Luhaga Mpina, kwanini umewaroga Watanzania?

Mushkov

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2024
Posts
357
Reaction score
686
Tangu hukumu ya Mpina itolewe pale Bungeni, vijiwe na maeneo yote yenye mikusanyiko wanamlilia Mpina na wamewachukia kabisa wanaojiita Wabunge.
Zaidi ya 98% wanaona Mpina hakutendewa haki.

Zaidi sana wameichukia serikali hii kwa kiwango kisichoelezeka, hasa kwa kosa la kuwakumbatia MAFISADI.

Hukumu ya Mpina imeweka mambo wazi kabisa kwamba kwa serikali hii, MAFISADI wanalindwa na kutetewa na mihimili yote ya serikali na wanaowafichua MAFISADI wanapigwa mawe na mihimili yote ya serikali.
Zaidi sana watu wanamkumbuka mtumishi wa Mungu, JPM.

Pia soma Bunge lajadili juu ya adhabu ya Mbunge Luhaga Mpina. Laamua kumfungia vikao 15
 
Bashe anatuhumiwa kulidanganya bunge na watanganyika, badala ya kujitokeza personally ajibu tuhuma za Mpina dhidi yake, kamati ya bunge ndio inajitokeza kumtetea baada ya kukutana na Bashe vichochoroni na kuyamaliza.

Hawa wajinga kwa akili zao mbovu wanataka kutuaminisha lile suala limeisha na Bashe ni msafi, kama Bashe ni safi kwanini asijitokeze mbele ya waandishi wa habari akajibu tuhuma dhidi yake?

Watanganyika sio wajinga, Bashe ni mchafu mpaka siku atakayojitokeza personally kujibu tuhuma dhidi yake kama zilivyotolewa na Mpina.

Spika Tulia ni mchafu kwa kumkingia kifua Bashe, na mama Abdul ndio mchafu zaidi kuendelea kukaa na waziri kwenye serikali yake aliyeshindwa kujibu tuhuma dhidi yake.
 
Zaidi sana watu wanamkumbuka mtumishi wa Mungu, JPM.
Kunaweza kuwa na ukweli katika hili,...'qualified truth'.
Nilicho ipendea mada yako hasa hasa ni maelezo haya uliyoweka hapa chini:
Zaidi sana wameichukia serikali hii kwa kiwango kisichoelezeka, hasa kwa kosa la kuwakumbatia MAFISADI. Hukumu ya Mpina imeweka mambo wazi kabisa kwamba kwa serikali hii, MAFISADI wanalindwa na kutetewa na mihimili yote ya serikali na wanaowafichua MAFISADI wanapigwa mawe na mihimili yote ya serikali.
 
Mi ninachoshangaa hata wale waluomchukia JPM wanamkumbuka. Kwamba Bora yule alikua na mapungufu mengine Kwa wanasiasa ila kwenye uchumi na kuwajali wanachi angekua hai tungekua mbali.

Nikashangaa sana, tajiri uliemchukua Leo hii unamkumbuka duuhh, Hali sio poa.
 
Ni kweli kabisa, leo wafanyabiashara wote wanasema bora wakati wa JPM kwa sababu hizi:-
1. Wakati wa JPM, wafanyabiashara walisisitizwa sana kulipa Kodi ya biashara yao lakini hawakuhujumiwa kama ilivyo sasa. Leo hii mtu ana mtaji wa milioni 5, ikitokea ameuza bila kutoa risiti akakutwa na watu wa TRA anaambiwa alipe fine milioni 15,000,000/=. Hapo kama siyo ukichaa ni nini?

2. Sababu ya pili wanasema kwamba, wakati wa JPM watu walilipa kodi lakini waliona matunda ya kodi zao tofauti kabisa na sasa ambapo asilimia kubwa ya kodi wanazolipa zinawatajirisha MAFISADI ambao wanalindwa na utawala.
 
Tangu hukumu ya Mpina itolewe pale Bungeni, vijiwe na maeneo yote yenye mikusanyiko wanamlilia Mpina na wamewachukia kabisa wanaojiita Wabunge.
Zaidi ya 98% wanaona Mpina hakutendewa haki.

Zaidi sana wameichukia serikali hii kwa kiwango kisichoelezeka, hasa kwa kosa la kuwakumbatia MAFISADI. Hukumu ya Mpina imeweka mambo wazi kabisa kwamba kwa serikali hii, MAFISADI wanalindwa na kutetewa na mihimili yote ya serikali na wanaowafichua MAFISADI wanapigwa mawe na mihimili yote ya serikali.
Zaidi sana watu wanamkumbuka mtumishi wa Mungu, JPM.
Sahihi kabisa
 
taja chama chako cha siasa tuweze kutathmini hayo maoni ya vijiwe vingi kihusu huyo muungwana :pulpTRAVOLTA:
 
Ndani ya CCM aliyebaki na Legacy ya Magufuli nI Mpina pekee na sasa wameapa kufa nae.. Kifupi CCM wameamua kula naye sambamba...mbaya zaidi Msukuma kigeugeu leo anajifanya kumkaanga ndugu yake Mpina ambapo kipindi Jiwe akiwa hai ndiyo alikuwaga chawa mkuu wa Sukuma ngang.
 
Tangu hukumu ya Mpina itolewe pale Bungeni, vijiwe na maeneo yote yenye mikusanyiko wanamlilia Mpina na wamewachukia kabisa wanaojiita Wabunge.
Zaidi ya 98% wanaona Mpina hakutendewa haki.

Zaidi sana wameichukia serikali hii kwa kiwango kisichoelezeka, hasa kwa kosa la kuwakumbatia MAFISADI. Hukumu ya Mpina imeweka mambo wazi kabisa kwamba kwa serikali hii, MAFISADI wanalindwa na kutetewa na mihimili yote ya serikali na wanaowafichua MAFISADI wanapigwa mawe na mihimili yote ya serikali.
Zaidi sana watu wanamkumbuka mtumishi wa Mungu, JPM.
Moja ya kitu ambacho Tanzania kinatusumbua Bado ni woga kwa baadhi ya watu. Nimejalibu kusikiliza hatua kwa hatua suara hili nimeona Bado sana tunajikongoja kuelekea kule. Mtu mmoja anahojiana na bunge Zima yeye ana hoja wao Wana maneno. Sijapenda hii. Lkn acha kazi ienderee
 
Back
Top Bottom