Luhaga Mpina: Mfumuko wa bei umetengenezwa. Ataka uchunguzi kilichojificha Symbion na mikataba mibovu ikafutwe bungeni

Luhaga Mpina: Mfumuko wa bei umetengenezwa. Ataka uchunguzi kilichojificha Symbion na mikataba mibovu ikafutwe bungeni

Serikali ipo pale kwa kazi gani, nini majukuku ya serikali makini?

Unafikiri JPM angeruhusu huu ujinga, asingeweka mikakati.

Hii serikali kila kitu wanaongeza, wanasingizia Corona, Vita. Hawana uchungu na maisha ya Watz wa kawaida.
Nakubaliana na wewe ni jukumu la serikali unakosea pale angekuwa JPM angeruhusu hapo ndio kuna shida. Tanzania sio kisiwa ok JPM amefariki RIP kwani serikalini watu waliofanya kazi na JPM hawako? Tunataka mawazo mbadala nini kifanyike hakuna serikali inayoongozwa na mtu mmoja kuna watu nyuma. Kumbuka mafuta ya kula na sukari yalianza kupanda wakati wa JPM sio leo alifanya nini? Rais Samia kosa kubwa kutegemea walewale hana washauri wazuri katika mambo ya uchumi. Tatizo la serikali ya CCM nasema tena ni walewale. Na hii hata wapinzani walete mawazo mbadala tusilalamike tu shida tunaijuwa nini kifanyike?
 
Mpina amekosea nini mkuu?!

Nyerere alisema nini kuhusu wasukuma ebu tujuze
Mpina yeye analalamika tu kutwa sijamsikia akija na solution, kasema inflation imetengenezwa sasa aseme aliyetengeneza nani? dhumuni nini? na solution ni nini? kuongea rahisi tu hawahawa hata siku moja wakati ule hakukuwa na hata mmoja kuuliza pesa inatoka wapi wakati ilikuwa inajulikana ni mikopo tena bank za kibiashara lakini kimyaa wote. unafiki kitu kibaya sana hata yule mbunge wa Mtera alisema sisi wanafiki mtu mmoja to Lazaro alisema wazi hawezi kufanya kazi na JPM wazi na akaondoka wengine wote wakae kimyaa wanafiki. Nakubaliana kitu kimoja Rais Samia ana watu wa hovyo katika baraza lake la mawaziri wa hovyo sana tu.
 
Kuna mifumo mingi sana imetengenezwa na watanzania.eg : ehms ,gothomis ,etc.ni kutojiamini tu na kutoamini vya kwako!! Inawezekana ni kulipa fadhila???
 
Akichangia hotuba ya waziri wa viwanda na biashara, mbunge Kisesa, Luhaga Mpina ameongelea mambo mbalimbali ikiwemo uhusiano kati ya sekta binafsi na umma, mikataba mibovu ukiwemo wa Tanesco na Symbion, bilioni 70 za mkataba wa maendeleo ya tehama Tanesco na Mahindra ya India, mkataba mpya unaokuja TPA, bei ya mafuta nchini na mfumuko wa bei.

=======

Luhaga Mpina: Suala la uwekezaji wa Serikali na sekta binafsi linahitaji kuangaliwa kwa makini sana, mikataba mingi tuliyoingia inanyonya mapato ya nchi, uchumi wa nchi, inahamisha rasilimali, inapora ajira za watanzania.

Sasa hivi TPA nae ameanza kutafuta mbia, mikataba ya namna hii lakini ipo mikataba inayotusumbua mpaka sasahivi ya TRA na sicpa. Ipo mikataba tumeingia majuzi ya India Mahindra na Tanesco zaidi ya bilioni 70 kwaajili ya kuendeleza mifumo ya Tehama wakati wataalamu wa tehama tunao hapa wa kila aina wanaoweza kudevelop mifumo ya Tehama. Vijana wetu wamedevelop mifumo kama GPG, POS na hata Maxmalipo, leo unaenda kutafuta mfumo India kwaajili ya kufanya nini?

Sasa hivi naskia symbion wanapigiwa chapuo tuilipe bilioni 356 lakini inapigiwa hili chapuo wakati huohuo hatuambiwi alieingia mkataba huo na kutusababisha tuwe na mkataba ambao hatuwezi ku-exit hata kama mkataba unatuingizia hasara, amechukuliwa hatua gani?

Wabunge tukataeni mikataba ya namna hii lakini tukataeni hata kulipa hizi fedha, uchunguzi ufanyike kilichojificha nyuma ya Symbion.

Mikataba yote ambayo tunaitambulisha kama mikataba mibovu iitishwe hapa bungeni tuweze kuifuta.

Mwisho Luhaga Mpina ameongelea mfumuko wa bei nchini na kusema pamoja na Covid na vita lakini mfumuko umechangiwa na kukosekana uadilifu na usimamizi makini.

Mpina amesema upangaji holela wa bei kinachoshangaza kwanini wahusika hawajachukuliwa hatua. Amedai waziri anawajua waagizaji wa mafuta nje ya nchi, ngano na anawajua wazalishaji wa ndani ya nchi.

View attachment 2217807
Point tupu, Waziri ni mfanyabiashara mkubwa wa mafuta
 
Hauna akili wakat was JPM Kulikua na mfumuko Huu wa Maisha ? Ulisikia chokochoko za symbion??..

Tunakoelekea ,mtashangalia hata Hawa walozuiliwa mchanga madini, nao walipwe.

Tatizo Moja Tanzania, ni kukoswa watu wazalendo, Wenye uchungu na wafia nchi.

Mtu kama wewe, Hupaswi kupewa nafasi yoyote ile ya Kiongozi hata KAZINI kwako !!.

Maana Hautakua Productivity yoyote.
Tatizo la Tanzania ni mifumo mibovu ya CCM
 
Jamaa namuelewa ana pointi nyingi za msingi sana, ameamua kuweka maslahi ya taifa mbele hata kama yatagharimu ubunge wake mbele ya safari, huyu kwangu ndie mzalendo.

Watakaompinga nawashauri wampinge kwa kujibu hoja zake, sio zile kelele za wakati wake alifanya nini, kuendelea kujidumaza kwa majibu mepesi kama hayo ni kuliangamiza hili taifa.
Hata vitabu vitakatifu binasema kuwa, yeye atendaye mema, huku nafsini mwake ana dhamira chafu, Mungu hulitia unajisi jambo lile alilolitenda. Na kwa upande mwingine, mtu hata akafanya kosa, lakini wakati akifanya kosa hilo, alikuwa na dhamira njema nafsini mwake, Mungu hulitakatifuza kosa lile.

Mpina yawezekana anayoyasema yana ukweli wa kiwango fulani, lakini kutokana na dhamira yake chafu, na historia yake chafu, na kujishikiza kwake na wachafu hapo awali, hawezi kuaminika kwa lolote. Ni sawa na jambazi anayeuza kufuli akakuambia kuwa unastahili kutumia hizi kufuli imara ninazoziuza ili kujilinda dhidi ya majambazi. Lazima utapatwa na mashaka, hata kama unaziona kufuli anazoziuza ni imara.
 
Hauna akili wakat was JPM Kulikua na mfumuko Huu wa Maisha ? Ulisikia chokochoko za symbion??..

Tunakoelekea ,mtashangalia hata Hawa walozuiliwa mchanga madini, nao walipwe.

Tatizo Moja Tanzania, ni kukoswa watu wazalendo, Wenye uchungu na wafia nchi.

Mtu kama wewe, Hupaswi kupewa nafasi yoyote ile ya Kiongozi hata KAZINI kwako !!.

Maana Hautakua Productivity yoyote.
Mchanga gani wa madini uliozuiliwa? Tenganisha ukweli na ulaghai wa kisiasa uliokuwa ukifanywa na marehemu.

Kama ulizuiliwa, halafu nini kilichofuata? Umewahi kuiona ile MDA aliyoisaini Kabudi na Barrick? Ina nini cha maana, zaidi ya kuongeza tu mrabaha toka 4% mpaka 6%?

Nchi hii, kutokana na kuwa na wajinga wengi, ni rahisi sana kuyumbushwa na wanasiasa laghai.

Ukimwacha Nyerere na Mkapa, hakuna kiongozi mwingine aliyetengeneza mifumo ya kuboresha uchumi na utawala.
 
Jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la pembeni,matajizungusha weeee Kisha utatamka JPM
 
Mawazo chanya, fikira chanya, Mtazamo chanya na matumizi sahihi ya uongozi huyu ni aina ya kiongozi anayetambua wajibu wake
 
Shida ni kuwa akili za waTanzania zimelemaa kwenye ushabiki badalaya maslahi ya taifa yaani watu hawaangalii msingi wa hoja bali Wana angalia nani katoa hoja.......
 
Uzungumzii ndio kiswahili gani? Unataka niuzungumzie kukuridhisha wewe?
Mwamba umeuvaa uchama sijui unakufaidisha nini au unabadilisha nini kwenye maisha yako mambo zaidi inakufanya uwe na akili mgando, huo upuuzi wakushabikia vyama nashukuru Mungu akunipa
 
Hatujakuelewa unalalamika, unachangia au unatoa mada?????.Hebu jipambanue, this is GT avenue, acha blabla u kn. Jibuni hoja za Luhaga ak.a kibano
Mpina is a blind owl crying for the safety of spoiling rats beacuse he can no longer catch them.
 
Mpina yeye analalamika tu kutwa sijamsikia akija na solution, kasema inflation imetengenezwa sasa aseme aliyetengeneza nani? dhumuni nini? na solution ni nini? kuongea rahisi tu hawahawa hata siku moja wakati ule hakukuwa na hata mmoja kuuliza pesa inatoka wapi wakati ilikuwa inajulikana ni mikopo tena bank za kibiashara lakini kimyaa wote. unafiki kitu kibaya sana hata yule mbunge wa Mtera alisema sisi wanafiki mtu mmoja to Lazaro alisema wazi hawezi kufanya kazi na JPM wazi na akaondoka wengine wote wakae kimyaa wanafiki. Nakubaliana kitu kimoja Rais Samia ana watu wa hovyo katika baraza lake la mawaziri wa hovyo sana tu.

Sasa km unakubali baraza la mawaziri ni hovyo sasa hao si ndio wanaosimamia sera za serikali, nchi ikiwa inaenda ndivyo sivyo wakuulizwa ni nani…Mpina anyamaze tu kimya kisa kipindi cha nyuma hakuongea..

Kuhusu solution msikilize vizuri kuna mapendekezo ameyatoa yakitekelezwa tutasogea…lakini baraza lako hili unalosema itakuwa ni ndoto
 
Na huko Kenya, France, Marekani, UK n.k ambako kunaripotiwa mfumuko wa bei mkubwa kuwahi kushuhudiwa toka 2008, pia huo mfumuko umetengenezwa?

Vipi kuhusu wananchi Ulaya kutoruhusiwa kununua mafuta ya kula zaidi ya chupa moja nako kumetengenezwa na January Makamba na washirika wake?

Huyu mpuuzi Mpina si ndio inasemekana aliharibu maisha ya wavuvi wengi na kujimilikisha ekari nyingi kinyume na sheria hapo Morogoro? Huu uchungu na wananchi ameutoa wapi ghafla bin vuu?

Asifikiri anaweza kugombanisha wananchi na serikali halafu arukie kwenye hicho chama chao cha Umoja Party!

Huyu mjinga better he is reminded waliopo madarakani saivi wamekulia kwenye corridors of power. Wanajua mchezo wake wa mbuni kuficha kichwa chini huku kiwiliwili kikiwa nje!

View attachment 2217827

Aliaribu kivipi maisha ya wavuvi ebu tudadavulie….

Serikali igombane na wananchi mara mbili?!

Hao waliokulia kwenye corridors of power wanamiguu mingapi?!
 
hoja hii nayo i
Akichangia hotuba ya waziri wa viwanda na biashara, mbunge Kisesa, Luhaga Mpina ameongelea mambo mbalimbali ikiwemo uhusiano kati ya sekta binafsi na umma, mikataba mibovu ukiwemo wa Tanesco na Symbion, bilioni 70 za mkataba wa maendeleo ya tehama Tanesco na Mahindra ya India, mkataba mpya unaokuja TPA, bei ya mafuta nchini na mfumuko wa bei.

=======

Luhaga Mpina: Suala la uwekezaji wa Serikali na sekta binafsi linahitaji kuangaliwa kwa makini sana, mikataba mingi tuliyoingia inanyonya mapato ya nchi, uchumi wa nchi, inahamisha rasilimali, inapora ajira za watanzania.

Sasa hivi TPA nae ameanza kutafuta mbia, mikataba ya namna hii lakini ipo mikataba inayotusumbua mpaka sasahivi ya TRA na sicpa. Ipo mikataba tumeingia majuzi ya India Mahindra na Tanesco zaidi ya bilioni 70 kwaajili ya kuendeleza mifumo ya Tehama wakati wataalamu wa tehama tunao hapa wa kila aina wanaoweza kudevelop mifumo ya Tehama. Vijana wetu wamedevelop mifumo kama GPG, POS na hata Maxmalipo, leo unaenda kutafuta mfumo India kwaajili ya kufanya nini?

Sasa hivi naskia symbion wanapigiwa chapuo tuilipe bilioni 356 lakini inapigiwa hili chapuo wakati huohuo hatuambiwi alieingia mkataba huo na kutusababisha tuwe na mkataba ambao hatuwezi ku-exit hata kama mkataba unatuingizia hasara, amechukuliwa hatua gani?

Wabunge tukataeni mikataba ya namna hii lakini tukataeni hata kulipa hizi fedha, uchunguzi ufanyike kilichojificha nyuma ya Symbion.

Mikataba yote ambayo tunaitambulisha kama mikataba mibovu iitishwe hapa bungeni tuweze kuifuta.

Mwisho Luhaga Mpina ameongelea mfumuko wa bei nchini na kusema pamoja na Covid na vita lakini mfumuko umechangiwa na kukosekana uadilifu na usimamizi makini.

Mpina amesema upangaji holela wa bei kinachoshangaza kwanini wahusika hawajachukuliwa hatua. Amedai waziri anawajua waagizaji wa mafuta nje ya nchi, ngano na anawajua wazalishaji wa ndani ya nchi.

View attachment 2217807
hoja hii nayo iliishia wapi
 
Back
Top Bottom