Luhaga Mpina anaongozwa na chuki na ukabila kuliko uzalendo na ukweli. Ushahidi huu hapa

Masitting kabisa wewe
 
Zitto Kabwe ni kweli kuwa hujawahi kuona madudu ya rafiki yako Makamba aliyoyafanya akiwa Waziri wa Nishati ?
Kama sio udini na ushikaji wenu kwa nini umtetee January Makamba?
Wakati Watanzania wote wanajua madudu ya Makamba ni makubwa kuliko ya Dotto Biteko.
Ushikaji na udini usikutoe kwenye reli .
 
Ukiishiwa hoja na kuna hoja za kujibu unaweza andika uharo kama huu wa mleta mada..
 
Huo ufisadi wizara ya Nishati umeanza waziri akiwa nani? Biteko au Makamba?!

- Zile $30 mil kwa ajili ya maintanance waziri alikuwa Makamba.

- Rushwa ya kugawa mitungi ya gas bungeni siku ile hotuba ya bajeti ya wizara ya Nishati ikisomwa, waziri alikuwa Makamba.

Hiyo ni baadhi tu nimekuwekea hapo kukuonesha kwanini Mpina amekomaa na Makamba, sijui kwanini unakuwa mkali Mpina kumtaja Makamba.
 
Una hoja za kitoto ujue
 
Tuseme ukweli. Je hakuna tatizo kwenye suala la sukari iliyoagizwa bila kulipiwa kodi?. Sasa hivi wananchi wanaolima miwa wameshindwa waipeleke wapi miwa yao. Soko limejaa kutokana na sukari iliyoagizwa bila kulipiwa kodi. Hivi Serikali liko kwa ajili ya wananchi au watu wachache?.
 
Kwahiyo kama Makamba na Maharage waliiba na kuharibu waachwe tu Kwa sababu waliiba na wameondoka??

Wewe ni mjinga mmoja
 
Mjinga mmoja!! Ukandamizaji wa mafisadi??

Na hao unaowasifia ni kwasababu wanakula na wezi!!

Huna akili
 
Kwa thread hii moja kwa moja ninakupa title ya MNUFAIKA wa madudu ya Makamba.

Ina maana wewe ulikuwa diaspora kipindi cha giza totoro la umeme kabla Biteko hajapewa kijiti?

Haya mambo anayojitokeza Mpina na kuyafafanua kabla ya kuyapeleka mahakamani, alishahangaika nayo huko huko Bungeni muda mrefu sana, ingia You Tube utayapata.

Tumpe shime Mpina kwa kuthubutu angalau kuonesha nia ya kuchukia ufisadi kwa vitendo kuliko maneno yako ya kufisha moyo ya ukabila.
 
Hauko serious na kumfuatilia ufisadi wa rafiki yako January. Tunaleta taarifa za Mpina enzi za January akiwa waziri unazifanya as if zimesemwa Leo,?

Mpina Katoa vielelezo, vyako viko wapi?
 
Kwenye hoja ya sukari wangalau Mpina amesimama sehemu sahihi. Lakini kwenye hii vita yake, siwezi kumtenganisha na vita ya sukuma gang v/s msoga gang. 50/50 kwenye mizani yangu, ana hoja sahihi, lakini iliyo nyuma ya vita vmya makundi.
Lakini si anatetea mali za umma?
 
Achana na hao akina mama wa UWT
 
Hakuna ukabila mnataka kupotosha wahuni wahed nyie. Wakabila na wadini tunawafahamu sana.
 
ufisadi wizara ya Nishati umeanza waziri akiwa nani? Biteko au Makamba?!
Ufisadi upi huo? Alichosema Mpina ni kuna pesa tunapaswa tudai ila hatujadai sababu ya hongo, sasa nachojua waziri ni Biteko je naye hajadai pesa za CSR na IPTL sababu kahongwa pia? Kama ni hapana kwanini bado hajazidai, na kama hajazidai why Mpina hajaelekeza lawama huko?
Rushwa ya kugawa mitungi ya gas bungeni siku ile hotuba ya bajeti ya wizara ya Nishati ikisomwa, waziri alikuwa Makamba.
Mbona Mpina hajaongelea hii kwenye video? Kagusia tu IPTL, Bwawa la Nyerere na pesa za CSR!! Mfano pesa za CSR za mwaka 2023 je Biteko amezidai? Kama hajazidai why lawama iwe kwa Makamba?

Mimi nataka kujua why Biteko haguswi
 

Jibuni hoja zake badała ya kumtia ila asokuwa nayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…