Inawezekana ni sahihi kufungua kesi mahakamani, hilo si swali langu, na wala sijapinga hilo.
Nilichouliza ni kwamba, Mahakama inaweza kusikiliza kesi na kutoa hukumu ya kuhusu shauri la Bunge lilivyojiendesha lenyewe, kwa kuzingatia kuwa Mahakama haitakiwi kuingilia shauri la Bunge linavyojiendesha, kwa sababu kusikiliza na kuhukumu mashauri ya hivyo kutakuwa ni kuingilia uhuru wa Bunge kujiendesha lenyewe?
Huoni kwamba hii kesi itatupiliwa mbali na Mahakama, na Mahakama itasema "Hili ni jambo lenu la Bungeni, mna utaratibu wenu wa kumaliza mashauri yenu ya Bungeni, sisi Mahakama hatutakiwi kuingilia mashauri yenu ya jinsi mnavyoendesha Bunge kwa sababu kufanya hivyo kutaingilia uhuru wa Bunge na kuharibu kanuni za separation of powers"?
Huoni kuwa kesi itatupiliwa mbali kwa mantiki hii?