Luhaga Mpina, shikilia hapohapo

Luhaga Mpina, shikilia hapohapo

Huyu jamaa ana Saka uwaziri tu hakuna jingine, akilipata Hilo atakua kma Bashiru na Polepole. Sijui kwanini waTanzania hatujifunzi tu juu ya Hawa wanasiasa wa CCM.

Kabisa, nashangaa wapinzani kuwasifia hawa wahuni wa CCM, hizi Hadaa za wañaccm ni kosa kubwa wapinzani kudanganyika. Huyo Mpina anatengenezwa hivyo ili kuonyesha kuna wañaccm wanaweza kuhoji matakwa ya wananchi. Lakini akipewa cheo leo hii hatahoji chochote cha maana. Wapinzani stukeni na huo usanii wa wanaccm.
 
Jamaa kwani zitto anataka kuwa nani kwenye siasa ? Yaani tuikatae hoja yake njema kisa ndoto zake usizozikubali. Na frankly speaking kila mtu anapambani tumbo lake regardless chama gani.

Hana hoja zozote, anafanya hivyo kuteka wajinga wasiojua kusoma between the lines.
 
Hujanielewa!! Mpina alikua mbunge machachari sana 2010-15 enzi hizo akiwa kamati ya Biashara/ mitaji na uwekezaji? ila baadae akapewa uwaziri na JPM akapoa... Akaacha kupigania maslahi ya wananchi bungeni yeye kazi yake ikawa ni kupongeza tu.

Cha kushangaza kakosa uwaziri ndio amegundua eti ndege zikikamatwa zitangazwe!! Kwamba Acacia watulipe matrillion yetu!! Kwamba malipo nje ya bajeti ni ufisadi ilihali mambo hayo pia yalifanyika kipindi Cha JPM ila alikaa kimya kulinda cheo.

Huyu ni mnafiki tu siku akipewa uwaziri atasema katiba mpya Haina ulazima na atasifia mikopo ya Samia.

Jifunzeni kwa Polepole wa awamu ya JK na awamu ya JPM!! alikana katiba mpya kabisa kwamba ni makaratasi ya kabatini tu
Mkuu 'zitto junior', kihelehele kinazidi kunipanda nijibu hoja zako kuhusu huyu jamaa Luhaga Mpina.

Niseme wazi, ni kazi ngumu sana kumtetea yeyote aliyeko, au aliyewahi kuwa ndani ya CCM (kasoro ya Mwalimu Nyerere, Moringe Sokoine, Rashid Kwawa, na wengine nisiowafahamu).

Lakini, inapokuja kuhukumu jumla jumla hivi kama tunavyofanya hapa, sisi wenyewe tunafanya makosa yaliyo wazi.

Kwa mfano: kutegemea Luhaga Mpina kuwa na msimamo tofauti nje ya serikali ambayo yeye alikuwa ni waziri ndani yake, hili siyo swala rahisi katika nchi zetu hizi za dunia ya tatu.
Hata kuwa mbunge, ndani ya chama, na kujipambanua kuwa tofauti sana na hoja zinazosimamiwa na serikali, hilo linahitaji ujasiri, na ni jambo la kuungwa mkono na walio nje ya mfumo wa serikali, badala ya kubeza juhudi hizo.

Umeeleza wewe mwenyewe hapo, kwamba historia ya huyu jamaa kisiasa, akiwa mbunge, alikuwa akisimamia na kuyasema aliyoona hayafai yanayofanywa na serikali yake. Binafsi, naona hii ni ishara ya mtu kuwa na msimamo juu ya jambo. Anayo anayoyasimamia, kama mwanasiasa.

Rekodi yake alipokuwa waziri, pia inaonyesha kuwa hakuwa mtu wa kukaa na kusubiri mambo yafanyike, bali alikuwa mshiriki.
Doa linalomwandama na mambo ya uvuvi, ni ishara tosha ya mtu anayelenga kufanya jambo linapoamriwa.

Hapa analumiwa, hasa kutokana na njia zilizotumika kushughulikia swala la uvuvi, uliokuwa ukifanyika kinyume cha taratibu zilizowekwa. Ni muhimu sana kusisitiza, hili lilikuwa ni tatizo la kutofuata taratibu uliofanywa na baadhi ya wavuvi.
Sijui, pengine pangekuwepo na njia nzuri za kushughulikia jambo hilo bila kuwaumiza walioumia, lakini mwanzo wa kuumia huko, ni kwamba kulikuwepo na ukiukwaji wa taratibu.

Kwa hiyo, mimi namwangalia Luhaga Mpina kwa matumaini. Hata kama hawezi kuhamia kwenye vyama vya upinzani, hususani CHADEMA, yumkini, hata huko ndani ya chama chake kuna watakaoweza kuungana naye na kutikisa huko huko wakiwa ndani ya chama chao. Hii itakuwa ni nafuu, siyo kwa wapinzani pekee, bali kwetu sote kama taifa.

Naendelea kumsikiliza kwa makini zaidi Luhaga Mpina anachozungumza huko Bungeni, na hata nje ya Bunge. Tumpe nafasi ya kujitofautisha na wengine ndani ya chama chake.
 
G55 ilianzishwa ndani ya CCM na lengo lake halikuwa kuvunja Muungano wala Serikali tatu bali kumdhibiti Dr. Salmeen Amour dhidi ya agenda yake ya kuipeleka Nchi Katika moja ya jumuia za kimataifa ambazo hazikuwa zinakubalika na Mhimili (OIC) na walipofanikiwa hilo kina Njelu kasaka wakaendelea na mambo mengine

hata zilipoanza vurugu za Richmond wachache sana ndio walielewa motive yake

napenda tu kukufahamisha kuwa Kamati kuu za Vyama vyote vikubwa asilimia zaid ya 70 wamejaa 'Mtu kazi'
Haya sasa ona 'spin' za aina yake zinavyoibuliwa kwa lengo maalum.

Hapa anapelekewa ujumbe mahsusi mwanzilishi wa mada; bila shaka akipewa tahadhari.

Kusema kundi la GG55 ndani ya CCM lengo lake lilikuwa ni tofauti na swala la Muungano ni kupindishi kuliko wazi kwa maksudi kabisa kwa lengo ulijualo mwenyewe.
Na bandiko linajieleza waziwazi lengo ni nini.
 
Haya ya kuhusu G55 kama ni uongo basi nimeusoma kwny kitabu cha Maisha ya Mzee Ally Hassan Mwinyi …kaeleza kwa kirefu sana na hata zogo hilo lilimalizwa baada ya kuwahakikishia Wenyewe kuwa Znz itajitoa kwny OIC
 
Sina ufahamu wa yaliyoandikwa ndani ya kitabu hicho; lakini ninauelewa wa mijadala iliyofanyika ndani ya Bunge wakati huo kuhusu jambo hilo..
Leo ndiyo mara ya kwanza kusikia likiunganishwa na maswala mengine mbali ya kudai serikali ya Tanganyika; na wala siyo kuvunja muungano.
 
kila siku tunasoma ili kupata jambo jipya na hakuna deadline ya kuelimika, ungekuwa ni msomaji wa vitabu ningekushauri usome kitabu cha Mzee Ally Hassan Mwinyi na cha Njelu Kasaka mwenye G55 , maana hawa ndio main Characters upate kufahamu yaliyokuwa nyuma ya pazia ya mjadala ule

kwenye Siasa kila jambo lina pande mbili , kuna namna lilivyosukwa ili jamii ilione kama ilivyokusudiwa na kuna lengo la kusukwa ili lionekane kama lilivyoonekana na Mimi ni mfukunyuku sana wa upande wa pili kwny saga zote za kisiasa …siku zikipita inshallah utajua lengo la pili la kuona hizi heka heka za hawa Wabunge baadhi walioanza kukosoa ghafla Serikali

ila pia una hiyari ya kuamini unachohisi ni sahihi pia
 
Shida haipo kwenye katiba.

Kwani katiba ya sasa inafuatwa ipasavyo?
 
Shida haipo kwenye katiba.

Kwani katiba ya sasa inafuatwa ipasavyo?

Iwapo katiba mpya itapatikana bila machafuko, huku chama kinachofaidika na katiba hii kikiendelea kuhodhi mchakato wa katiba mpya, tusitegemee hata hiyo katiba mpya kufuatwa kwa usahihi.
 
kila siku tunasoma ili kupata jambo jipya na hakuna deadline ya kuelimika, ungekuwa ni msomaji wa vitabu ningekushauri usome kitabu cha Mzee Ally Hassan Mwinyi na cha Njelu Kasaka mwenye G55 , maana hawa ndio main Characters upate kufahamu yaliyokuwa nyuma ya pazia ya mjadala ule

kwenye Siasa kila jambo lina pande mbili , kuna namna lilivyosukwa ili jamii ilione kama ilivyokusudiwa na kuna lengo la kusukwa ili lionekane kama lilivyoonekana na Mimi ni mfukunyuku sana wa upande wa pili kwny saga zote za kisiasa …siku zikipita inshallah utajua lengo la pili la kuona hizi heka heka za hawa Wabunge baadhi walioanza kukosoa ghafla Serikali

ila pia una hiyari ya kuamini unachohisi ni sahihi pia
Binafsi ni muumini wa 'adage' "elimu haina mwisho"; na elimu haina sehemu moja tu inakopatikana, i.e, vitabuni. Siku hizi elimu inapatikana sehemu mbalimbali zaidi ya vitabuni pekee.

Mzee Mwinyi, au Njelu Kasaka wanapoandika vitabu vyao, ni wazi wanaweka 'perspective' zao na maoni yao hayawezi kuwa ndio ukweli sahihi wa mambo; kama ilivyo, kwako msomaji, kama unasoma ukiwa umejiandaa kupokea maoni yao kuwa ndio ukweli au la.

Hili unalosema la wabunge kwenda kuigiza Bungeni, kwa kuwasilisha jambo huku wakilenga jambo lingine lililo pembeni, hii ndiyo 'spin' niliyoizungumzia hapo mwanzo.
Ni wewe msikilizaji unayeweka tafsiri jinsi unavyoona wewe inakufaa kwa jambo husika, hasa ukiwa na malengo yako unayotaka yawe.

Mjadala Bungeni uliowahusu G55 ulikuwa wazi kama ulivyoongelewa Bungeni na watu kuushuhudia. Uwepo wa tafsiri nyingine kuhusu mjadala huo, hilo ni jambo la mtu binafsi kufuatana na hisia zake mwenyewe.
 
Back
Top Bottom