Luhaga Mpina: Deni la Serikali lapaa kutoka Trillion 62.4 mwaka 2021, Hadi kufikia Trillion 96.9 mwaka 2024 !!

Luhaga Mpina: Deni la Serikali lapaa kutoka Trillion 62.4 mwaka 2021, Hadi kufikia Trillion 96.9 mwaka 2024 !!

Kosa la Mpina ni lipi hapo mkuu?

Miaka 4 unakopa Trilioni 33plus.

Akipewa mingine 5, deni litakua Trilioni 150.

Kizazi kijacho kitatushangaa sana tuliongozwaje na watu wa namna hii?

Mikopo inaenda kwenye pikipiki nchi nzima, samia legal aid(unajiuliza rais tena unatoa msaada wa kisheria, si ubadili sheria ama uboreshe sheria tu?)

Hiyo mikopo ndio inaenda kwenye mara samia scholarship, sasa bodi ya mikopo ipo ya nini? Inaenda kugharamia mamilioni wanayopewa kina Mwamposa(mwamposa alipaswa kua jela mwaka 2020 aliua watu Moshi na bado yuko uraiani)

Serikali haitaki kusimamia ukusanyaji kodi, inaona ikope kuliko kuhimiza kulipa kodi.

Unajiuliza miaka 5 ya Samia hakuna ufisadi mkubwa mkubwa Tanzania, watanzania wote wameokoka, mbona hakuna fisadi hata mmoja alieshitakiwa ama mafisadi wote waliokoka kipindi hiki cha Samia?

Hii nchi chini ya vegetables haiwezi kwenda mahala popote.
Unakopa hela halafu una wachukua akina Steve Mengele kuwapeleka Korea sababu ni chawa wa mama
 
Kuna shida gani ukikopa hizo hela? Mbona huulizi matumizi ya mikopo?

Nchi zote Zenye maendeleo Zina madeni makubwa sana

Pili pikipiko na Mali zingine za chama zimenunuliwa Kwa hela za chama so Wacha propaganda za kijinga.

Samia Scholarship ni program ya bodi ya mikopo,inaonesha huelewi unachoongea.

Kuna Serikali imekusanya hela nyingi Toka uhuru kuzidi ya Samia? Na hakuna mwaka TRA imewahi kusanya chini ya asilimia 97%

Ufisadi ambao wewe unaujua na kuwajua ilitakiwa kuwaumbua na kuutaja ,kama umeshindwa manake hakuna udhibiti wa Serikali ni mkubwa.

Mbona Nchi hii ni Kati ya Nchi 10 Zenye maendeleo makubwa Afrika? Unaswmaje haijafika popote? Huoni unakuwa mjinga?View attachment 3217948
Nani aliyetoa hizi takwimu isiwe ni babu Wassira
 
Back
Top Bottom