Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina, ametoa wito kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumtaka Waziri wa Fedha kuidhinisha utoaji wa taarifa zote zinazohusu mikopo, mamlaka za rufani za kodi, misamaha ya kodi pamoja na mamlaka za uchunguzi.
Mpina amesisitiza umuhimu wa taasisi kama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kufanya uchunguzi wa kina kuhusu uadilifu wa matumizi ya fedha za umma na ukwasi (Utajiri) wa baadhi ya Viongozi wa Serikali na kufichwa kwa Taarifa za miamala shuku
Amesema ni wakati wa kuweka wazi taarifa zote kwa manufaa ya umma, hasa katika kipindi ambacho matumizi ya fedha za serikali yanapaswa kuwa wazi na yenye tija kwa maendeleo ya wananchi.
Chanzo: Jambo TV