Pre GE2025 Luhaga Mpina amshtaki Spika Tulia na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuondolewa Bungeni kinyume na Sheria

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Jioni Njema
Huku si jioni.

Hujaweza kufuatilia hoja yangu.

Nimeandika Spika anaweza kushitakiwa mahakamani. Akimpiga jirani yake anaweza kushitakiwa mahakamani.

Ila, kwenye suala la anavyoendesha Bunge, ukimshitaki Spika mahakamani, mahakama itakataa kusikiliza hiyo kesi na kukwambia Bunge ni muhimili unaojitegemea, Spika anavyoendesha Bunge ni suala la Bungeni, Mahakama haiwezi kuhukumu suala hilo kwa kuangalia separation of powers. Pelwka malalamiko yako Bungeni mkayamalize huko.

Usichoelewa kipi hapo?
 
Hahaha! Dah! Na hayo mengine huwa unayafuatilia hadi mwisho?

Au unaachana nalo na kuendelea tu na jingine?
Mimi na Watanganyika wenzangu ni kama mbwa anayefukuza kila gari analoliona hatujii tushike lipi , ghafla bin vuu unashangaa 2025 hii hapa😄
 
Vipi covd 19
 
Katiba ndo Mama Kwa mihimili yote hakuna aliyejuu ya katiba Kama Kuna haki za kikatiba zimevunjwa lazima haki ifuatwe.
Ukumbuke pia hao wabunge hawajateuliwa na spika kama ulivyotolea mfano wa raisi anayeteua na kutengeu bali ni wananchi waliwapigia kura Kwa kufuata taratibu zote za kikatiba
 
Kama Spika hawezi kuwajibishwa, kutakuwepo na shida kwenye “checks and balance”

Mahakama bado inaweza kutoa ufafanuzi kwenye hili suala.

As far as I know, checks and balance is a principle of government under which separate branches are empowered to prevent actions by other branches.

Mahakama itatoa ufafanuzi na mwishowe tutarudi tu kwenye kutaka katiba mpya endapo kutaonekana kuna utata wa kikatiba kwenye maamuzi kutolewa.
 

Nakwambia hivi, Spika ni mkuu wa muhimili, mahakama haiwezi kuhukumu kesi ya jinsi Spika anavyoendesha bunge.

Wapi katiba inaruhusu Spika kushitakiwa mahakamani kwa suala la jinsi anavyoendesha Bunge?

Soma hapa imeelezwa vizuri separation of state ni nini na mihimili inaweza kuingikiana vipi (kwa mfano kwenye impeachment procedute ikiyoandikwa kwenye katiba). Hakuna sehemu ambayo kuna provess ya kumshitaki Spika mahakamani kutokana na anavyoendesha Bunge.


View: https://medium.com/@amirihamisi1996/separation-of-powers-in-tanzania-theories-and-reality-d313b003bdc4
 
Kwa mahakama hizi sitegemei lolote la maana kwani ni kashfa kwa serekali.
 
Mahakama ilishatoa ufafanuzi kuhusu hili, na kuna precedent tayari kwenye kesi inayofanana na hii ambayo haikuwa this clearcut. I forgot the case.

By the way, hili si suala la Tanzania tu, mabunge karibu yote ya Westminster yana kipengele hili.

Na zaidi, hili si suala la Spika tu. Hata mbunge hawezi kushitakiwa mahakamani kwa mambo aliyoyafanya ndani ya bunge akifanya kazi zake za kibunge. Analindwa na "parliamentary immunity".

Yani kwa mfano, hata Mpina akionekana kapika data, kachafua watu, kwa maneno ya uongo aliyoyasema Bungeni, kama mbunge, Mpina hawezi kushitakiwa na kuhukumiwa mahakamani, kwa sababu ana parliamentary immunity. Mahakama itasema hili ni shauri la Bunge. Lipelekeni kwa Spika mkamalizane Bungeni huko.

Sasa kama Mpina hawezi kushitakiwa na kuhukumiwa na mahakama kwa suala la bungeni, Spika atashitakiwa vipi?
 
Hiyo kesi haina mashiko, proceeding za Bunge zina kinga chini ya sheria na katiba, atapigwa kama ngoma
Shida ni katiba. Rais akiamuwa hakuna muhimili wa kumzuia.

Hata kwenye hii issue mwamuzi wa mwisho ni Rais.

Maghufuli alikuwa mkweli aliposema “serikali ni muhimili uliojichimbia kuliko mihimili yote”, pale alipokuwa akijibu swali la Pascal Mayalla aliyemuuliza Maghufuli yeye kama mkuu wa serikali ni kwanini anatoa maagizo kwa mahakama kuhusu mwenendo wa kesi.

Bunge na mahakama haviwezi kuwa mihimili huru yenye kufanya kazi inavyotakiwa chini ya katiba hii.
 
Nafasi ya Spika ipo kwa mujibu wa Katiba, na atatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba, sheria, taratibu na kanuni, akikiuka na ikathibitishwa amekiuka, Spika anaweza kuondolewa.

Kwenye mihimili mitatu, yote ina majukumu ya kutenda kwa mujibu wa Katiba, ikitokea mihimili mmoja umekiuka mamlaka yake, then hii mihimili mingine ina jukumu la kuufanyia checks and balance.

Na kwa mujibu wa kesi ya Mpina dhidi ya spika, anadai kwamba sheria imekiukwa kumuondoa bungeni.

Sasa utaratibu uliopo, Bunge lina jukumu la kutunga sheria, Mahakama inatafsiri sheria na Serikali inatekeleza sheria.

Labda kama ikiwezekana uweke hiyo kesi inayoonyesha “precedent” ili tuweze kufanya “reference”

Pia nafahamu kuhusiana na kinga ya bunge kuhusu yanayozungumziwa mule ndani. Lakini kwenye issue hii, ni suala la ukiukwaji wa katiba na sheria.
 
Spika akiharibu, Bunge lina utaratibu wa kumuwajibisha, mpaka kumuondoa kwa kura ya kukosa imani na kumvua Uspika.

Ukileta issue ya Spika kuharibu iamuliwe mahakamani, mahakama itakurudisha Bungeni na kukwambia Bunge lenu lina utaratibu wa kumuwajibisha Spika anayeharibu, mahakama hairuhusiwi kuingilia mambo ya bunge linavyoendeshwa.

Hapa checks and balance ina apply kwa kutoruhusu mahakama kuliingilia bunge. Ukiruhusu mahakama iamue bunge liendeshwaje, hapo ndipo umeharibu checks and balance.

Mahakama haiwezi kumuwajibisha hata mbunge tu kwa mambo anayoyafanya bungeni, kwa sababu ya parliamentary immunity, itakuwa Spika, ambaye ni mkuu wa muhimili wa bunge?
 
Issue hii tumeshaijadili sana humu. Na kama sikosei hakuna “precedent” spika au bunge kushitakiwa mahakamani.

However nakumbuka mijadala ambayo tulipata “insights” flani kutoka kwenye michango ya Petro E. Mselewa, Mzee Mwanakijiji pamojq Na Pascal Mayalla , especially kipindi kile cha sakata la Job Ndugai na CAG. Pia suala la wale wanachama wa chadema almaarufu “COVID 19”
 
Hata Mzee Mwanakijiji alishawahi kuandika hapa…

 
Kuna kesi ambayo ilipelekwa mahakamani, mahakama ikasema haiwezi kuhukumu kesi hiyo, kwa sababu ilikuwa ni kesi ya shauri la bunge, na mahakama haitakiwi kuhukumu kesi za mambo ya bunge linavyojiendesha, mahakama ikasema shauri hilo lirudi kumalizwa bungeni.

Nimesahau tu ilikiwa kesi gani.

I suspect kesi hii, kama itasikilizwa, inaweza kusikilizwa kwenye hoja nyinginenyingine tu lakini hii ya kumshitaki Spika mahakamani is a complete non starter.

Huyo Mpina mwenyewe tu, mbunge, ikigundulika alisema uongo bungeni, kapika data, kapakazia watu kwa uongo, ndani ya bunge, kama mbunge, hawezi kushitakiwa na kuhukumiwa mahakamani. Kwa sababu ana parliamentary immunity.

Itakuwa Spika, mkuu wa muhimili wake?
 
Speaker anajiona mungu mtu kazi kutafuta nyadhifa nje ya nchi huku uspeaker nyumbani umemshinda. Msisahau kile kisa cha kupitisha fasta mkataba wa bandari. Mkataba ulisemekana haufai hata kulumangia ugali.
 
Kifungu cha 29 D na E cha Sheria na Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge sura namba 296 ndiyo msingi wa kesi hiyo. Kusema bunge tena ndo likaamuwe kama limefuata sheria na katiba au la, kutakuwa hakuna mantiki ya “checks and balance”

Mahakama inaweza kutoa tafsiri endapo Katiba na sheria vimekiukwa kwenye maamuzi dhidi ya Mpina.
 
While there’s a separation of powers, there’s also check and balance of power.

Unafahamu maana ya Judicial Review?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…