Akichangia hotuba ya waziri wa viwanda na biashara, mbunge Kisesa, Luhaga Mpina ameongelea mambo mbalimbali ikiwemo uhusiano kati ya sekta binafsi na umma, mikataba mibovu ukiwemo wa Tanesco na Symbion, bilioni 70 za mkataba wa maendeleo ya tehama Tanesco na Mahindra ya India, mkataba mpya unaokuja TPA, bei ya mafuta nchini na mfumuko wa bei.
=======
Luhaga Mpina: Suala la uwekezaji wa Serikali na sekta binafsi linahitaji kuangaliwa kwa makini sana, mikataba mingi tuliyoingia inanyonya mapato ya nchi, uchumi wa nchi, inahamisha rasilimali, inapora ajira za watanzania.
Sasa hivi TPA nae ameanza kutafuta mbia, mikataba ya namna hii lakini ipo mikataba inayotusumbua mpaka sasahivi ya TRA na sicpa. Ipo mikataba tumeingia majuzi ya India Mahindra na Tanesco zaidi ya bilioni 70 kwaajili ya kuendeleza mifumo ya Tehama wakati wataalamu wa tehama tunao hapa wa kila aina wanaoweza kudevelop mifumo ya Tehama. Vijana wetu wamedevelop mifumo kama GPG, POS na hata Maxmalipo, leo unaenda kutafuta mfumo India kwaajili ya kufanya nini?
Sasa hivi naskia symbion wanapigiwa chapuo tuilipe bilioni 356 lakini inapigiwa hili chapuo wakati huohuo hatuambiwi alieingia mkataba huo na kutusababisha tuwe na mkataba ambao hatuwezi ku-exit hata kama mkataba unatuingizia hasara, amechukuliwa hatua gani?
Wabunge tukataeni mikataba ya namna hii lakini tukataeni hata kulipa hizi fedha, uchunguzi ufanyike kilichojificha nyuma ya Symbion.
Mikataba yote ambayo tunaitambulisha kama mikataba mibovu iitishwe hapa bungeni tuweze kuifuta.
Mwisho Luhaga Mpina ameongelea mfumuko wa bei nchini na kusema pamoja na Covid na vita lakini mfumuko umechangiwa na kukosekana uadilifu na usimamizi makini.
Mpina amesema upangaji holela wa bei kinachoshangaza kwanini wahusika hawajachukuliwa hatua. Amedai waziri anawajua waagizaji wa mafuta nje ya nchi, ngano na anawajua wazalishaji wa ndani ya nchi.
Amenifurahisha binafsi sana kwa kutaja dalili za nia mbaya ya Serikali ya Samia kutoka kusimamia uadilifu na kukuza ufisadi.
Kwa mfano ni dalili za kuipigia chapuo kampuni ya Symbion kutoka Marekani kulipwa mabilion eti fidia wakati mkataba ulisimamishwa na walikaa kimya bila shaka kwa kukubaliana na hoja za kuvunjiwa mkataba.
Kuwalipa Symbion kwanza itakuwa kufungua pandora box kwa mikataba ya kifisadi iliyovunjwa kuanza kuidai nchi kama ile iptl kampuni ya iliyochezesha rumba nchi muda mrefu hadi Hayati Magufuli alipoingia madarakani au ile kampuni ya Richmond iliyosumbua hadi ikafikia kujiuzulu Waziri Mkuu.
Lingine ni hili la TANESCO kuingia mkataba na kampuni ya wahindi eti wao kuweka mfumo wa computer kusimamia management.
Tangu January Makamba aingie uwaziri kila mzalendo muamini wa falsafa ya kijamaa hajafurahia. Ila sio hilo ila ni mashaka na uadilifu wake au mtazamo wake.
Nchini kuna ujuzi mkubwa wa kuunda mifumo ya computer sasa kukimbimia wahindi bila shaka ni maslahi ya kifisadi tu.
Kwanza hasara ya kutumia mfumo wa wahindi ni kutoa fursa kwa wahindi kutuhujumu mipango yetu ili tuendelee kuwa tegemezi.
Jamaa namuelewa ana pointi nyingi za msingi sana, ameamua kuweka maslahi ya taifa mbele hata kama yatagharimu ubunge wake mbele ya safari, huyu kwangu ndie mzalendo.
Watakaompinga nawashauri wampinge kwa kujibu hoja zake, sio zile kelele za wakati wake alifanya nini, kuendelea kujidumaza kwa majibu mepesi kama hayo ni kuliangamiza hili taifa.
Ni kweli alikuwa kimya, lakini haya anayaongea Kuna hoja kubwa sana.
Ni CCM wote wapo hivyo, hata Nape baada ya kuwekwa pembeni alianza kuongea bungeni na kukosoa.
Mwisho Luhaga Mpina ameongelea mfumuko wa bei nchini na kusema pamoja na Covid na vita lakini mfumuko umechangiwa na kukosekana uadilifu na usimamizi makini.
Hawa ndio Akina MAGUFULI, TUNAOWATAKA WAWE WENGI WENGI .
Haya angeyasema lissu ungekuja kusema "mwanasheria msomi katapika nondo" kwakuwa ni mtu ambaye humpendi ata kama kaongea jambo la maana unadhiaki, ndo maana chadema mmepoteza ushawishi kwa wananchi.
Asante wewe umeongea ukweli, ifike mahala, sio kila mwana CCM anayetofautiana na mamlaka akaitwa sukuma gang, sababu hii inawapa nguvu sana wapigaji na wale wote wenye nia mbaya na hii nchi.