Hujanielewa!! Mpina alikua mbunge machachari sana 2010-15 enzi hizo akiwa kamati ya Biashara/ mitaji na uwekezaji? ila baadae akapewa uwaziri na JPM akapoa... Akaacha kupigania maslahi ya wananchi bungeni yeye kazi yake ikawa ni kupongeza tu.
Cha kushangaza kakosa uwaziri ndio amegundua eti ndege zikikamatwa zitangazwe!! Kwamba Acacia watulipe matrillion yetu!! Kwamba malipo nje ya bajeti ni ufisadi ilihali mambo hayo pia yalifanyika kipindi Cha JPM ila alikaa kimya kulinda cheo.
Huyu ni mnafiki tu siku akipewa uwaziri atasema katiba mpya Haina ulazima na atasifia mikopo ya Samia.
Jifunzeni kwa Polepole wa awamu ya JK na awamu ya JPM!! alikana katiba mpya kabisa kwamba ni makaratasi ya kabatini tu
Mkuu 'zitto junior', kihelehele kinazidi kunipanda nijibu hoja zako kuhusu huyu jamaa Luhaga Mpina.
Niseme wazi, ni kazi ngumu sana kumtetea yeyote aliyeko, au aliyewahi kuwa ndani ya CCM (kasoro ya Mwalimu Nyerere, Moringe Sokoine, Rashid Kwawa, na wengine nisiowafahamu).
Lakini, inapokuja kuhukumu jumla jumla hivi kama tunavyofanya hapa, sisi wenyewe tunafanya makosa yaliyo wazi.
Kwa mfano: kutegemea Luhaga Mpina kuwa na msimamo tofauti nje ya serikali ambayo yeye alikuwa ni waziri ndani yake, hili siyo swala rahisi katika nchi zetu hizi za dunia ya tatu.
Hata kuwa mbunge, ndani ya chama, na kujipambanua kuwa tofauti sana na hoja zinazosimamiwa na serikali, hilo linahitaji ujasiri, na ni jambo la kuungwa mkono na walio nje ya mfumo wa serikali, badala ya kubeza juhudi hizo.
Umeeleza wewe mwenyewe hapo, kwamba historia ya huyu jamaa kisiasa, akiwa mbunge, alikuwa akisimamia na kuyasema aliyoona hayafai yanayofanywa na serikali yake. Binafsi, naona hii ni ishara ya mtu kuwa na msimamo juu ya jambo. Anayo anayoyasimamia, kama mwanasiasa.
Rekodi yake alipokuwa waziri, pia inaonyesha kuwa hakuwa mtu wa kukaa na kusubiri mambo yafanyike, bali alikuwa mshiriki.
Doa linalomwandama na mambo ya uvuvi, ni ishara tosha ya mtu anayelenga kufanya jambo linapoamriwa.
Hapa analumiwa, hasa kutokana na njia zilizotumika kushughulikia swala la uvuvi, uliokuwa ukifanyika kinyume cha taratibu zilizowekwa. Ni muhimu sana kusisitiza, hili lilikuwa ni tatizo la kutofuata taratibu uliofanywa na baadhi ya wavuvi.
Sijui, pengine pangekuwepo na njia nzuri za kushughulikia jambo hilo bila kuwaumiza walioumia, lakini mwanzo wa kuumia huko, ni kwamba kulikuwepo na ukiukwaji wa taratibu.
Kwa hiyo, mimi namwangalia Luhaga Mpina kwa matumaini. Hata kama hawezi kuhamia kwenye vyama vya upinzani, hususani CHADEMA, yumkini, hata huko ndani ya chama chake kuna watakaoweza kuungana naye na kutikisa huko huko wakiwa ndani ya chama chao. Hii itakuwa ni nafuu, siyo kwa wapinzani pekee, bali kwetu sote kama taifa.
Naendelea kumsikiliza kwa makini zaidi Luhaga Mpina anachozungumza huko Bungeni, na hata nje ya Bunge. Tumpe nafasi ya kujitofautisha na wengine ndani ya chama chake.