Luhaga Mpina na Tundu Lissu, msiishie kwenye sukari tu, bali chunguzeni na biashara ya kukopesha mitandaoni

Luhaga Mpina na Tundu Lissu, msiishie kwenye sukari tu, bali chunguzeni na biashara ya kukopesha mitandaoni

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Hakika nawaambieni, hii biashara haramu ya kukopesha mitandaoni kwa riba kubwa tena kwa kutumia mitandao ya simu ya humu nchini pasipo wahusika kukamatwa, ni biashara ya vigogo kama ilivyo biashara ya kuagiza sukari.

Kama unabisha, wewe tengeneza App zako na uzitumie kufanya biashara haramu uone kama hutakamtwa ndani ya siku chache tu.

Fanyieni uchunguzi jambo hili, mtakuja kuniambia.

Huu urefu wa kamba huuu!!!
Riba za asilimia 35 mpaka 40 ndani ya siku 5 mpaka 6 kwa mamilioni ya watanzania masikini, ni moja ya biashara inayowalipa sana hawa watu na silaha yao kuu ni anaeshindwa kulipa anatangazwa mitandaoni.

Haya mambo ni possible tu kwenye nchi ambazo serikali ni lege lege ama corrupt.
 
Hakika nawaambieni, hii biashara haramu ya kukopesha mitandaoni kwa riba kubwa tena kwa kutumia mitandao ya simu ya humu nchini pasipo wahusika kukamatwa, ni biashara ya vigogo kama ilivyo biashara ya kuagiza sukari.

Kama unabisha, wewe tengeneza App zako na uzitumie kufanya biashara haramu uone kama hutakamtwa ndani ya siku chache tu.

Fanyieni uchunguzi jambo hili, mtakuja kuniambia.
Najiuliza
Rais wetu huwa anaelezwa ukweli yanayojiri au wanamuacha tu akumbane na ajali ya kisiasa mbeleni?
 
Ukiacha kuwa ni biashara ya riba kubwa,Lakini ni Biashara kichaka yakutakatisha pesa walizoiba washenz..i hawa.
Yaani wamejisajili kwenye mitandao ya simu(Mpesa, tigo pesa, n.k) wanafanya biashara haramu na hakuna anaekamtwa!!
 
Hakuna eneo wananchi wanapigwa kama hili, mobile loan ni tatizo kubwa Tanzania na halina weledi kabisa .. Imagine mtu anakopewa pesa kiduchu riba lundo ! Wakopaji wanafedheheshwa, wanazalilishwa, wananyanyasika .. Serikali ikomeshe huu wizi, sauti zaidi zipazwe. USTAWI LOANS Mr. Finance wanaongoza kuzalilisha watanzania kupitia hii mikopo haramu.
 
Kampuni za hovyo kabisa,hiyo ndio mikopo ya kausha damu
Riba ya asilimia 35 mpaka 40 ndani ya siku 7 na serikali ipo tu inaangalia. Shida za wananchi zisiwe chanzo cha kuwanyonyq hivi.
 
Hakika nawaambieni, hii biashara haramu ya kukopesha mitandaoni kwa riba kubwa tena kwa kutumia mitandao ya simu ya humu nchini pasipo wahusika kukamatwa, ni biashara ya vigogo kama ilivyo biashara ya kuagiza sukari.

Kama unabisha, wewe tengeneza App zako na uzitumie kufanya biashara haramu uone kama hutakamtwa ndani ya siku chache tu.

Fanyieni uchunguzi jambo hili, mtakuja kuniambia.
Wewe, mimi na wote wapenda haki tuendelee kulala.
 
Kuna jamaa alikopeshwa 100K kwa riba ya 32K ndani ya siku 14, ni ukichaa kwakweli.
Bora hiyo, kuna wanaolipisha riba kama hizo ndani ya siku 5 mpaka 6 humu kwenye mitandao. Haya makampuni yamejaa utapeli na wizi kuputia shida za watu.
 
juzi mama yake mshkaji kapigiwa simu eti kijana wake ni tapeli wa mtandaoni amlipie deni lake kabla hajatiwa nguvuni , bimkubwa alichanganyikiwa kinoma
 
Hii nchi sasa hivi kila mtu anajipigia... Msitegemee mtasikilizwa... Ukipata nafasi piga sehemu unayoweza maisha yaende... Otherwise kufa na uzalendo wako
 
Back
Top Bottom