Pre GE2025 Luhaga Mpina amshtaki Spika Tulia na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuondolewa Bungeni kinyume na Sheria

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wasi wasi wangu huyu Ngosha watu wa usalama wanaweza kumfanya kitu kibaya sawa na Dr Ulimboka miaka ile ya awamu ya nne.

Ni kama ana chuki dhidi ya SSH ni kama haamini kuwa JPM hayupo tena pale ikulu.
 
Mahakama inafuata sheria. Usifanye kosa la kuchanganya sheria na haki.

Mahakama zishawahi kutupa kesi za mashauri ya bunge kwa msingi wa kutenganisha nguvu za Bunge na Mahakama.

Nimeuliza swali hujanijibu, sijui kama hata umelielewa.

Mahakama haiingilii Bunge. Hii ni mihimili tofauti na yote inajitegemea. Sijui watu hawaelewi hii kanuni au vipi?

Hii kesi ya Spika na masuala ya Bunge linavyoendeshwa itasikilizwaje na Mahakama bila Mahakama kuingilia uhuru wa Bunge?

Huoni kwamba Mpina alitakiwa kwenda Bungeni na kuweka motion ya kumpigia Spika kura ya kukosa imani, Spika awe impeached? Wabunge wamalize mambo yao Bungeni bila ya kuingia kwenye mtego wa kupeleka kesi Mahakamani halafu Mahakama ikatae kusikikiza kesi kwa sababu ni jambo la uendeshwaji wa Bunge, na Mahakama haiwezi kuingilia mambo ya uendeshwaji wa Bunge?
Upuuzi umejaa Tanzania hii.
 
Wasi wasi wangu huyu Ngosha watu wa usalama wanaweza kumfanya kitu kibaya sawa na Dr Ulimboka miaka ile ya awamu ya nne.

Ni kama ana chuki dhidi ya SSH ni kama haamini kuwa JPM hayupo tena pale ikulu.
Ni kweli wanaweza kumfanya hivo, ila wajue ipo sehemu tunaelekea, na kwa kufanya hivyo watakuwa wanatusogeza kwa mwendo wa kasi bila ghasi.
 
Aliposhughulikiwa yule Dr nini kilifanyika?. Serikali inafanya mengi sana na yanagusa moja kwa moja maisha ya mtu mmoja mmoja.

Uwe na hoja ya kina kuweza kushawishi umma unaotatuliwa matatizo yao kila kukicha.

Uelewa pia ni tatizo la kitaifa, Mpina alipinga sana uwekezaji pale bandarini kwa hoja ndefu akiwa haelewi kwa uhakika nini kinakwenda kufanywa.
 
Kwan Kesi ya MPINA Kwa Spika ni juu ya Adhabu, au Kanuni na Sheria ambazo zilikiukwa katika kufikia Hukumu hiyo??.

Na kama Kanuni na Sheria zinakiukwa na Bunge, ni nani hasa Sasa mwenye MAMLAKA ya kuzitafasiri ?.

Swali la Mwisho, mawakili zaidi ya 100, Hawa wote Hilo hawalijui kiasi kwamba Kiranga ndio unalijua pekeako??. 🤣
Kesi ya Mpina ni kuhusu nini?

Kanuni na sheria za Bunge zinapokiukwa hilo ni jambo la Bunge, mwenye mamlaka ya kuzitafsiri ni muhimili wa Bunge, si Mahakama. Mahakama inatafsiri sheria za nchi, si kanuni za Bunge.

Mawakili wanaweza kujazana hata 1,000 kuonesha solidarity na Mpina kwamba kaonewa, au hata kula hela za Mpina, au hata kusikia Mahakama itasemaje, wakijua kwamba kesi haina mashiko Mahakamani na itakataliwa.

Na kwa mawakiki wetu hawa wengine siwezi jushangaa hata wakiamininkwamba wana kesi wanayoweza kushinda, tuangalie mahakama itasemaje.

Mimi natabiri kuwa, kwenye hoja yoyote ya kumshtaki Spika kwa jinsi alivyoliendesha Bunge, mahakama itatupilia mbali shauri hilo, kwa kisema haiwezi kuingilia suala la Spika anavyoendesha Bunge, hilo ni suala la kumalizwa Bungeni.

Hizi kesi nyingine ni za kisiasa za kujenga sympathy kwenye public opinion kuliko kutafuta ushindi Mahakamani.
 
Inawezekana ni sahihi kufungua kesi mahakamani, hilo si swali langu, na wala sijapinga hilo.

Nilichouliza ni kwamba, Mahakama inaweza kusikiliza kesi na kutoa hukumu ya kuhusu shauri la Bunge lilivyojiendesha lenyewe, kwa kuzingatia kuwa Mahakama haitakiwi kuingilia shauri la Bunge linavyojiendesha, kwa sababu kusikiliza na kuhukumu mashauri ya hivyo kutakuwa ni kuingilia uhuru wa Bunge kujiendesha lenyewe?

Huoni kwamba hii kesi itatupiliwa mbali na Mahakama, na Mahakama itasema "Hili ni jambo lenu la Bungeni, mna utaratibu wenu wa kumaliza mashauri yenu ya Bungeni, sisi Mahakama hatutakiwi kuingilia mashauri yenu ya jinsi mnavyoendesha Bunge kwa sababu kufanya hivyo kutaingilia uhuru wa Bunge na kuharibu kanuni za separation of powers"?

Huoni kuwa kesi itatupiliwa mbali kwa mantiki hii?
Mkuu kumbuka mchakato wote wa ndani ya Bunge ulishafanyika kwahiyo kwa mujibu wa katiba yetu chombo pekee chenye uwezo wa kutoa haki na chenye uamuzi wa mwisho ni mahakama.

Kwamba Bunge linaweza kumtimua mbunge yeyote na mbunge huyo akaishia kukaa benchi kisa tu ya doctrine of separation of power?

Mahakama yenyewe itakachozingatia ni kwamba all procedures zilifuatwa wakati wa mchakato wa kumsimamisha mbunge ikiwemo 'natural justice' ambayo ni haki ya kusikilizwa kikamilifu.

Sioni kama mahakama itatupilia mbali shauri hili kwa kufanya hivyo manake imeacha jukumu lake la kikatiba la kutoa haki pasipo kujali haki hiyo imevunjwa na nani ama na muhimili gani.
 
Mawakili wa Luhaga Mpina wanazungumza na waandishi wa habari muda huu.

Pamoja na nambo mengine, mawakili hao wamesema mojawapo ya kesi zilizofunguliwa ni ile anayomshtaki Spika wa Bunge na Mwanasheria mkuu wa Serikali kwa kunyang'anywa na kunyimwa haki ya kuwakilisha wananchi wa kisesa na watanzania wote kwa vikao 15 Bungeni ambapo msingi wa kesi yake anaamini ameonewa kwa kuondolewa kinyume cha Sheria.

Aidha, Mpina anaamini hatua za kuchukuliwa dhidi yake zilikuwa zimepangwa hata kabla ya yeye kusikilizwa.

Hadi sasa, zaidi ya Mawakili 100 wamejitolea kumsaidia Mpina kwenye kesi hii.

===

Kesi (ya kupitia uhalali wa kisheria kuhusu utolewaji wa vibali vya kuagiza sukari) imefunguliwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam ambapo mdai ni ndugu Luhaga Mpina, ambao anawashtaki ni Waziri wa Kilimo, Bodi ya Sukari, viwanda vya ITEL, Zenji Industries, Waziri wa Fedha ambaye yeye anashtakiwa kwa kutoa misahama ya kodi ya VAT (Kodi ya Ongezeko la Thamani) ambapo Mpina anadai hata taarifa ya msamaha wa kodi haikuchapishwa katika gazeti la serikali, lakini pia Mpina amemshtaki Kamishina Mkuu wa TRA kwa kutokudai na kukusanya kodi kwa watu waliopewa vibali vya kuagiza sukari lakini wa mwisho kushtakiwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, shauri hilo liko mahakamani tayari.

Pia soma

HUYU JAMAA ANASHINDA KESI WAPENDWA

MWABUKUSI PART TWO

NIKOKWA WAKALA
 
Haya ndiyo mambo tunatakiwa kubwa busy nayo na story za Simba na Yanga
 
Kwahiyo More than ya mawakili 100 , hawajui Sheria linapokuja suala la Bunge?.

Ila wee chiembe ndio unajua ?

Toa upuuzi wako.
Idadi sio issue, hata wewe nyumbani kwako unaweza kuwa na mbuzi au kondoo 10000, lakini hawawezi kukutisha, hizo kesi zinasaidia academics tu, hakuna namna mahakama itaingilia Bunge
 
Inawezekana ni sahihi kufungua kesi mahakamani, hilo si swali langu, na wala sijapinga hilo.

Nilichouliza ni kwamba, Mahakama inaweza kusikiliza kesi na kutoa hukumu ya kuhusu shauri la Bunge lilivyojiendesha lenyewe, kwa kuzingatia kuwa Mahakama haitakiwi kuingilia shauri la Bunge linavyojiendesha, kwa sababu kusikiliza na kuhukumu mashauri ya hivyo kutakuwa ni kuingilia uhuru wa Bunge kujiendesha lenyewe?

Huoni kwamba hii kesi itatupiliwa mbali na Mahakama, na Mahakama itasema "Hili ni jambo lenu la Bungeni, mna utaratibu wenu wa kumaliza mashauri yenu ya Bungeni, sisi Mahakama hatutakiwi kuingilia mashauri yenu ya jinsi mnavyoendesha Bunge kwa sababu kufanya hivyo kutaingilia uhuru wa Bunge na kuharibu kanuni za separation of powers"?

Huoni kuwa kesi itatupiliwa mbali kwa mantiki hii?
Mfano Rais yupo muhimili wa Executive ambapo mwajiriwa aliyefukuzwa kazi na mwajiri wake anaweza kuanzia ngazi za usuluhishi kama CMA akakata rufaa hadi kwa Rais akitka arejeshwe kazini lakini Rais anaweza kushikilia msimamo wa mtu huyo kutorejeshwa kazini.

Mtu huyo akienda mahakamani (Labour division) kudai haki yake ya kurejeshwa kazini haina maana kwamba mahakama itakataa kusikiliza shauri lake kisa tu muhimili mwingine ulishamfukuza kazi.

Shauri litasikilizwa na kama mtu huyo ana haki basi atarejeshwa kazini.

Rejea mamlaka ya kuteua ambayo yapo vested to the President.
Rais anaweza kumteua mtu yeyote kushika madaraka ya ofisi yoyote ya umma lakini kama kuna ukiukwaji uliofanyika kwenye zoezi zima la uteuzi labda mtu huyo kukosa sifa fulani basi mtu yeyote anaweza kwenda mahakamani kupinga uteuzi huo.

Rejea kesi ya Addo Shaibu dhidi ya Rais Magufuli na mwanasheria mkuu wa serikali ambapo Addo Shaibu alipinga uteuzi wa Adelardus Kilangi kuteuliwa kuwa mwanasheria mkuu wa serikali.
 
Idadi sio issue, hata wewe nyumbani kwako unaweza kuwa na mbuzi au kondoo 10000, lakini hawawezi kukutisha, hizo kesi zinasaidia academics tu, hakuna namna mahakama itaingilia Bunge
Kwa nini Watanzania wengi inaonekana hawaelewi hii point ya msingi kabisa?

Hivi watu wetu hawajui basic separation of powers hivi?
 
Mfano Rais yupo muhimili wa Executive ambapo mwajiriwa aliyefukuzwa kazi na mwajiri wake anaweza kuanzia ngazi za usuluhishi kama CMA akakata rufaa hadi kwa Rais akitka arejeshwe kazini lakini Rais anaweza kushikilia msimamo wa mtu huyo kutorejeshwa kazini.

Mtu huyo akienda mahakamani (Labour division) kudai haki yake ya kurejeshwa kazini haina maana kwamba mahakama itakataa kusikiliza shauri lake kisa tu muhimili mwingine ulishamfukuza kazi.

Shauri litasikilizwa na kama mtu huyo ana haki basi atarejeshwa kazini.

Rejea mamlaka ya kuteua ambayo yapo vested to the President.
Rais anaweza kumteua mtu yeyote kushika madaraka ya ofisi yoyote ya umma lakini kama kuna ukiukwaji uliofanyika kwenye zoezi zima la uteuzi labda mtu huyo kukosa sifa fulani basi mtu yeyote anaweza kwenda mahakamani kupinga uteuzi huo.

Rejea kesi ya Addo Shaibu dhidi ya Rais Magufuli na mwanasheria mkuu wa serikali ambapo Addo Shaibu alipinga uteuzi wa Ardelarus Kilangi kuteuliwa kuwa mwanasheria mkuu wa serikali.
Mahakama zenyewe zinasikilizia Rais ameamkaje siku hiyo hizo nazo ni Mahakama?
 
Back
Top Bottom