GE2025 Luhaga Mpina: Kwanini uwe mshindani ambaye unategemea Vyombo vya Dola?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
Akizungumza leo Septemba 13, 2025 katika Makao Makuu ya ACT Wazalendo, Mgombea Urais wa Chama hicho, Luhaga Mpina amesema:

Vyombo vya Dola vitupe ulinzi tu, usitumie nguvu ya Dola kupata ushindi, kama Watanzania hawakutaki nenda nyumbani ukapumzike.

Vyombo vya Dola visitumike vibaya kwa kuwa unaweza kushiriki kufanya hujuma kisha ukashangaa Mpina anatangazwa mshindi, utaweka wapi sura yako.

Vyombo vya Dola vifanye kazi yao kisha viache mambo mengine yaamuliwe katika uzinduzi wa kura.

Mtajulishwa kuhusu ratiba ya Kampeni na michakato mingine.
 
Sawa. Ngoja tuone kama hivyo vyombo vya dola vitamsikiliza na kuyatii haya maneno yake.
 
Akizungumza leo Septemba 13, 2025 katika Makao Makuu ya ACT Wazalendo, Mgombea Urais wa Chama hicho, Luhaga Mpina amesema:

Vyombo vya Dola vitupe ulinzi tu, usitumie nguvu ya Dola kupata ushindi, kama Watanzania hawakutaki nenda nyumbani ukapumzike.

Vyombo vya Dola visitumike vibaya kwa kuwa unaweza kushiriki kufanya hujuma kisha ukashangaa Mpina anatangazwa mshindi, utaweka wapi sura yako.

Vyombo vya Dola vifanye kazi yao kisha viache mambo mengine yaamuliwe katika uzinduzi wa kura.

Mtajulishwa kuhusu ratiba ya Kampeni na michakato mingine.
Ni Mgombea yupo anategemea vyombo vya Dola ?? Yule 100bn, au wale wenye 100m
 
Back
Top Bottom