wapo kwenye ofisi za umma zilizojaa magari ya anasa na kujenga majengo ya umma ya anasa ya Kwa pesa za kupandisha Kodi na tozo kwenye mafuta ya chakula na Petroli na sukari na ushuru wa mazao ya wakulima na pembejeo badala ya pombe na sigara ambazo ni vitu vya anasa.?

Ndio maana tunataka Katiba mpya.
Katiba mpya itaweka misingi ya kuwapata viongozi wema kwenye Taifa hili lenye wahuni wengi wenye fedha na madaraka.
Kama pangekua na uhuru wa kisiasa na haki na uchaguzi huru bila shaka Mbunge Mpina asingeweza kujitokeza na kupinga Suala la wanyonge kupunguziwa Bei ya mafuta Kwa sh.100/- Hilo lingemcost sana mana wananchi walishangilia na kuona kuwa Januari ni Waziri aliyeguswa na ugumu wa maisha unaosababishwa na kupanda Kwa Bei ya mafuta kutokana na tozo nyingi.

Ni wazi kabisa kuwa wabunge wa CCM na Washirika wao walipitisha tozo nyingi kwenye mafuta,Luku, simu, mazao, na kila mahali lakini hawakuona haja ya kupunguza matumizi ya kifahari kwao na kupunguza posho zao kwenye nchi yenye maskini na ukosefu mkubwa wa ajira.

Waulize wanadai posho na mishahara mikubwa ili Nini hawana jibu zaidi ya kufanya ufuska na uhuni na ulevi TU.
Akitokea Waziri akapunguza tozo wanamshambulia mana wanadhani kuwa anatafuta umaarufu.
Lakini hata kama Waziri atapata umaarufu haijalishi mana Tunataka umaarufu unawagusa wanyonge.
Ndugai alijaribu kupinga tozo za Ewura alionyesha kuwa Ile ni kampuni ya wezi. Alishauri tutumie tbs mana ni shirika la umma. Sasa unajiuliza Vipi Kuna tbs na Ewura Kwa wakati mmoja halafu Ewura inachukua tozo kubwa na kuwaumiza wananchi. Nini kazi ya tbs?

Sio Makamba mbaya Bali mifumo na katiba ya hovyo ndiyo inayowaleta wabunge wa hovyo wenye kujali maslahi yao na kushindwa kuwajali wananchi na kupunguza kero zao.

Ni Tanzania TU ndipo ambapo wabunge wanaungana kuwapandishia wananchi Kodi na tozo huku wao wakiwa na maisha ya anasa na starehe kwenye soko lile lile na kuzuia mishahara ya watu wa chini isipande.

Niwakumbushe TU Makamba ,Mwigulu, Nape ,Jafo, Ridhiwani ,Zito Kabwe na Ado Shaibu kuwa Wasidhani kuwa katiba ya Sasa ina mustakabali mwema kwao. La hasha ni Kwa muda TU.
Katiba mpya ndiyo itakayojenga misingi Bora kwao na kwa familia zao na Kwa Taifa Zima la Leo na Kesho. Kwa Katiba hii na Dunia inakokwenda uchumi unadoda halafu unakua na wabunge aina ya Mpina na Zungu na Waziri wa fedha na serikali isiyojua wakati mgumu wa maisha Kwa watu wa chini na Nini Cha kufanya Kwa majanga ya uchumi wa kidunia na kuzuia kupanda bei holela, halafu wanatumia katiba ya hovyo kuzuia watu wasichague viongozi waadilifu wenye uchungu na maisha ya wanyonge Iko siku watashangaa.

Hii katiba mbovu inawanufaisha wazee waliovuruga nchi kipindi Cha Mkapa. Wazee walikwapua Mali za umma na kujimilikisha . Hao wanaona katiba hii ni Bora sana mana walifanya uovu ambao umelindwa na katiba hii. Walipaswa wawe magerezani na wengine wawe wamefilisiwa Mali zao ili Watoto wa mama Tanzania wasipate shida mpaka ya mafuta ya kupikia chakula. Walikwapua viwanda vilivyokuwa vinazalisha mafuta ya kupikia kuanzia mafuta ya karanga ,siagi n.k . Wakawapa matapeli wa kihindi Kwa mgongo wa nyuma. Mabilionea wote wa kihindi nyuma yao Kuna wanasiasa wa awamu ya Tatu. Leo hii nchi yenye mazao ya chikichi, korosho,karanga,alizeti,ufuta, makweme, mawese, pamba, na kila aina ya mimea inayotoa mafuta na mifugo lakini Bei ya mafuta tunapangiwa na matapeli wanaojiita wawekezaji wakishirikiana na wanasiasa wa CCM.

Sasa nimkumbushe January Makamba kuwa ajiuzulu Kisha aungane na Jenereli Ulimwengu kudai katiba mpya.
Aungane na Ndugai kudai uhuru wa nchi dhidi ya Mabeberu ,vita vya Urusi vinapandisha Vipi Bei ya Miwa ya sukari na alizeti wakati wakulima ni wavuja jasho wasiotumia gesi ya Urusi. Mikopo ndiyo inayotufikisha hapa mahali pa kupangiwa na hao Mabeberu wa magharibi na Mashariki.
Makamba ajiuzulu aungane na Polepole kupinga uhuni na wizi wa Mali za umma.

Makamba ajiuzulu akae pembeni mana amepigiwa kelele za kutosha na wanaCCM wenzake ambao wapo Kwa ajili ya matumbo yao.

Makamba ni Mzalendo wa kweli Historia itamkumbuka.
Jambo alilo lifanya Makamba ni la kizalendo Kwa wanyonge. Kumpunguzia mnyonge sh.100 imewatoa roho Majambazi yanayouza mafuta na kuhonga wabunge.

Hivi ni nani kati ya anayepinga kuondolewa Kwa tozo au anayeongeza tozo Kwa wananchi wote mil. 60 ni Mzalendo. Bila shaka Januari anaguswa na hali ngumu za watanzania. Anaumia kuona wananchi wanapandishiwa Bei kila siku.
Makamba Amejaribu kuonyesha uzalendo wake Kwa watanzania lakini wanaosaka Mali na ukubwa hawaoni wanataka ajiuzulu eti amekiuka katiba na kulisababishia Taifa hasara.
Hiyo hasara. Blalifuli.

Hivi kazi ya serikali ni kuwaumiza wananchi au kulinda maisha yao kulingana na uwezo wao?

Mishahara Iko chini, mvua hazikunyesha za kutosha. Biashara nyingi zilisimama. Wanasiasa wengi wanaotokana na jitihada zao walienguliwa na kunyanganywa kura na kukosa ajira wengine mpaka Leo ni wagonjwa na wengine wamefungwa ,hali ya maisha ni ngumu ,uchumi unayumba kila mahali Duniani. Serikali isingekua ni hii ya wezi na wahuni wa CCM Leo hii wangefanya mabadiliko makubwa ya kupunguza tozo , kupunguza mishahara ya watawala, kupunguza tozo au kufuta tozo za wakulima zinazowanufaisha wahuni wanaojiita mawakala wa kutoza maushuru ya wakulima na kupeleka kiduchu kwenye Halmashauri. Wizi mtupu Kwa wakulima.
Serikali ingekua sio ya CCM na washirika wake wanaoangalia maslahi yao Leo hii ingefuta posho zote zinazozidi 100, 000/- Kwa siku zinazotolewa Kwa majaji, wabunge,Mawaziri n.k ili pesa hizo zitumike kwenye kuongeza uzalishaji wa ndani unaofanywa na wazawa na ubunifu upewe kipao mbele.

Nilitegemea Waziri Mkuu na Waziri wa fedha waje na mkakati wa Kupiga marufuku gari zote za kifahari kwa Watawala na viongozi wote. Kama mtu anataka gari ya kifahari anunue Kwa pesa zake.

Leo hii Kuna watumishi wa kawaida sana lakini wanaogelea kwenye magari ya kifahari na kutumia mafuta Kwa Kodi ya maskini huku bidhaa zikipanda Bei . Watu hawajadili haya wanajadili Waziri aliyepunguza Bei ya mafuta. Watanzania tumelogwa na nani?
Tulipaswa tuandamane kumpinga Mpina anayefurahia kupanda Kwa Bei ya mafuta.

Ni mara ngapi bunge limekaa kimya mabilioni ya fedha za umma yakitumika Kwa mambo yanayolitia Taifa hasara kubwa lakini Kwa sababu yanakuja na Rushwa wanakaa kimya.?

Hivi nani asiyeona wabunge wanapokaa kimya mikataba mibovu ikiwa inapitishwa ? Hivi nani haoni wabunge wanaokaa kimya Mawaziri wa Elimu wakija na mitaala mibovu na kujipatia Tenda za kubadili vitabu kila mwaka huku wananchi wakipoteza Kodi zao Kwa serikali Kununua vitabu vipya kila mwaka Kwa sababu ya Waziri mmoja mhuni na mlafi akishirikiana na wabunge wanaomiliki mashule na wamiliki ambao wengi wao walikua watumishi wa umma na viongozi.

Ni Mbunge Gani au mtawala yupi ndani ya CCM na washirika wake haoni jinsi ambavo Pesa za Tassaf zinavyotafunwa Kwa vikao huku walengwa wakiwa hata hawajulikani.?

Ni mwanaCCM yupi ambaye amewahi kusimama na kuhoji juu ya mabilioni yanayotolewa Kwa kukimbiza Mwenge huku vitu vikipanda Bei.!!
Au ni Mbunge yupi wa CCM anayehoji kuhusu mabilioni yanayotolewa kama mikopo kule Halmashauri kutumika kisasa na kuwakopesha wanaCCM wasio na mbele wa nyuma halafu zinapotea na uchaguzi ukipita wanapita Kwa wizi wa kura halafu pesa zinapotea na wanasubiri uchaguzi Mwingine?
Kama unajua utaiba kura Kuna haja Gani yakutumia mabilioni ya pesa kufanya kampeni na wasanii kila mahali na kuwanunua mabodabida na Bajaji na kugawa pesa vijijini ?
 
Kwahiyo unashauri nini, uozo uendelee ?? Hakuna kumtaja mwenzake? Haujaeleweka hoja yako ni nini. Ingekuwa hivyo unavyofikiria hakuna hakimu hata mmoja angemfunga binadamu hata mmoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…